Mbeya: Wananchi wenye hasira wachinja hadi kuua watoto wawili wa Diwani wa CCM

Mbeya: Wananchi wenye hasira wachinja hadi kuua watoto wawili wa Diwani wa CCM

Mkuu watendee haki mende,

Unajua mende wa ufilipino na mashariki ya mbali wanaweza kujua tetemeko la ardhi siku tano kabla ya tukio. Mende wana akili mkuu.

Nashukuru mkuu kwa mchango mzuri
 
Chama cha Mizigo, madiwani wa maCCM wanakuwa na matatizo gani?

Wangelipiza kwa diwani husika, "wangemmabina" kwa watoto wake wamekosea sana japo ujumbe umemfikia akiwa hai.

Poleni wafiwa ila huyo diwani wammabina fasta...

acha wawanyoshe mpaka na wao roho ziwaume
 
Kuna JIRANI yangu kafumaniwa akiwa na make wa JIRANI yake!
Lazima itakuwa mambo ya siasa.
Waltz mmekuwa wajinga sana. Kila uhalifu mnauchanganya na siasa
 
Acha kushabikia ujinga.

Wewe uliposhabikia kwa kusema Pale Soweto CDM wamejilipua wenyewe ulikuwa unamaanisha nini je wale waliokufa haukuona kama ni binadamu? na hata juzi sikuona wewe ukisikitika kwa MABINA kumuua yule kijana wa miaka 12 bali ulisikitika kwa mabina kupigwa mawe hadi kufa na ukilaumu eti wamejichukulia sheria mkononi na kulaani kwa nguvu zote NGUVU YA UMMA Tambua kuwa MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.
 
Mkuu wangu Idawa nadhani kuna sehemu unachanganya mambo, hasa kwenye heading...

Watu wasiojulikana hawawezi kuwa wananchi wenye hasira...Wananchi wenye hasira ni kama wale wa Kisesa-Magu waliomponda kwa mawe Clement Mabina hadi kuuawa...

Na hao wa Tunduma kama walikuwa na hasira na Diwani aliyewadhulumu wangemshambulia yeye na kumdhuru lakini si kuvizia baba na mama hawapo kisha wanamchinja mtoto mdogo wa umri wa miaka 6 na kumnyonga kwa waya msichana wa kazi...Kimsingi aliyechinjwa ni mtoto mdogo wa miaka 6 na aliyenyongwa ni msichana wa kazi wa Diwani huyo...

Si vibaya ukaweka heading kuwa 'Watu wasiofahamika wawaua watoto wawili wa Diwani wa CCM'...

Kipindi cha MUSA na FARAO aliyekufa ni mtoto wa farao siyo farao.
kimsingi inauzi kwa viongoz tuliowaamin kati ya watu wengi wanaangalia familia zao tu, haya sasa familia ndo hiyo inanyongwa.
siyo kitendo kizuri kukatisha uhai wa mtu hata kama umeumizwa sana.
 
Wewe uliposhabikia kwa kusema Pale Soweto CDM wamejilipua wenyewe ulikuwa unamaanisha nini je wale waliokufa haukuona kama ni binadamu? na hata juzi sikuona wewe ukisikitika kwa MABINA kumuua yule kijana wa miaka 12 bali ulisikitika kwa mabina kupigwa mawe hadi kufa na ukilaumu eti wamejichukulia sheria mkononi na kulaani kwa nguvu zote NGUVU YA UMMA Tambua kuwa MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.
Kwani CHADEMA kujilipua ndiko kungezuia wanachadema kufa? Bomu halina Macho! Wahuni wachache wa CHADEMA waliamua kufanya hivyo wakidhani kuwa ndio kukuza Chama, Mauaji dhidi ya watanzania na binadamu wengine yakemewe kwa NGUVU zote.
 
Japo siipend ccm lakini kwa hili la kuchinja watoto wadogo siafikiani nalo kbs, wahusika wachukuliwe hatua
 
Namwonea huuruma rais

sijui mpaka january atakuwa ametoa rambi rambi ngapi
 
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Wapumbavu kabisa hawa. hao watoto ndio waliochukua ardhi?:A S cry:
 
Sasa tumegeuka wanyama wa mwituni. Sasa kama wakiua watoto ndo viwanja vinarudi na kesi wanashinda? Tubadilike watanzania. Sifa yetu ya amani inatibuka polepole
 
Hizi ni dalili za kuchoshwa hasa pale vyombo vya usalama vinapokuwa havitendi haki

Hamna kitu hapo. Hao ni vichaa tu!
Utauaje mtu hata hati ya viwanja haijui? Thamani ya mwanadamu imekuwa viwanja kweli?
Tanzania inakuwa outdated kwa kasi sana!
 
Watu wasiojulikana wamewaua watoto wawili,mmoja akiwa ni binti wa kazi wa Diwani wa CCM kata ya Mkingamo wilaya Momba mkoani Mbeya.

Chanzo cha mauaji inasemekana ni dhuluma ya viwanja kwa wananchi wa kawaida.

Habari zaidi zinasema kawadhurumu wananchi viwanja vingi sana,wakati mwingine huuza kiwanja kimoja kwa zaidi ya watu watatu.
Inasemekana hata ukimpeleka mahakamani anakushinda kesi,kifupi ni kuwa mahakama aliiweka mfukoni.

Hali hii inalipeleka kubaya taifa letu. Itafika kipindi hali itakuwa tete na zaidi wananchi wakiona haki yao inapotea bila mtetezi ujue watatafuta njia mbadala....
 
Vipi nawe ni tapeli wa viwanja vya raia?

Jamani tujulishane wapi bastora,gobole zinauzwa.nimechoka kusikia habari za hawa manyang'au
 
Mkuu wangu Idawa nadhani kuna sehemu unachanganya mambo, hasa kwenye heading...

Watu wasiojulikana hawawezi kuwa wananchi wenye hasira...Wananchi wenye hasira ni kama wale wa Kisesa-Magu waliomponda kwa mawe Clement Mabina hadi kuuawa...

Na hao wa Tunduma kama walikuwa na hasira na Diwani aliyewadhulumu wangemshambulia yeye na kumdhuru lakini si kuvizia baba na mama hawapo kisha wanamchinja mtoto mdogo wa umri wa miaka 6 na kumnyonga kwa waya msichana wa kazi...Kimsingi aliyechinjwa ni mtoto mdogo wa miaka 6 na aliyenyongwa ni msichana wa kazi wa Diwani huyo...

Si vibaya ukaweka heading kuwa 'Watu wasiofahamika wawaua watoto wawili wa Diwani wa CCM'...

Ndo tumefikia hapa??
 
huo ni ujumbe tosha kwa huyo diwani kwamba BADO YEYE-- baada ya watoto kuuawa, itafuata zamu yake--hili ni funzo zuri sana kwa mafisadi wenye tabia kama zake.

Bado Dr Slaa na Mbowe wanaochochea watoto wa wenzao wafe wapate mtaji wa Siasa,KIGOMA wameshindwa kuchochea au kutekeleza mauaji na kusingizia POLISI

Moderator please usiitoe hii,please be fair
 
Juma lililopita tu, a prominent party leader alimuua kijana na bastora alafu naye akauawa. Nilichosikia ni kuwa waliomuua ni 'wananchi wenye hasira' huku nikiwa sina uhakika kama naye 'alikuwa na hasira' kwa kumuua kijana!
Sasa wale wanaosema 'ni upepo tu utapita' mbona huu wa sasa unaonekana kuwa na nguvu kali hata zaidi ya tufani!?
Tunaelekea kubaya ambapo muda sio mrefu tutashindwa hata kusimulia maana tunavichekea vyanzo vya matatizo kwa kudhani kuwa tutatatua matatizo yenyewe1

Viongozi wetu watambue kuwa amani Tanzania ilikuwepo kwakua ardhi ilikuwa accessible to all. Raia wengi kwakutokuwa informed walishindwa kuunganisha ufukara wao na serikali. Wengi walikuwa na perception kuwa it was there problem kwani ardhi wanayo so aliyekuwa fukara ilikuwa ni kwa uzembe wake.

Siasa zetu enzi hizo zilitoa picha hiyo. Kwa sasa population imeongezeka mno na wachache wetu wenye position na income power wamejimegea maeneo makubwa tena waki wa relocate wenyeji. Hii inatokea kutokana na kuwa vijiji vingi havija sajiliwa na havina hati ya ardhi ya vijiji vyao so kisheria kweli wanakuwa na uhalali wa kumiliki ardhi hizo. Lakini tukumbuke bado watanzania wamezoea customary right ambayo ikiwa formalised inakubalika kuwa ni legitimate; lakini nyingi za hizo rights hazina deed so hawa mafisadi ardhi wanatumia hiyo loop hole against informal setting ambayo japo kisheria siyo halali kama haijawa certified ila kwenye communities bado zinatambulika. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Sasa serikali inatambua kuwa haijazipatia vijiji vingi certificate kutokana na financial constraint, sasa iweje viongozi hao hao ambao wanatakiwa kuzilinda hizo right on behalf of communities mpaka hapo zitakapo rasimishwa wawageuke watu wao? Kwanini serikali isitafute njia za kisheria kuwabana hao viongozi wa jinsi hiyo ili kukomesha hii tabia? Adhabu ya kiongozi itofautishwe na raia wa kawaida mpaka tutakapo kubali kuwa cheo ni dhamana!

Sera ya Ardhi Tanzania kungekuwa na social capital ni nzuri sana kwani inatoa fursa kwa kila mtu kupata ardhi lakini hao custodians wa hizo right ndiyo ambao wameigeuza sera hiyo ku confiscate ardhi za raia badala ya kuilinda kwa niaba yao ili iwe accessible kwa kila mtu.

Kuhusu wafugaji na wakulima tatizo lipo kwa wataalam wetu wa mipango ardhi pamoja na local government. Kusema ukweli hawa watu wanategemeana kama tungekuwa na mipango mizuri. Kwamfano kuna informal arrangement kati ya wafugaji na wakulima kuhusu kulisha mifugo mazao yakiwa shambani. Mipango hii imegeuza na watendaji kichaka cha kuwanyonya wakulima na wafugaji hukuwakiwachonganisha badala ya kuwasaidia waweze kuishi kwa kufaidishana. Pia attitude ya wakulima wetu kudhani mazao ya kulima ni mahindi na maharage tu? Hata kama ikiwa hivyo bila kutambua kuwa hayo mazao pia ni chakula cha mifugo na si lazima yaliwe na binadamu tu swala la soko kuwa tatizo lisingekuwepo. Wataalamu nao badala ya kuwasaidia wanakuza migogoro hiyo kwakutokuwa na suluhisho sahihi la matumizi bora kwaaajili ya kufuga na kulima mazao. Ifahamike pia majani ya kulishia mifugo ni zao pia na usingetegemea maeneo kama Hedaru watu kulima mahindi badala ya majani ambayo yanaweza hata kusafirishwa kwa kupakiwa vizuri kama mazao mengine yakawafikia.

Mimi na vijana wenzangu ambao ndiyo kwanza tunaanza kulitumikia Taifa letu tupo na mipango mingi ya kuleta majibu katika maswali magumu kama haya. Pengine hatutaweza kulimaliza kwa haraka bali tunamipango ya kujenga mifumo itakayo punguza kero hizi kwakiasi kikubwa. Wengine wetu wataingia kwenye siasa, wengine tutabakia watumishi wa umma na wengine watajiunga na communities zetu sehemu mbalimbali nchi nzima ili hatimaye tuweze kuleta impact!

Kwakua tuna nia na tunaamini katika Mungu, tutaweza tu!
 
Back
Top Bottom