Mbeya: Watu wanne (4) mbaroni kwa kufurahia kifo cha Rais Magufuli kwa kupika supu na kununua lita 20 za Ulanzi

Mbeya: Watu wanne (4) mbaroni kwa kufurahia kifo cha Rais Magufuli kwa kupika supu na kununua lita 20 za Ulanzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia Watu wanne kwa tuhuma za kufurahia kifo cha hayati John Magufuli kwa kupika supu na kununua ndoo ya lita 20 ya pombe ya kienyeji ya Ulanzi.

Pia soma > Manyara: 8 mbaroni kwa kushangilia kifo cha Magufuli



Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia Watu wanne kwa tuhuma za kufurahia kifo cha hayati John Magufuli kwa kupika supu na kununua ndoo ya lita 20 ya pombe ya kienyeji ya Ulanzi

RPC wa Mbeya, Urlich Matei amesema ni jambo la kushangaza kwa baadhi ya Watu kufanya vitendo hivyo huku Nchi ikiwa kwenye maombolezo ya siku 21
 
Ila polisi wetu kuna wakati wanafanya vitu kama hawana akili ya kufikiri vile! Sijui wana ugonjwa gani hawa viumbe! Hivi wana ushahidi gani hasa kama hao watu wanafanya sherehe kwa sababu magufuli kafa?

Na kwa nini kila mtu alazimishwe kuomboleza? Maombolezo siku zote ni kwa wale wafiwa tu! Na ndiyo maana mkiwa msibani (nyumbani/makaburini) utakuta watu wengine wanalia/wana nyuso za huzuni, huku wengine wakipiga tu stori na kucheka, Kana kwamba hakuna kilicho tokea vile!

Huo ndiyo msiba. Huwa nawashangaa sana hata hawa MATAGA waliopo humu! Yaani wanataka wote tulie na kuomboleza pasipo na sababu yoyote ile ya msingi! Wamesahau maombolezo hutokea kwa wafiwa tu, au wale walio guswa na msiba.
 
Back
Top Bottom