Ila polisi wetu kuna wakati wanafanya vitu kama hawana akili ya kufikiri vile! Sijui wana ugonjwa gani hawa viumbe! Hivi wana ushahidi gani hasa kama hao watu wanafanya sherehe kwa sababu magufuli kafa?
Na kwa nini kila mtu alazimishwe kuomboleza? Maombolezo siku zote ni kwa wale wafiwa tu! Na ndiyo maana mkiwa msibani (nyumbani/makaburini) utakuta watu wengine wanalia/wana nyuso za huzuni, huku wengine wakipiga tu stori na kucheka, Kana kwamba hakuna kilicho tokea vile!
Huo ndiyo msiba. Huwa nawashangaa sana hata hawa MATAGA waliopo humu! Yaani wanataka wote tulie na kuomboleza pasipo na sababu yoyote ile ya msingi! Wamesahau maombolezo hutokea kwa wafiwa tu, au wale walio guswa na msiba.