Mbeya: Watu wanne (4) mbaroni kwa kufurahia kifo cha Rais Magufuli kwa kupika supu na kununua lita 20 za Ulanzi

... lakini Mkuu kumbuka walipofariki hao uliowataja, kipindi cha maombolezo ya misiba yao, hapakuwa hata na "sisimizi" aliyedhurika! Lakini yule mwingine ilitolewa taarifa, tena taarifa rasmi, kwamba "kasindikizwa" na makumi wakitoa heshima zao; wakaongozana naye! Unadhani nani alikuwa "mtu wa watu" zaidi?
 
Msiba wa mtu wa Mungu huambatana na heri nyingi. Msiba wa laana huambatana na maafa mengi.
 
Ninao Ushahidi wa watu kadhaa kukamatwa maeneo ya Mwanjelwa Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuhisi tu kwamba Wali wao waliopika pamoja na vinywaji vyao walivyokunywa kwa pamoja eti ilikuwa ni kushangilia kifo cha Dr Magufuli , jambo ambalo halijawahi kuthibitishwa na yeyote , na bila shaka kutokana na hulka za Jeshi la polisi Tanzania kuna Wahanga wengine waliobambikwa kusherehekea jambo hili maeneo mengine kama ilivyo ada .

Sisi ambao hatukukamatwa na bado tuko uraiani tusinyamaze na kujisahaulisha kuhusu uonevu huu wa jeshi la polisi , tupige kelele watu wale waachiliwe mara moja na walipwe fidia kwa kupotezewa muda wao kwa tuhuma za uongo , binafsi kwa muda wa mwezi mzima tangu jambo lile litokee nilipika nyama kwa kificho ili nisiambiwe nasherehekea , huku ndiko nchi yetu ilikofikishwa , Ajabu na aibu sana !
 
Mbona nyama choma waliagiza wengi sana,mbona kwenye familia nyingi kukiwa na msiba wanachinja ng'ombe kama mboga.Sasa intelijensia iliona huko mby tu?
 
Mbona nyama choma waliagiza wengi sana,mbona kwenye familia nyingi kukiwa na msiba wanachinja ng'ombe kama mboga.Sasa intelijensia iliona huko mby tu?
Kwetu Babu akifa, wajukuu wanasherehekea, miziki na nyama choma
 
Kwani hapo Hotel Desderia hakumshangilia? Maana mlijua kiboko ya wazembe na mafisadi ametoweka.
 
wewe unaongea kama nani, na hatuwaachii pumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…