Mwanasiasa mtata
JF-Expert Member
- Oct 25, 2022
- 1,520
- 3,781
Swali gumu sana kwa maccm. Wanaogopa kusema mkataba kwasababu una mapungufu mengi. Na wanaogopa kusema ni makubaliano kwa sababu makubaliano hayawezi kijadiliwa na bunge, sasa kazi kwao na inakuwa ile slogan ya ukimung'unya mchale na ukitema mchale🤣🤣Nadhani, kwa maoni yangu issue ya kwanza ni JE IGA NI MKATABA AU NI MAKUBALIANO?
kwa maana hiyo huo ni Mkataba haramu => Haukidhi matakwa ya kisheria.Mdude mawakili wako wote wamekubali hakuna mkataba; kwa maana hiyo serikali iko sahihi kwa kusema kilichopo ni makubaliano
mkataba kati ya Tanzania na Dubai uliohusu rasilimali za Tanzania bila kushirikisha wananchi na kupitishwa bungeni ilikinzana na ibara 1,8,18(d), 21[2] 27 ya katiba ya Tanzania 1977, Na kifungu kifungu 11[1][2][3] na kifungu cha 12 cha sheria ya mali asili, sheria na. 5 ya mwaka 2017.
mkataba huo unavifungu 6(2) 7[2], 23[4] kinaathiri Usalama wa nchi, uhuru wa nchi na kuhatarisha usalama wa rasilimali za nchi kwa kuwa inakinzana na ibara ya 1,8,18(d) 28 ya Katiba ya Tanzania
Na kwamba waleta maombi Wanaomba tamko la mahakama kwamba vifungu vyote vinavyoathiri usalama wa taifa, rasilimali za nchi na uhuru wa nchi. Viondolewe.
lengo la notice ni kusaidia katika uchambuzi wa Mkataba husika
Mkataba huu unahusu, sea port, lake port na economic zone na inahusisha maeneo yote ya nchi na ilipaswa kuwahusisha watu wa kanda za maziwa katika hili.
Bila kuzingatia kanuni ya haki ya asili ni kitendo kibaya na wananchi hawakuhusishwa.
kitendo hiki ni kitendo batili.
sheria za kimataifa zinatambua haki yetu ya jamhuri katika permanent sovereignty ya kufaidi, kutumia maliasili yake
inaeleza Mamlaka na nguvu ya watu ya kuhakikisha kwamba mipango yote, makubaliano yote yanalinda maslahi ya watu na jamhuri yetu
inaeleza kusudio la kuweka sheria madhubuti ili kuhakikisha umiliki, udhibiti wa Rasilimali asili na kulinda ukuu wa nchi kuhusiana na mali asili zake.
migogoro inayotokana na suala la rasilimali zetu itaamuliwa na mahakama au chombo chochote kilichotebgenezwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania
kinakataza kabisa
kusikilizwa na kuamuliwa na sheria za kigeni na mahakama za kigeni.
mkataba utakuwa na changamoto dhidi ya ukuu wake (Sovereignty) kama unapendelea wawekezaji wa nje na kuzipa nguvu sheria husika, maana yake mkataba huo ni tata
Adv. Mwabukusi: Kifungu hiki kinaondoa ukuu wa nchi katika kufaidi rasilimali za nchi kama sheria zote mbili nilizotaja hapo juu na kuipa Dubai mamlaka Quote ibara 4(2). Kifungu hiki 4(2) kinainyima nchi yetu kuachana na haki ya kutafuta fursa kwingine zaidi ya Dubai hivyo kukinzana na sheria zote
ibara ya 21 ya IGA, inakinzana na Sovereignty ya nchi yetu.
migogoro ya rasilimali za nchi kwa kutumia mahakama za ndani na sheria za ndani. Lakini kifungu cha 21 kimeondoa hayo mamlaka.
Kifungu cha 23[4] cha IGA kinaondoa kabisa ukuu wa nchi [sovereignty )
Tutawasilisha kwamba mkataba huu hauna sifa za kisheria za kuwa mkataba.
Mkataba huu unahusu uwekezaji lakini haujaambatishwa na nyaraka yoyote au kifungu chochote kjnachoonyesha, huyu DP WORLD anawekeza kiasi gani.
Hakuna kjnachoonyeshwa anawekeza nini au kiasi gani zaidi ya kueleza kitu anachopewa
This is serious illegality juu ya uhalali wa Mkataba.
Ibara 123 ya Katiba ya umoja wa kiarabu (Quote) kinaeleza bayana kwamba: mshiriki wa umoja wa kiarabu atathibitisha makubaliano na nchi nyingine na makubaliano husika kama hayata kinzana na maslahi ya umoja.
DP WORLD hawana capacity to contract na hakuna instrument yoyote ambayo DP World imeruhusiwa na umoja wa kiarabu kufanya makubaliano na Tanzania.
Montevideo Convention inatoa sifa ili nchi uweze kutambukika
kufanya makubaliano
DUBAI haina hiyo capacity
DP WORLD sio competent by virtue of Section 2,10,11(1] of the law of contract.
kukosekana kwa issue hizo kunathibitisha mkataba huu ni batili. Its void abuinitial.
tunaiomba mahakama yako tukufu kuuondoa mkataba huu.
Ukuu wa Katiba ya nchi dhidi ya huu mkataba wa IGA.
kuishi kwa mazingatio ya katiba ya nchi hakutakiwi kuchukuliwa kama utumwa bali ni wokovu.
mkataba wa IGA umekiuka vifungu katika ibara ya 1, 8,28(1)(3) ya Katiba ya Tanzania.
ibara 4[2) ya IGA Inayoeleza scope of cooperation na kutoa wajibu katika serikali ya JMT kuwa agent wa Dubai mwenyejukumu la kuifahamisha dubai kila fursa nyingine za bandari.
Tunaomba mahakama ione kwamba ibara husika ya IGA inavunja katiba na tunaomba mahakama itoe tamko kuwa inavunja katiba ya nchi.
kutoa exclusive rights kwa DP WORLD ni kuikosesha nchi yetu kujilinda na kulinda
hakuna hata reservation rights.
mahakama ione kwamba kifungu 5(1) kinakiuka ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania na ione kwamba hiyo ni sababu ya kubatilisha mkataba wa IGA.
ibara 6(2] ya IGA (Quote as its) serikali ya Tanzania imezuiwa constructively kuingilia sehemu ya DP WORLD
Ibara hii inavunja ibara ya 28 ya katiba ya Tanzania na kwakuwa Katiba imetoa wajibu wa chi kama nchi huru na kifungu hiki ni kuifanya nchi iingie kwenye changamoto kubwa za kiusalama.
Ibara 8(1] a,b,c ya IGA, ibara 8[2], 10[1), 23[3][4], 26,27 inakiuka ibara ya 1,8 na ibara 28 ya Katiba ya Tanzania
zinakusudia kuendekeza vitendo vya uvamiz
inatoa mianya ya uvamizi
Tunailika mahakama yako ione kwamba ibara ya .. ina prejudice haki ya watanzania waliopewa wajibu wa kushiriki katika masuala yanayowahusu.
Hebu fungua fuvu hilo kijana,...huoni kama walitaka kutufanya watoto kwa ku kudanganyia pipi?Nadhani, kwa maoni yangu issue ya kwanza ni JE IGA NI MKATABA AU NI MAKUBALIANO?
Huko 'Vienna' ndiko wanakokubali mambo ya kipuuzi yakiwekwa kwenye Mkataba?Walichokosea mawakili wasomi, hata Jaji mwenyewe ni kutumia sheria za ndani kutafasiri mkataba wa kimataifa (International Treaty). Sheria ziko wazi kabisa, kwamba mikataba ya kimataifa inatafasiriwa kupitia Vienna Convention on the Law of Treaties 1969. Huwezi kutumia The Tanzania Law of Contract Act, hata siku moja.
Ile IGA ni mkataba wa kimataifa, na HGA ndiyo mkataba wa utekelezaji ambao ungesimamiwa kwa sheria za ndani ya nchi na zile za kimataifa (Hybrid Legal Dichotomy) kwenye suala zima la usuluhishi. Hilo limewekwa wazi hata kwenye Stabilisation Clauses za kwenye IGA.
Mama amekuwa kiburi kwasababu mali inakwenda kwa wajomba na kama yeye hakuna anachopoteza.kesi hii mwabukusi na wenzake hakika watashindwa, hata kabla hawajapeleka walijua wanapeleka ila watashindwa. hata hivyo, naamini wao lengo lao hata halikuwa kushinda, ila walilenga kupaza sauti nchi yote na nje ya nchi ijue kuwa watanganyika hii kitu wameikataa, na washinde au washindwe hiyo itabaki alama itakayowahukumu viongozi wa serikali milele, wajukuu wetu watakuja kuwanyooshea vidole kwamba hamkusikiliza kelele za wananchi na hata kesi ilipofunguliwa bado hamkusikia. kwasababu hio, washinde, wasishinde kwao ni ushindi tu kwasababu wamefanikiwa kufikisha ujumbe na kupambana pale mkono unapofika. hadi sasa wameshashinda kwasababu lengo lao limeshatimia ambalo halikuwa kushinda kwenye makaratasi bali kushinda kwa kufikisha kilio cha watanganyika walio wengi. wametumia uwezo wao wote kuzuia dp world, at least they have done something, and we should appreciate what they are doing.
Hata mimi nimemshangaa huyu jamaa. Hajasoma hata Utangulizi wa Mawakili wa Wananchi wametaja rejea ipi!Unafahamu kinachojadiiwa hapo Mahakaman???? Maccm bure kabisa
👍👍🙏Swali gumu sana kwa maccm. Wanaogopa kusema mkataba kwasababu una mapungufu mengi. Na wanaogopa kusema ni makubaliano kwa sababu makubaliano hayawezi kijadiliwa na bunge, sasa kazi kwao na inakuwa ile slogan ya ukimung'unya mchale na ukitema mchale🤣🤣
Moja ya element ya mkataba ni consideration.Kwenye huo mkataba hakuna hiyo.Ndiyo maana mawakili wametumia LCAHuko 'Vienna' ndiko wanakokubali mambo ya kipuuzi yakiwekwa kwenye Mkataba?
Sheria zetu zinapingana na hiyo 'Vienna' au vipi?
Naelewa nachokiongelea, huyo wakili Mwabukusi ni mwanasiasa tu aliyeshindwa ubunge 2020 anatafuta kutoka upya 2025.Hapa utakuwa umechanganya mafile Mzee, huu siyo uchaguzi, ni kesi inayohusu Bandari!
Mlalamikiwa na 4 mnamo tar 5 June 2023 saa saba mchana alitoa taarifa kwa umma kutaka umma ufike kwa ajili ya public hearing kesho yake 6 June 2023 (masaa 24) tu. Masaa 24 tu wananchi walitakiwa kwenda ukumbi wa msekwa bungeni kutoa maoni. Tangazo hilo halikuambatana na Mkataba wa IGA hivyo wananchi waliombwa kutoa maoni kwenye kitu wasichokijua.
Adv. Mpoki: Mbili, Kutoa tangazo kwenye mtandao sio njia sahihi kuwafikia watu wengi kama Taifa. Na masaa 24 waheshimiwa majaji, ni muda mfupi wa wananchi kuona Tangazo, kutafuta mkataba IGA, KUsoma, kuelewa na kwenda kutoa maoni Bungeni dodoma Ukizingatia walalamikiwa walikuwa na mkabata tangu October na wao wamekaa na mkataba miezi 8 halafu wananchi wanapewa masaa, 24 tu. Sio sahihi.
Kwenye majibu yao, wameonyesha waty 72 ya waliotoa maoni na majina yao. Nadhani hii haitoshi kuwa shahidi kwa kuwa hakuna kiapo cha hao watu 72. Hakuna kiapo chochote katika mahakama hii kitu ambacho ni jambo la kusemekana na sio halisi pale ambapo hakuna kiapo
Kama kuna nyaraka imemtaja mtu, mtu husika lazima ale kiapo kuhusu nyaraka husika. Kanuni ni kwamba; unapoandika kiapo na unamtaja mtu mwingine, yule mtu mwingine lazima atoe kaipo kinyume na hapo kiapo husika hakitakiwi kutambulika na mahakama.
Adv. Mwabukusi: Waheshimiwa majaji kwa ufupi, vifungu hivi vinaeleza kwamba kama mkataba utakuwa na changamoto dhidi ya ukuu wake (Sovereignty) kama unapendelea wawekezaji wa nje na kuzipa nguvu sheria husika, maana yake mkataba huo ni tata.
Adv. Livino: Ibara inaelezea wajibu wa watu wote, kuilinda nchi katika hali yoyote inayoonekana inayoathiri nchi. Waheshimiwa kutoa exclusive rights kwa DP WORLD ni kuikosesha nchi yetu kujilinda na kulinda rasilimali za nchi maana hakuna hata reservation rights.