kesi hii mwabukusi na wenzake hakika watashindwa, hata kabla hawajapeleka walijua wanapeleka ila watashindwa. hata hivyo, naamini wao lengo lao hata halikuwa kushinda, ila walilenga kupaza sauti nchi yote na nje ya nchi ijue kuwa watanganyika hii kitu wameikataa, na washinde au washindwe hiyo itabaki alama itakayowahukumu viongozi wa serikali milele, wajukuu wetu watakuja kuwanyooshea vidole kwamba hamkusikiliza kelele za wananchi na hata kesi ilipofunguliwa bado hamkusikia. kwasababu hio, washinde, wasishinde kwao ni ushindi tu kwasababu wamefanikiwa kufikisha ujumbe na kupambana pale mkono unapofika. hadi sasa wameshashinda kwasababu lengo lao limeshatimia ambalo halikuwa kushinda kwenye makaratasi bali kushinda kwa kufikisha kilio cha watanganyika walio wengi. wametumia uwezo wao wote kuzuia dp world, at least they have done something, and we should appreciate what they are doing.