Mbeya: Yaliyojiri katika Kesi ya kupinga mkataba wa Bandari na DP WORLD - Julai 26, 2023

Mbeya: Yaliyojiri katika Kesi ya kupinga mkataba wa Bandari na DP WORLD - Julai 26, 2023

Naelewa nachokiongelea, huyo wakili Mwabukusi ni mwanasiasa tu aliyeshindwa ubunge 2020 anatafuta kutoka upya 2025.

Yupo kwenye kampeni hata hapo mahakamani, anajua atashindwa kwenye hili suala zima la kesi lakini umaarufu tayari keshaujenga.
Ahsante kwa taarifa, lakini mimi humu siangalii kabisa masuala ya kisiasa wala sina mpango nayo na wala sihitaji kumjua huyo Mwambukusi historia yake kisiasa, Ila namuangalia kama ni Mpigania haki wa mali za Taifa ambazo ndiyo urithi wetu na vizazi vijavyo!
 
Unajidanganya, mwenzio yupo kujinufaisha kisiasa pale.
 
26 Julai 2023
Mbeya, Tanzania

Umma Wafurika Mahakamani, kesi Mkataba wa Bandari

Huko 'Vienna' ndiko wanakokubali mambo ya kipuuzi yakiwekwa kwenye Mkataba?

Sheria zetu zinapingana na hiyo 'Vienna' au vipi?
Tafasiri zote za mikataba ya kimataifa hufanywa kupitia VCLT. Lakini pia huwezi kutumia katiba ya nchi kupinga vipengele vya mkataba, unachotakiwa kupinga ni sheria ya idhinisho la mkataba (Instrument of Ratification). Kama utaratibu ungekuwa ni huu, basi nchi nyingi zingekuwa zinafungua kesi mahakamani ili kuvunja mikataba ya kimataifa.

Mawakili wasomi wana kesi na madai mazuri na halali kabisa, lakini kuna vitu vichache ambavyo wangetakiwa kuvirekebisha kabla ya kufungua kesi. Matatizo mengi yatakuja kwenye Legal Technicalities na siyo Merits za kesi.
 
kesi hii mwabukusi na wenzake hakika watashindwa, hata kabla hawajapeleka walijua wanapeleka ila watashindwa. hata hivyo, naamini wao lengo lao hata halikuwa kushinda, ila walilenga kupaza sauti nchi yote na nje ya nchi ijue kuwa watanganyika hii kitu wameikataa, na washinde au washindwe hiyo itabaki alama itakayowahukumu viongozi wa serikali milele, wajukuu wetu watakuja kuwanyooshea vidole kwamba hamkusikiliza kelele za wananchi na hata kesi ilipofunguliwa bado hamkusikia. kwasababu hio, washinde, wasishinde kwao ni ushindi tu kwasababu wamefanikiwa kufikisha ujumbe na kupambana pale mkono unapofika. hadi sasa wameshashinda kwasababu lengo lao limeshatimia ambalo halikuwa kushinda kwenye makaratasi bali kushinda kwa kufikisha kilio cha watanganyika walio wengi. wametumia uwezo wao wote kuzuia dp world, at least they have done something, and we should appreciate what they are doing.
Miaka mitano tu watakuja kupata aibu ya Karne, watashangaa bandari itakavyokuwa yenye ufanisi, watashangaa bandari itavyochangia 50% + ya bajeti ya nchi, hakika watajidharau Kwa jitihada zao mfu za kupinga maendeleo.
 
Ahsante kwa taarifa, lakini mimi humu siangalii kabisa masuala ya kisiasa wala sina mpango nayo na wala sihitaji kumjua huyo Mwambukusi historia yake kisiasa, Ila namuangalia kama ni Mpigania haki wa mali za Taifa ambazo ndiyo urithi wetu na vizazi vijavyo!
Anapigania maslahi yake ya baadae ya kuweza kuingia bungeni. Kauli zake mara nyingi ni za kuchanganya masuala ya kisheria na kisiasa, masuala ya kuiongelea Tanganyika ni kielelezo tu cha uanasiasa wake.
 
Miaka mitano tu watakuja kupata aibu ya Karne, watashangaa bandari itakavyokuwa yenye ufanisi, watashangaa bandari itavyochangia 50% + ya bajeti ya nchi, hakika watajidharau Kwa jitihada zao mfu za kupinga maendeleo.
Haya maneno yalisemwa mara nyingi na viongozi wa CCM, kuanzia kipindi cha Net Group Solution ya Makaburu, Umeme wa Gesi Mtwara, Bwawa la Kufua Umeme la Nyerere (ambalo leo tunapashwa kuwa halitaleta nafuu yoyote kwenye umeme) na Bandari kumilikiwa na DP World. Ila baada ya kupata akili, kitakachosikika Bungeni ni kuwa hawajui suala hilo lilipitishwa vipi Bungeni!
 
Rekebisheni huu mkataba kwa kuwashirikisha Wanasheria wa ndani na nje ili DP World aanze kazi.
Tanzania ishalipa pesa nyingi sana kwa mikataba mibovu.

Je mnataka tuendelee kulipia mikataba mibovu au kwenda Mbele?

Je hiyo mikataba mibovu iliyopelekeka kulipishwa pesa nyingi sana ilisainiwa na kuridhiwa na nani?

Mimi naomba kwa upole mwingi kuwa Serikali irekebishe huo mkataba na DP World waje kushusha makontena.

HUO MKATABA SIO WA KUSHUSHA MAKONTENA BALI WA KUITAWALA TANGANYIKA.

Huyo Mwarabu si alifukuzwa kwa mtutu Zanzibar.
Je Leo Amekuwa Mtakatifu tena?

Hivi mnataka kweli Nchi ya Tanzania ikauombe ruhusa mji wa Dubai kama itataka kutumia raslimali zake zote za maji.

Yaani hadi pantoni la Kigamboni liruhusiwe na mji wa Dubai kutembea.

Na wa Chama Cha Mwananchi hamjastuka kabisa kabisa kweli...[emoji848]
Ha...ha...ha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimemkumbuka Raisi Trump wa Marekani.

Aliongea kitu kwa uchungu mkubwa sana.
Salute tu Donald Trump.
 
2020 kule Mbeya, jimbo likachukuliwa na Mwakibete, nadhani Mbeya Vijijini.
Kama una akili timamu, unaweza kunipinga kwamba Mwaka 2020, uke haikua uchaguzi Bali uchafuzi?.

Mimi ni Pro Magufuli, ila uchaguzi wa 2020, haikua uchaguzi.

Mimi Nina Demu wangu Mwalimu wa shule, Kuna Siku naongea naye huku namrekodi bila kujua.

Aliniambia uchaguzi huo, alikua akiingia ndan mtu wa CCM anapewa makaratasi 10 ajaze.

Wale mawakala wanakuaa wanapewa Hela tayari.

Wakala mbishi, anatafutiwa kesi aonekane kaleta fujo anaaondolewa.

Ule haukuwa uchaguzi !.
 
Mama amekuwa kiburi kwasababu mali inakwenda kwa wajomba na kama yeye hakuna anachopoteza.

CCM inabidi ibadili katiba ya chama ya kuwa rais ndioe m/kiti wa chama, maana kama tutapata rais mjinga nchi itateketea
Hiyo ndiyo hukumu ya mahakimu au yako?
 
Tafasiri zote za mikataba ya kimataifa hufanywa kupitia VCLT. Lakini pia huwezi kutumia katiba ya nchi kupinga vipengele vya mkataba, unachotakiwa kupinga ni sheria ya idhinisho la mkataba (Instrument of Ratification). Kama utaratibu ungekuwa ni huu, basi nchi nyingi zingekuwa zinafungua kesi mahakamani ili kuvunja mikataba ya kimataifa.

Mawakili wasomi wana kesi na madai mazuri na halali kabisa, lakini kuna vitu vichache ambavyo wangetakiwa kuvirekebisha kabla ya kufungua kesi. Matatizo mengi yatakuja kwenye Legal Technicalities na siyo Merits za kesi.
Wewe unaeleweka na unafaa kusikilizwa.

Lakini, kama "Mkataba" ni mbovu kutokana na tafsiri ya sheria zetu, unaweza kuwa mzuri kwenye hayo matakwa ya 'Vienna'?
Mbona kama ni hivyo, sheria zetu zitakuwa ni mbovu kwelikweli?

Hawa mawakili wakiacha kuegemea kwenye sheria zetu, na wakajikaza juu ya ubovu wa mkataba huo kwa matakwa ya 'Vienna', kuna jambo gani baya litakalotokea?
 
Back
Top Bottom