Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
Ilikuwa ni awamu ya wanyonge

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mbona huo mradi umeacha Kigamboni?

Sijajua kwa nini, ila nadhani Kigamboni labda ilikuwa kwenye mipango mingine au vile wakati ule haikuwa wilaya (wilaya ya Kigamboni imeanza mwishoni mwa 2015)...

Chanzo cha hiyo miradi ilikuwa ni mwaka wa fedha 2015/16 ambapo serikali iliingia mkataba na Benki ya Dunia, wakati huo mkataba ulikuwa wenye thamani ya dola za Kimarekani 300 milioni...
 
Sasa watu wenye kipato cha chini wanahitaji lami au kuongezewa kipato??
Imesaidia kuyapa hadhi kidogo baadhi ya maeneo
Lakini usitafute logic sana katika hilo yalikuwa ni maono ya mtawala
Leo ujenzi aina hiyo hautaendelea lakini hayo mafungu hayataonekana pia kwamba yameelekezwa wapi kwa hiyo haikuwa mbaya

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwani Mwiguru hajasaini mradi mwengine kama huu,maana sasa kupita manzese kwenda kinondoni ni dk tu.
Nchi imetenga Trilion 15 kugharamia madeni,nafikiri upo mwendelezo wa hii mikopo.
 
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
Watu wako tayari kubomolewa kupisha lami

Ova
 
ushangai kimara tu hapo kuna barabara zina unganisha wilaya mpaka wilaya lakin hakuna lami?

Mwendazake alisema tume chagua upinzani hivo tumletee wa chama chake ili aweze kutuwekea lami wakti huo huo anasema Maendeleo hayana chamaaa

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Kibamba imesahaulika kama Kigamboni??
Kigamboni iko vizuri zaidi ya kibamba mkuu,kibamba ukiondoa moro road huko ndani ndani hamna barabara ya kueleweka,sasa kipindi cha mvua na udongo ule wa mfinyazi balaa lake linakua kubwa,ukija kwenye issue ya upatikanaji wa maji salama,kuna baadhi ya maeneo bado wanatumia maji ya mifereji,kwa dar hamna jimbo duni kama kibamba
 
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
Mbweni hujui ni kwa Samia? Kuna sehemu wanaita Ubungo...mbweni lami kila mahali.

Kwa rais patakosaje lami?
 
Back
Top Bottom