Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

Ubungo nayo si ilikuwa chini ya upinzani,hacha ujinga kwani upinzani unahusiana nini wao ndo wanajenga barabara?
Kawe ilikuwa chini ya upinzani wakati wa miradi ya barabara...

Pili, mradi wa ujenzi wa barabara ulilenga baadhi ya maeneo tu na mengi ni yale yenye watu wa kipato cha chini...
 
Alijenga yeye lami Samia?
Au hujui zimejengwa wakati gani?
Usijifanye mtetezi wa kila kitu na huwezi kujua vitu vyote.

Samia ni jirani yangu, pembeni kabisa kwa dada yake Gwajima (huyu ni maarufu alikuwa katibu wa wizara)

Naelewa fika kuwa lami ililetwa kwa msukumo wa Samia alipokuwa Makamu na sasa akiwa rais.

Hasa hizi za mtaani kwake...sio dhambi kwa huduma kama hizo kuletwa karibu na makazi ya rais
 
Usijifanye mtetezi wa kila kitu na huwezi kujua vitu vyote.

Samia ni jirani yangu, pembeni kabisa kwa dada yake Gwajima (huyu ni maarufu aliiuwa katibu wa wizara)

Naelewa fika kuwa lami ililetwa kwa msukumo wa Samia alipokuwa Makamu na sasa akiwa rais.

Hasa hizi za mtaani kwake...sio dhambi kwa huduma kama hizo kuletwa karibu na makazi ya rais
Kawaletea lami ...furahieni basi
 
Mbezi beach sio Wapiga kura kule ndio watafuna kodi

kule Makolongo yakizidi unabadilisha aina ya gari badala ya kwenda kwa Diwani kulalamika
Uneongea vizuri mkuu,nilienda Mbezi beach kule kwa Zenna kuna makorongo kabsaa...ila majumba ni ya kifahari kuuliza nikaambiwa wanaoishi huko wala hawana shida na lami...hali ikizidi wao wananunua tu magari yenye uwezo wakupita kwenye njia zenye shuruba kama hizo.
 
Mbezi beach sio Wapiga kura kule ndio watafuna kodi

kule Makolongo yakizidi unabadilisha aina ya gari badala ya kwenda kwa Diwani kulalamika
Ndo ukweli wenyewee, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyinyi mnaoletewa lami Hadi mlangoni ndo mnakuwaga wa kwanza kusema Rais hajafanya kitu
Ninaamini una akili timamu lakini umeamua kujifanya chizi.

Hakuna mahali nimesema rais Samia hafanyi kitu...hapana.

Yapo mazuri mengi anafanya ..

Lakini anamapungufu mengi pia.
1. Hapambani na rushwa ipasavyo

2. Haonyeshi uongozi thabiti na sauti yake haiheahimiwi wa watumishi wa uma ukilinganisha na mtangulizi wake.

3. Kubwa na baya zaidi...ametuingiza kwenye mkataba wenye masharti ya hovyo na haonyeshi kitilia maanani malalamiko ya wengi...
Latika hili inaonyesha kuna watu wanamshinikiza kwa maslahi yao.
 
Uneongea vizuri mkuu,nilienda Mbezi beach kule kwa Zenna kuna makorongo kabsaa...ila majumba ni ya kifahari kuuliza nikaambiwa wanaoishi huko wala hawana shida na lami...hali ikizidi wao wananunua tu magari yenye uwezo wakupita kwenye njia zenye shuruba kama hizo.
Na wanafanya hivyo makusudi kuwahadaa wananchi, ili wao waendelee kutafuna kodi vizuriii.
 
Hayo maeneo watu walisahaulika sana kwa huduma nyingi. JPM akawapelekea maji, barabara zenye taa na zahanati.

Na huko ndio linatoka kundi kubwa la wapiga kura. Kisha mtu anakuambia JPM aliiba kura.
Nampenda sana Rais wetu wa sasa Mama Samia, ni muungwana sana , ana upendo na kuthamini watu. Lakini namkumbuka sana JPM kwasababu kipindi chake alitengeneza nidhamu kubwa sana kwa watendaji serikalini, watendaji wengi walikuwa wanaumiza vichwa sababu ya kumuogopa Magufuli.
Nimepita njia ya Mbezi - Makabe nikaumia sana kuona barabara inayowekwa lami yaani ni below standard halafu ujenzi umeanza tangu mwaka jana mwezi July lakini hata km 1 hawajafika. Kibaya zaidi upana wa barabara hata Lori mbili hazipishani na hakuna service road. Nikawaza kuwa kama tatizo ni bajeti ni mara 10 ingeachwa hadi hapo zitakapopatikana fedha za kujenga barabara ya viwango kama ya goba, madale au njia ya Malamba kuelekea Kinyerezi.

Nina uhakika Mawaziri, Makatibu wa Wizara na watendaji wa Idara na taasisi wa sasa hawana hofu hata kidoko. Japo woga sio mzuri lakini Mtanzania bila kusimamiwa na kutishiwa hawezi kuwajibika ipasavyo.

Waziri Mbarawa na watendaji wa TANROAD ni shida. Not committed
 
Kuna kitu kinanishangaza Sana...ukienda Manzese Hadi vichochoroni kuna lami..ukienda Yombo kuna lami mitaani Tu .huko Buza Hadi vibarazani kuna lami...Ukifika mbezi beach ukishatoka Bagamoyo road Tu ni vumbi juu ya vumbi...majumba makali ...eneo planned lakini barabara vumbi....wakati ukienda Mbweni JKT angalau kuna lami za mtaani kiasi lakini mbezi beach vumbi vumbi.....yaani Manzese Hadi mto umepigwa zege.....
Kuna mtu anajua why???
Wamebana barabara na mifensi yao na migeti ya kifahari..

Acha wajifunze.
 
Samia hatakuja kukaa hapo...Marais Wana Jenga sehemu nyingi...
Hata kununua Masaki sehemu nzuri zaidi..
Jibu swali Acha kuwaza kichadema
Mimi sina chama mdogo wangu.

Kipata kiwanja Ubungo barabarani kuna ugumu sana mkuu.

VIgogo wamepashikilia sana.
Karibu 75% ya mawaziri wana maeneo kule
 
Back
Top Bottom