MBEZI: Rais Magufuli azindua kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani

MBEZI: Rais Magufuli azindua kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani

Baada ya kufungua daraja la juu la Kijazi sasa Rais Magufuli amewasili Kituo kikuu kipya cha mabasi ya mikoani tayari kabisa kwa kukifungua rasmi.

Watu ni wengi sana.

Up dates;

====

WAZIRI JAFO AAGIZA MKURUGENZI WA JIJI KUANDAA BANGO LA STENDI YA MAGUFULI

Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuandaa bango litakaloitambulisha Stendi ya Magufuli

Jafo amesema hayo katika uzinduzi wa Stendi mpya ya mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani iliyoko Mbezi Luis

Pia, amemuomba radhi Rais Magufuli kwa kutumia jina lake kwenye stendi hiyo kabla ya kumuomba ridhaa

BAADHI YA ALIYOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI:

Maendeleo hayana chama, lakini lazima kuwepo na chama kinachotoa maelekezo. Wananchi wa Kibamba hamkukosea, tembeeni kifua mbele

Sifurahii sana majina yangu kutumika kwenye vitu namna hii. Kwa sababu mnaweza kuita Magufuli Stand, halafu Wamachinga na Mamalishe wakawa wananyanyaswa hapa

Nitaumia sana kama Wananchi hawa wanyonge watakuwa wanafukuzwa, halafu pameandikwa Magufuli. Maana yake itakuwa ni Magufuli anayewafukuza, kwa hiyo sitakubali

Katika stendi hii kuna vitu vingi vizuri ambavyo sijui kama watu wa kawaida wataingia. Kuna Hoteli ambayo sijui kama Machinga ataruhusiwa kuingia

Nakubali hii stendi kuitwa jina langu. Kwahiyo nataka stendi itakapoanza hawa Wamachinga wasifukuzwe kwa sababu ni kwao

Jengeni utaratibu kwa hawa wafanyabiashara ndogo ndogo ili mabasi yakiingia wanunue chakula kwa Mama Ntilie. Watakaokuwa na hela watanunua kwenye mahoteli lakini mihogo na matikiti maji yanunuliwe

Miaka 60 tangu tupate Uhuru hakujajengwa stendi nzuri kama hii. Miaka 60 baada ya Uhuru hakujajengwa 'flyovers' kama ile ya Ubungo. Ni lazima Watanzania mtembee kifua mbele

Najua hii ni 'challenge' kwa Viongozi, kwamba hapa tutafanyaje. Ni kazi ya Viongozi kutatua changamoto. Kwahiyo mjipange mpige bongo vichwa vyenu kujua hawa wengine ambao wameshalipa elfu 20 watafanyaje biashara zao hapa

Ile barabara ya njia nane tuliomba Wafadhili wakaturingia, nikamuita Mfugale nikamuuliza hatuwezi kujenga hii? Akasema tunaweza. Nikamwambia tengeneza njia nane ili hasira yangu iwapate kabisa

=====

RAIS MAGUFULI: MAENDELEO HAYANA CHAMA, LAKINI LAZIMA KIWEPO CHAMA KINACHOTOA MAELEKEZO

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema unapokuwa Kiongozi, ni lazima upate watu wanaowakilisha watu kwakuwa bila 'connection' kazi haziendi

Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua stendi ya Mabasi ya Mbezi Luis ambayo imepewa jina la Magufuli Bus Terminal

Amesema, "Dar es Salaam karibu yote ilikuwa watoto wa jirani, sasa mmenizalia watoto asilia. Maendeleo hayana Chama lakini lazima kiwepo chama kinachotoa maelekezo"

View attachment 1710840

View attachment 1710913

View attachment 1710841

View attachment 1710910
View attachment 1710895

View attachment 1710896
Wananchi wakishangilia baada ya Rais kusema jambo lililowafurahisha
Tutakuenzi daima
 
Back
Top Bottom