Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Bro tuna mambo genuine ya kufikiria. Peleka mazingaombwe yako shule ya maingi huko. Tuache tuishi uhalisia

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Hahaaaaaa kizazi cha chanjo kama kawaida yenu. Nyie mjuacho humu duniani ni kula tunda kimasihara na kubet tu ila kila kitu ni kupinga tu. Haya hongera kwa kufikiria.
 
Mambo ya imani magumu sana.....na ugumu unakuja zaidi huwa hayana uthibitisho wa moja kwa moja.
Hongera kwa kufika mbinguni
Hayana ugumu sister na sijapost hapa kwa lengo la kutaka kuaminisha watu au kujisifu ila nimeona nishare experience yangu. Sasa itanisaidia nini nipost uongo wakati tunatumia fake id na hakuna anayenifahamu.

Nimeweka kwa lengo tujifunze kuhusu uhalisia wa uwepo wa Mungu na si vinginevyo. Wewe kama Mkristo naamini utaambulia na kujifunza kitu kwa hiki nilichoandika. Soma kwa utaratibu, pitia huvyo vifungu vya Bible then muulize Mungu ukweli katika hilo.
 
Kuna kipindi hapo kati ilikua inanitokea mara kwa mara yani naota kitu halafu kesho yake kinakua hivyo hivyo..ningeshikilia hapo hapo possible na mie ningepaa mbinguni [emoji16]
Hauko peke yako watu wengi hukutwa na hiyo hali lakini ndoto ni ndoto tu. Ukiota unapaa, ukiota una mbawa kama malaika, ukiota tajiri, ukiota uko ulaya, angani bado ni ndoto tu.
 
Mi unadhani nna shida basi? Nakuelewa ila namie nimeandika tu mtazamo wangu kuhusu imani.....imani ni kitu kigumu sana
 
Kuna kipindi hapo kati ilikua inanitokea mara kwa mara yani naota kitu halafu kesho yake kinakua hivyo hivyo..ningeshikilia hapo hapo possible na mie ningepaa mbinguni 😁
Nimekupenda sister, kumbe umeokoka. Hongera kwa hilo. Mtu asikudanganye na maneno ya kiingereza mara coincidence mara Lucid dream. Kiuhalisia, Tunaye mwalimu na kiongozi aliye roho wa kweli. Yeye hutuongoza katika maisha yetu na hutufanya tujue mambo yajayo. Mi ninacho hiko kitu hata sasa.

Yaani ratiba nzima ya siku ya kesho naijua pitia ndoto. Najua kesho nitaenda wapi, kukutana na nani, nitaongea naye nini n.k. wewe kimepotea "possibly" umetingwa nq kukosa utulivu wa maombi na kumtafuta Mungu au ratiba ya maombi hauna kama zamani au husomi na kutafakari Neno sasa kama zamani na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu.

Hiyo ya kuwa mkame na kutokujua au kutokuota ya kesho hata mimi hunitokeaa pale ambapo nimetingwa na kazi za kidunia kwani ni muajiriwa wa serikali lakìni pia tu huwa kuna kipindi cha ukame kwetu wanadamu na hii huwa Mungu anairuhusu kwa sababu maalumu.
 
Binafsi naamini kuna uwepo wa nguvu kuu sana yenye uwezo beyond human imagination na haichunguziki. Ila sismini katika dini yoyote japo mimi ni muumini wa dhehebu flani. Pia simwamini yesu na mitume na manabii, ila naamini hii nguvu japo sijui kama ndo inaitwa mungu mkuu.
Dini ni biashara na hata kuanzishwa kwake kumekaa kikupiga dili tu.

Maana zaka na sadaka tunazotoa tunaambiwa tunamtolea mungu ila kina wajuba wanazipiga balaa hadi wanarudi kuwahonga wakezrtu wenyewe. Huyu mungu tunayeambiwa kwenye makanisa ambaye ana mtoto akiitwa yesu nna wasiwasi na uelewa wake wa mambo maana tunaambiwa anajua kila kitu hata ambacho hakijatokea.

Huwa najiuliza jambo moja tu. Alimuumba shetani kwa nini huku akijua angeasi na kuwa adui yake. Tuseme hakujua na ilitokea bahati mbaya, ila shetani aliasi na kundi kubwa tu la malaika, why akumuua alivyoasi? Wakafa na malaika zake? Na badalanyake akakubali yesu afe kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu kwani hakukuwa na namna ingine ya kuwakomboa?

Well angefanya kumwondolea tu nguvu ya kufanya jambo lolote.
Nikiangalia hapa duniani shetani ana nguvu kubwa sana kuliko mungu, najua kuna watu mtakuja kubisha hapa nitawauliza mniambie ni nani unamwogopa kati ya shetani na Mungu?

Ukiniuliza mm nitakwambia namwogopa shetani na ndo maana watu kila siku tunaomba ulinzi wa mungu ambaye hatumwoni na hatuna uhakika kama anatulinda naa ttunaomba atulinde dhidi ya hila za mwovu shetani.

Katika theories nyingi wanasema kile kitu unachokiogopa ndo hicho unachokiabudu.

Tunamwambudu mungu sio ila kila siku tunamwomba atulinden dhidi ya mwovu kwa kusema hivo wote huwa tunamwabudu shetani bila kujua.
Nina mengi sana ya kuongea ila kwa leo ngoha niachia hapa kama trigger ya mawazo mengi ya wana jf najua wengine mtanitukana ila nawakaribisha wote napokea kila zuri na baya.asubuhi njema
 
Wale wale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…