Kwa wakristo lengo lao Sio Kwenda PEPONI bali kwenda mbinguni .
Wanaolenga Kwenda Peponi ni Waislamu tu.
Wengine wanalenga Kwenda mahala Kwingine kabisa.
Utafiti unaendelea. Pengine Mungu anaweza kuwaonyesha tena anatomy ya peponi ambako kumejaa ngono 24hr. Mbinguni ni worship 24/7. Tofauti inaanzia hapo. Sasa wapi ni wapi, utafiti uendelee.
Jehanum nafikiri ni moja tu na huwa haibishaniwi kwa sababu haina kanuni za mtu kuzifuata akiwa duniani. Anayebishaniwagwa ni Mungu kwa kuwa Ni Mkuu sana na anamiliki mbingu, duniani na ni Mtengenezi wa kila kitu. Mungu kama vile alivyoweka sheria ya mchana na usiku mahala pake, nyota za angani na bahari kuwepo kwa utaratibu, vile vile ameweka utaratibu wa maisha ya mwanadamu akiwa katika dunia aliyoiumba. Ninadhani hata wanyama nao kawawekea tratibu zao ila kwa kuwa hatujui lugha zao, pengine hatuwezi kuwa wasemaji wake.
Ubishi juu ya Mungu unaanzia katika kiburi cha mwanadamu ambaye hataki kuongozwa, kutawaliwa wala kuishi kwa kanuni anazotaka Mungu. Anataka aishi anavyojisikia na ndiyo sababu ya kuanza kubisha habari za Mungu ili ajustify kwamba hakuna mamlaka zaidi inayoongoza maisha yake na ambayo hana ubavu hata wa kuihoji. Hajiulizi kwa nini siku ya kufa ikifika haibishi kufa. Hata kama alikuwa jeuri kama gadafi ama sadamu husseni, wakifa wanakuwa wapole wasiokuwa na uwezo hata wa kusogeza kidole. Na kwa nini watu wanaogopa na kukimbia sana kifo.
Ubishi juu ya Mungu na Mbingu zake ni kiburi cha mwanadamu ambacho ndicho mauti yake. Kwa hiyo jehanum haibishiwi kwa sababu haijawahi kujibainisha kuwa iko juu ya mtu na ikampa masharti ya kuishi. Mwanadamu ana kiburi, hatakikuongozwa wala kutawalaiwa. Anataka aishi na kufanya anachotaka na ndiyo kiburi hicho kilipelekea kumdhihaki Mungu, kumhoji Yeye na Mbingu ili watu wahalilishe ushetani wao. Angalia watakaokuja hapa wakibisha, uone hoja zao. Kikubwa Mungu hachunguziki na haishi kwa kanuni za kibinadamu. Anafanya mambo kwa mpangilio sana kama walivyofahamu waleta habari na hana mipaka. Mtu asilete habari za kwamba Mungu hawezi kuwaonyesha watu habari za Mbingu as wao ndio wanakaimu nafasi ya Mungu.
Kikubwa tu ndugu zangu. MUNGU HAJIPINGI. UFUNUO, MAONO, MAFUNDISHO AU UJUMBE WOWOTE UNAOSEMEKANA UNATOKA KWA MUNGU, TUNAUPIMA KATIKA MANENO YA MUNGU KAMA UNALINGANA NA MAANDIKO KWA UPANA WAKE. LOLOTE LINALOPINGANA NA NENO LA MUNGU HILO SI LA MUNGU WATU WA MUNGU TULIKATAE!. NINASIKITIKA KUNA WATU WANAKARIRI MSTARI MMOJA BIL AHATA KUUFAHAMU UNDANI WAKE NA UNAHUSIANA VIPI NA MAANDIKO MENGINE, WANAKUJA HA UPEPO WAKIDHANI WAMEMMJUA SANA MUNGU. HAPANA NDUGU ZANGU. TUJIFUNZE KUMJUA MUNGU KATIKA NENO LAKE KWA UPANA MAANA NDILO MUNGU ANALIHESHIMU. MATUKIO, MAFUNUO, MAFUNDISHO,,VYOTE MUNGU AMEVISEMA. ANAYEJIFUNZA HUUONA UKWELI NA HUTAFUTA KUELEWA.
Ni vizuri tukianza kujifunza kwanza katika Mungu, tuoanishe tunayoyaona na kuyasikia kama yako upande wa Mungu ama kinyume chake, ndipo tuseme. Kama mtu hana ufahamu juu ya hayo, ni afadhali kunyamaza kimya kuliko kujitengenezea hukumu za maneno ya kumdhihaki Mungu.
Mungu atupe siku njema ya amani.