Mbinu mpya za kuibiwa walevi kupitia wanawake wa mjini

Mbinu mpya za kuibiwa walevi kupitia wanawake wa mjini

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,104
Reaction score
4,090
Walevi wa mwanza kuweni macho acheni kubeba kila mwanamke bar kwa kuwa ana makalio makubwa.

Kisa kifupi nlichosimuliwa na kijana tuliekutana mlango wa kutokea lodge mwanza.

Nimetoka zangu safari nikapoa lodge ilia asubuhi nifanye mishe zangu hapo mwanza then nigeuke

Asubuhi nafunga mlango wa chumba niondoke nasikia maongezi kwenye korido kwamba kama Kuna mchizi analalamika kaibiwa hela jana usiku na vibaka.

Ikanidi nisogee na kusalimia na kuuliza kwan imekuwaje.?

Akasema brother jana usiku tulikuwa tupo bar na brother tunakunywa Ila mimi sio mlevi Ila brother akapata mwanamke wakawa kama couple ya ghafla wakawa wanakunywa pamoja na kuinjoi mvinyo lakin brother alilewa sana Ila yule demu alikuwa anakunywa kwa mahesabu makali na pombe nyingine alikuwa anajimwagia mwili mpaka nguo zake zikalowa. Sasa kufika majira ya saa nane usiku yule demu akamwambia brother nipeleke home nikabadilishe nguo ili turudi kuinjoy mimi nikamtalia nikamwabia usiende kwa kuwa wewe umelewa sana kama vipi twende na mimi ili turudi chap. Basi yule demu akasema ngoja nimpigie boda boda wangu simu atufuate basi punde boda akafika wakondoka lakin njia alizokuwa anapita yule boda ni vichochoroni mno mpka jamaa akawa kama kashtuka hivi lakin akaache kama ilivyo basi wamefika Mitaa ya bugando ndani ndani huko boda akasimama demu akashuka mara paaap vibaka hawa hapa na marungu na sime za kutosha.......

Kwanza wakampiga yule demu Kofi moja la nguvu yule demu akakimbia kusikojulikana lakin boda boda akaenda kutulia pembeni na akakimbia kabaki msindikizaji wakampukutisha kama milion na nusu Ila simu wakamuachia yule kijana.


Note huyu demu alikuwa anafahamiana kabisa na hawa waporaji na pale bar ilikuwa ndio njia ya kujipatia wateja wake ili wakalizwe kule chochoroni
 
Back
Top Bottom