Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Polisi ana bunduki, bomu, kisu, rungu na mafunzo. Anaenda akiwa full amejikoki kuonana na raia anayetoa maoni yake kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ili amkamate.Mwanasiasa wa mwisho kukutwana vidhibitinyumbani ni Seif Sharif Hamad mwanzoni mwa miaka ya 80 huko.
Mwanasiasa aliyefikia ngazi ya njuu nchini huwa na makazi mikoa mitatu,Dodoma,Dar es salaam na kijijini kwao kwa asili.
Kwa hapa Dar es Salaam wanasiasa wengi wana makazi zaidi ya moja,makazi rasmi na makazi yasiyo rasmi
Haya makazi yasiyo rasmi huweza kuwa ni nyumba ndogo yaani mchepuko,au simply safe house,ambapo hata dereva huenda asipajue,mkuu akiwa na kikao cha siri au mchepuko wake anawasha gari usiku na kuingia ndani,huko kuna mlinzi na mtu wa usafi.
Mambo yote ya ovyo hufanyika huko,iwe mikakati ovu ya kisiasa,michepuko,document za hatari hukaa huko.
Si mke wala watoto wa huyu mwamba hupajua hapa.
.
Polisi kupekua makazi rasmi ni kupotezeana muda mtaambulia kadi za mwaliko wa harusi na barua za kukumbushwa kulipa madeni ya benki,
Hakuna cha maana mtakachoambulia,mnafanya kazi kizamani sana
Ukiwapigia polisi kuwa kuna wahalifu wanavunja mahala wanakujibu hawana gari ama hawana mafuta... lakini kwa marehemu Kibao et all wanawafukuzia na magari manne manne na mitutu kibao.....
Nchi imeoza.
Raia wamesomewa albadir na serikali yao