Mafundi wanazingua sana, kwa mtu asiye na uelewa japo kidogo kwa hiko anachokifanya fundi lazima amchezeshe!
Hii ni kama tabia asili ya ufundi.
Lakini pia hii ni kwa mafundi wasioenda na wakati, kuna semina na mafunzo yanatolewa jinsi gani fundi atafaidika na kazi yake ya ufundi bila kumuibia mteja wake.
Pia mafunzo ya ujasiriamali ambao unafundishwa kuufanya ufundi wako kama biashara yenye mtaji na faida.
Kwa mtu ama fundi anaefanya kazi zake kwa kujifunza hawezi kuwea tegemeo la faida kubwa kwa kumzidishia mteja garama za vifaa vya ujenzi nk.
Unapopata kazi ya kutoka kwa mtu ni kama mteja amekuja kwenye biashara yako kama mwenye duka, unabidi umfanye awe mteja wako na kuwa balozi wa kazi yako, kama kibiriti kwenye duka A kinauzwa 100 na kina njiti 45 basi na dukani kwako iwe hivyo hivyo.
Fundi yoyote anaezingati mengi pamoja na hayo hawezi kumpoteza mteja na hata kuwa na upungufu wa kazi.
Pia wateja nao wanamchango mkubwa wa fundi kutokuwa mwaminifu, kazi ya ufundi unatumia akili nyingi na nguvu nyingi na muda mwingi kufanikisha, ila mteja anakubana kwenye malipo yako mpaka inafika nusu bei!
Na hii nikutokana na ufundi na fundi kutokuwa na thamani kwenye jamii ni kazi inayochukuliwa ya kawaida mno ingawa inahitajika, hivyo fundi ili kufidia walao japo kidogo , kama cement zingekuwa kumi basi lazima akuambie 12.
Au hizo kumi atatumia 8 kwa kupunguza ubora ili aweze walao kufidi muda nguvu na akili zitakazotumika.
Pia sheria za ufundi hupaswi kufanya makadirio kamili ya vifaa vya kazi bali uzidishe, ila uzidishapo iwe ni kuzidi kwa kiasi na mwenye kazi anashirikishwa vifaa vikivyobaki baada ya kazi .