Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Kama fundi unaona anafanya kazi nzuri mlipe vizuri sio materials za millions 20 halafu gharama unamlazimisha umlipe 1m.
 
Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki
Mafundi Maiko hao!
 
Watu wanasemaga "Hesabu hizi najifunza nitatumia wapi?" Hapa ndipo pa kutumia hesabu. Jua chumba chako ni sqr futi ngapi. Tafuta sqr futi za marumaru moja ni ngapi. Hapo utajua chumba kitakula marumaru ngapi. Tafuta gypsum board moja sqr futi ngapi. Utajua chumba kinahitaji boards ngapi. Hata tofali zitakazo hitajika kujenga nyumba unaweza kujua idadi yake kwa namna hii. Jua total surface area ya kuta za nyumba yako. Tafuta surface area ya tofali. Ukigawanya utajua unahitaji tofali ngapi? Hata bati unaweza kujua kwa namna hii hii. Hata rangi inayohitajika. Kama fundi anakuibia basi awe kama mwizi na siyo kukupiga kwenye mahesabu.
 
Wa umeme sie alikuwa mstaarabu hakutupiga kabisa ila wa pvc, gutters, plaster ......nacheka kwa huruma

Kuna duka flani la vifaa vya ujenzi kasoro tiles na umeme lipo mbezi kibanda cha mkaa wanauza vitu nusu bei hapo tu ndipo tulipoponea na ukimpeleka fundi unamuona uso umebadilika ghafla km anataka kulia kujinyea au kutukana, fikiria bajeti ya m 4 ishuke mpaka 2.3
Hili duka linaitwaje mkuu? Liko kibanda upande upi?
 
Mie kwangu vituko alitaka bati 200 zimebaki 26. Alitaka akanunue mwenyewe nikaenda mimi. Misumari alitaka 75 imebaki 12. Kofia zimebaki tano na kiloba cha Misumari nchi 4
 
Mie kwangu vituko alitaka bati 200 zimebaki 26. Alitaka akanunue mwenyewe nikaenda mimi. Misumari alitaka 75 imebaki 12. Kofia zimebaki tano na kiloba cha Misumari nchi 4
Hizo bati aina gani mkuu ?
 
Fundi wengi ni janja janja sana fundi alitafutwa wa mkoa mwingine ili kusiwe na mambo ya kufiwa/mtoto anaumwa/kuna msiba na blabla za uongo kumbe yupo site nyingine,kwenye mahesabu ya kupaua aliingeza Bati 22 na kumpa jirani ambae ndo tulikuwa tunamtumia kuweka vitu vyetu na tulimuamini jirani akamzunguka fundi na kusema ukweli ila bati alishauza so mwisho wa siku fundi hakupata gawio na mwisho wa siku tulijua wizi wake,hata ukiakaa site kama ni wezi ni wezi tuu unapigwa upo hapo hapo
 
tatizo mkiambiwa bei ya ufundi mnashusha sanaa nao mafundi wanajiongeza
 
Back
Top Bottom