Noo, sio kuwa nimekucheka, Mimi mwenyewe Nina ujenzi, fundi yupo site na vijana wake, eti ananiambia unajua hatujala, nikamwambia mi nimefunga, akasema sisi hatujafunga, nikamwambia kwahiyo niwaitie mama ntilie aje na msosi, akanambia Ni wewe tu bosi ukitununulia, nikamwambia si nimekupa advance ya kazi ili Mambo Kama hayo umalize. Eti ooh unajua boss majukumu. Nikamwambia Sina hela mwanangu. Tena nikaenda pembeniiii kwenye kivuli. Mara akaagizwa dogo mmoja. Naona Kila mmoja anatoa pesa yake wanampa yule mwenzao. Nikasema aloooo weeeee mmenikosa 😂😂😂😂