Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

kwa wale wanaoishi kwenye nyumba huku ujenzi unaendelea usilogwe
ukajitia mwema kuwapikia ili kazi waifanye kwa wakati kuwaepushia ile adha ya kutoka kutafuta chakula kama kazi ilikuwa ya wiki itaisha baada ya mwezi😅😅🤣🙌
Nashukuru huruma yangu ipo likizo kumbe ningejichanganya niliwaza kweli hilo ila nikapotezea, ningefurahishwaaa
 
Ishu ya wizi kwa wabongo nadhani ipo kwenye Damu, hata wachina kwenye makampuni yao ya ujenzi wanalia wizi wa Mafuta mpaka wizi wa vifaa vya ujenzi...kama ingekuwa sio sheria, Wachina hawawataki kabisa wabongo kazini kwao.....
 
Kweli aisee ina maana ukiwa na ujenzi uache kazi zote ni wewe na site tu, kuna ile huna idea ila upo tu km picha napo utapigwa tu, kiufupi bongo pagumu sana
Mkuu idea ya ujenzi ni rahisi sana kwa layman kuijua kama umemaliza shule sawa sawa.

Ukijua urefu wa tofari kuwa ni cm90, waweza kuprogram ujenzi wa ghorofa kwa kuelewa idadi ya matofari kwa calculater ya simu.

Formular ya hesabu za ujenzi ni kutoa, kugawa, kuzidisha na kijumlisha, simple mathematics asikwambie mtu.
Utakapoelewa kwamba mfuko mmoja wa saruji unajenga tofari ngapi, trip moja ya mchanga inachanganya saruji mifuko mingapi kwa lipu ama tofari utakuwa umeua, utatoa amri zako kwa fundi na akutii.

Ubabaishaji huanzia pale mafundi wanapozagaa eneo la ujenzi kupiga kazi na kama hauelewi chochote utaanza kujenga over expectiations na kuanza kuhoji maswali na hilo ndiyo kosa la kifundi.

Zingatia kanuni ulizojiwekea, usiulize maswali kila hatua, fundi atakuona hujui na kuanza kutengeneza mazingira ya kukupiga.

Kama una maswali tafuta fundi wa mfukoni asiyehusika na hiyo project, huyo atakwambia ukweli mtupu.

Dukani ni mwiko kumtuma fundi, hata kama bei inafahamika, siku ya manunuzi kuna discount, nenda mwenyewe utaokoa gharama.
 
Tumekusoma sakasaka asante sana
 
Simenti unaweka store, wakitaka mifuko kadhaa unahakikisha imechanwa na kuchanganywa yote ndio unasepa. Fundi mkuu na vibarua wake huwa wanashirikiana kuiba.
Mkuu ushapigwa sana kwa mtindo huo bila wewe kujua.

Kuna jirani yangu kamaliza nyumba kimasihara.

Alinunua kariba ya kufyatulia akatulia.

Kisha akawatangazia mafundi na vibarua wao kuwa anapokea tofari zima kuanzia moja, kipande, simenti ya kupima ama udongo uliochanganywa.

Kwa ndoo ndogo iliyojaa udongo alikuwa akinunua 300, vumbi la saruji 200 kwa kilo, tofari zima 500 na kipande 200.

Ilikuwa mafundi wakifika site wanahaha kujiokoteza ovyo kama mbwa.

Kwa hiyo fundi akikimbiza ndoo zake 5 tayari keshapata hela na jamaa chap anafyatua tofari na kupanga hata kama ni moja.

Kwahiyo mkuu kuchanganya na kuona kuwa tayari umewajibika, ulikuwa unaibiwa sana tu.

Usimamizi unahitaji kuua shughuli zingine zote, maana ukisimamia sawa sawa, project itamalizika haraka ili uendelee na majukumu yako mengine.
 
DAWA ni kuweka CID or informer mule mule katika mafundi unamwambia bana nitakulipa .nilinde nikulinde.
Kwahiyo watu wakichinja nguruwe(yaani kuiba kimyakimya kwa Siri sana) jamaa ananipa mchongo wote..hii inasaidia sana maana ukijua unawakata tu mishara yao au ktk pesa yao utakayowalipa
 
Napenda courage yako
Asante

Basi nilikuwa na kazi ya kufatilia kila hatua kama alivyoshauri mdau mmoja huko juu,, ilinisaidia kiasi flani fundi anakuwa anajua uko na uelewa na issues za ujenzi kumbe mweupe

Watu wazima wana unafuu kiasi katika ishu za upigaji kwenye ujenzi tuwatumie hao, ila vijana basi sina pa kuwapeleka ningefukuza wote nchi nzima
 
Nashukuru huruma yangu ipo likizo kumbe ningejichanganya niliwaza kweli hilo ila nikapotezea, ningefurahishwaaa
ohoooo jichanganye wakuonyeshe shooo🤣🤣🤣🤣wanajua msosi upo wa bure na asubuhi wanakuja na vitafunwa tu chai wanakunywa kwako🙌🙌🙌🙌 wanakuja kwa kuchelewa kazi hawamaliz haraka
 
Kwenye chai kama ulikuwepo vile😅😅😅 akili zao za kitoto sana kumbe

Sikukuu niliwapikia pilau nao tukajumuika nao ebanaee walivyoshiba tu wakaaga na kuaga nikasema atakaeniona nahurumia hawa viumbe aniite 🐕
 
Asante

Basi nilikuwa na kazi ya kufatilia kila hatua kama alivyoshauri mdau mmoja huko juu,, ilinisaidia kiasi flani fundi anakuwa anajua uko na uelewa na issues za ujenzi kumbe mweupe

Watu wazima wana unafuu kiasi katika ishu za upigaji kwenye ujenzi tuwatumie hao, ila vijana basi sina pa kuwapeleka ningefukuza wote nchi nzima
Noted with thanks
 
Back
Top Bottom