Nadhani uzi huu utatusaidia kung'amua janja janja wanazofanya mafundi, kwahiyo tutawamudu, juzi nimemuuliza fundi hii kazi itahitaji mifuko mingapi ya sementi, akanambia 25, nikamuuliza Bei ya sementi ipoje, akasema 16 Hadi 16 Mia 5. Nikaamua kwenda mwenyewe dukani bila kumwambia, nimekuta Bei Ni 14 na 15. Sijamwambia chochote, ntamletea sementi na nitamsimamia bampa to bampa, Kwanza ntampelekea mifuko 20 Kwanza. Ila Kuna mdau katoa wazo la kuulizia ratio kwa mafundi wengine ili kujua idadi halisi, nalo Ni Jambo la busara sana