Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

Unapanga jinsi ya kumdhibiti fundi asikuibie wakati wa ujenzi wakati wewe mwenyewe gharama za nyumba unayotaka kuijenga hailingani na kipato chako halali. Anza kujiuliza kwanza wewe hizo pesa za ziada umezipata wapi kabla ya kufikiria jinsi ya kumdhibiti fundi.
 
Wee
Mafundi wanalalamikiwa bure,na hali hii ndio imepelekea kuwa mazoea kwa hiyo hata wewe ukiwa na lengo la kumlipa fundi vizuri anaona wote ndio walewale.

Mimi fundi simu nipo kariakoo, anaweza akaja mteja ukamwambia kioo kinauzwa 50,000 na akakubali kabisa,sasa mwambie ufundi 20,000 au 15,000 kama atakubali kutoa atakwambia nina 5000.

Kama asingezaulika fundi basi haya yasingetokea,ila kweli mteja yupo tayari kununua bidhaa(materia)kwa bei kubwa lakini si kumlipa hela nzuri fundi.


Wewe utakuwa ni fundi mwenye tabia ya wizi. Kwa kawaida na kimkataba kabisa fundi hatakiwi kutoza gharama ya zaidi ya asilimia kumi ya gharama ya materials.
 
Ujenzi wako utakuwa gharama mara dufu ukiweka kampuni ya kusimamia na bado kwenye vifaa watakuibia.

Watanzania wengi ni wezi
Vyema kabla hujampa kazi, ifanyike quantification ya mahitaji kisha ndiyo utoe tenda

Otherwise ni kama ulivyosema, Ujenzi wa milioni 100 zinaweza kufika shilingi milioni 150🙌
 
Kwenye hii thread tutakuwa tuna share Mbinu za wizi za mafundi ujenzi ili kusaidia wale wanaotaka kujenga "wasipigwe ".

Wengi tumepigwa sana hadi kuzijua hizi mbinu.

Karibuni.
saf sana mimi saidia fundi mstaafu nitaweka kuwachomea utambi mabosi zangu wa zaman wanyonyaji wametunyonya sana hawa wehu munaowaita foman au injinia.
 
Maskini tunaojenga tuna taabu saana. Hata sisi huko maofisini tunapiga kwa nafasi yetu.

Dukani hulii lii bei njoo kwa fundi sasa. Unataka umnyonye why asikupige?
Unanunu materials mamilioni fundi anayefanyia kazi hayo materials ya mamilioni unampunja. Kazi unaitaita mafuñdi zaidi ya watano kuangalia nani kapunguza hata 20000 eti ndio umpe kazi.

Hapa unamsema fundi unasahau hata ww huko kazini kwako unapiga... Kama ni biashara unaipiga serikali kwenye kodi.
ahsante sana. kama fund mstaafu umetusemea.
 
Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki

Mimi aliniambia mabati 140 tutatumia mabati 119tu 21 yakabaki nilimwambia huu niuharibifu wa mali kama mtu umesomea na una uzoefu kwa miaka kadhaa kwa nini ukosee kiasi hiki kwenye makadrio
Pumbafu sana
 
Chamsingi ni mhimu kuwa na uelewa na mradi uliouanzisha angalau kidogo ukishindwa jiunge na jamii furom au nenda google utapata usaidizi angalau kwa machache yatakusaidia kupata mwelekeo
 
Makanjanja wameishafanya yao na imeindoka na fundi
Hawa jamaa wanaiba cement, nondo na kila kitu wanachakachua na mwisho wao mbaya tu

Hivi hili jengo limeporomoka ni nini kama sio ujenzi mbovu
Screenshot_20240418_065247_Instagram~2.png
 
Nadhani uzi huu utatusaidia kung'amua janja janja wanazofanya mafundi, kwahiyo tutawamudu, juzi nimemuuliza fundi hii kazi itahitaji mifuko mingapi ya sementi, akanambia 25, nikamuuliza Bei ya sementi ipoje, akasema 16 Hadi 16 Mia 5. Nikaamua kwenda mwenyewe dukani bila kumwambia, nimekuta Bei Ni 14 na 15. Sijamwambia chochote, ntamletea sementi na nitamsimamia bampa to bampa, Kwanza ntampelekea mifuko 20 Kwanza. Ila Kuna mdau katoa wazo la kuulizia ratio kwa mafundi wengine ili kujua idadi halisi, nalo Ni Jambo la busara sana
Jambo jema, hakikisha mapatano yenu yawe win win stution
 
Kwenye hii thread tutakuwa tuna share Mbinu za wizi za mafundi ujenzi ili kusaidia wale wanaotaka kujenga "wasipigwe ".

Wengi tumepigwa sana hadi kuzijua hizi mbinu.

Karibuni.
Ni umasikini tu, lkn kazi inatakiwa ifanywe kwa mkataba.

Changamoto ya umasikini wetu ni kwamba
.Boss anatafuta mbinu ya kumlalia fundi
.Fundi anatafuta mbinu ya kufidia kile alichomlalia boss

KAMA UNAJITAMBUA ACHANA NA KAZI ZA KIMAZOEA.
Fanya hivi
1. Tafuta fundi then angalieni gharama ya material na labour charge.
Tafuteni mwanasheria muingie mkataba wa kazi.

Kazi yako wewe client iwe kukagua ubora wa kazi kama uko sawa kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.

Lkn kwakua maboss wengi wanataka mteremko na kulalia mafundi, wanakwepa kutumia njia hii
 
Kuorodhesha idadi kubwa zaidi ya vinavyohitajika

Kuelekeza ununuzi wa material katika maduka wanayojua wao

Kuna maduka yanayotoa kamishem kwa mafundi kwahiyo siyo lazima kwamba akikuelekeza duka eti anania ya kukuibia.

Pia boss akiwa muungwana ni ngumu sana kuibiwa na fundi.
 
Mi kitu muhimu naonaga ni kuweka msimamizi ambae atakua makini na mifuko ya siment itakayokua inafunguliwa na kuhakikisha anakua na hesabu mkononi kila wakati siment inapotumika.

Kwenye bati sina uzoefu
Kama una muda simamia mwenyewe wasimamizi ndiyo wapigaji wakubwa.
 
Back
Top Bottom