Me I and my self
JF-Expert Member
- Sep 16, 2016
- 4,077
- 8,828
😂😂😂na vibegi vyao mgongon vya kuibia utasema wanabena vya maana
Mafundi Maiko hao!Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki
Hili duka linaitwaje mkuu? Liko kibanda upande upi?Wa umeme sie alikuwa mstaarabu hakutupiga kabisa ila wa pvc, gutters, plaster ......nacheka kwa huruma
Kuna duka flani la vifaa vya ujenzi kasoro tiles na umeme lipo mbezi kibanda cha mkaa wanauza vitu nusu bei hapo tu ndipo tulipoponea na ukimpeleka fundi unamuona uso umebadilika ghafla km anataka kulia kujinyea au kutukana, fikiria bajeti ya m 4 ishuke mpaka 2.3
Hizo bati aina gani mkuu ?Mie kwangu vituko alitaka bati 200 zimebaki 26. Alitaka akanunue mwenyewe nikaenda mimi. Misumari alitaka 75 imebaki 12. Kofia zimebaki tano na kiloba cha Misumari nchi 4
Ukiwa unaelekea mbezi mwisho mkono wa kulia kuna sehemu wanapark magari ya mizigo ulizia baba shopHili duka linaitwaje mkuu? Liko kibanda upande upi?
Ufafanuzi hii mkuuKulaza roller za nondo mbili kwenye box la linta badala ya kusukua nondo