Mbinu ya Kunyamaza kwa Samia Suluhu kumepunguza kwa sehemu kubwa hekaheka mtandaoni

Hamjambo!

1. Kama mnakumbuka vizuri. Baada ya MO29 moja ya mbinu nilizoandika zitakazoshusha hasira za watu ni pamoja na Samia Suluhu kutozungumza zungumza mara kwa mara kwenye luninga.

2. Mbinu hiyo inafanya kazi haswa tena ni mbinu kamilifu hasa ukiwa upo upper hand. Lakini ukiwa lower hand hiyo inaweza ikawa sio mbinu kamilifu.

3. Mtandaoni wanaharakati wanategemea mambo makuu yafuatayo ambayo ndio yanawapa energy kushambulia na kuifanya serikali ihanye;
a) Kuvuja kwa Siri
Endapo kuna leakage ya siri ndani ya mifumo na idara za serikali hii inawapa nguvu kubwa wanaharakati mtandaoni.
Kuvuja kwa siri kunategemea uwepo wa double agent na Moles ambao wao ndio kazi zao hizo kutoa siri kwa maslahi na sababu mbalimbali wanazozijua wao.

b) Kauli na hotuba za viongozi wa nchi hasa Rais.
Wanaharakati wanaposikia kiongozi Fulani atahotubia kwao ni advantage na wanakaa kitako kusikiliza kwa kina. Watadili na makosa, uongo, udhaifu wa hotuba ya kiongozi.
Kumbuka wanaharakati wengi Wana akili na uelewa mkubwa tofauti na watu wa kawaida. Hivyo wanauwezo wa kujua uongo kwa haraka, na kuyaona makosa ya wazi.

Kwa Tanzania, wanaharakati wengi hutegemea hotuba na kauli za viongozi ili kuwafanya wawe relevant.
Ukikaa kimya. Wanakosa chakuongea na watatumia mbinu zote kukuchokoa ili ujitokeze uongee ili uwepo wao uonekane.

C) Ufanisi Duni wa huduma za kijamii na miundombinu ya serikali.
Hiyo ni moja ya mambo yanayowafanya wawepo.

d) Polisi na vyombo vya dola kutofanya kazi kwa kufuata Sheria.
Hakuna kitu kinawanufaisha wanaharakati kama Polisi au watu wasiojulikana.
Yaani huo ni mtaji kwa Wanaharakati.
Fulani kakamatwa kiholela au kijambazi. Wanaharakati hao.
Fulani katekwa hajulikani alipo. Wanaharakati hao.

Wasiojulikana na ukamataji wa Polisi ni mtaji mkubwa wa wanaharakati. Hao ndio wanawapa kazi ya kufanya, wanawapa nguvu na kuwa maarufu.

Kipindi cha Kikwete akitawala, wanaharakati walikuwa wanawakati mgumu Sana. Na mtaji wao ulikuwa Mdogo Sana ambao ni kusemea Ufisadi kama wa Richmond, sijui Escrow n.k.

Lakini mtaji sasa umekua. Wana mambo mengi ya kuyazungumzia na serikali kupitia vyombo vya dola wanawawezesha.

4. Huwezi kuwadhibiti wanaharakati kwa kutumia nguvu. Kadiri unapotumia nguvu unawapa mtaji, unawapa agenda, unawafanya wawe relevant.

5. Wanaharakati mara nyingi ukitaka kuwanyima mtaji ni kufanya maendeleo yanayoonekana kiasi kwamba wananchi wawadharau.

6. Mbinu ya Pili wape Uhuru wapige kelele. Mtu akiongea mwanzoni atazingatiwa lakini mwishoni masikio ya wananchi yatamchoka. Watu huzoea sauti ileile. Lakini kuzima sauti hii, kisha inaibuka nyingine na kuipa nguvu agenda husika.
Kuruhusu sauti ni kuiua sauti hiyo kifo cha asili. Kwani Kila sauti inakilele.

7. Baada ya Siku sabini mpaka tisini watu wengi hasira hushuka, na ule munkari hupungua. MTU anazoea hali ya hasira kisha inayeyuka.

8. Nilishauri Samia Suluhu akae kimya na kama atajitokeza aongelee mambo mengine kabisa yasiyohusiana na matukio mabaya yaliyokwisha tokea.

9. Jitahada kubwa ifanyike kuwaunganisha watu Kwa njia laini, Rafiki, zenye dalili za upendo, kuungama, na kuleta taifa pamoja.

10. Huyo anayeratibu mzozo wa kidini Kwa hao vijana kujibishana na Kanisa Catholic aache mara moja. Mbinu hiyo haina tija. Inapanua mgogoro.

11. Wapigwe marufuku watu wote hasa vijana wasiohusika na dini kutolea ufafanuzi mambo ya kidini kwa lengo la kuitetea serikali..

12. Mzozo huo haulengi kusahaulisha tukio la MO29 Isipokuwa unaupa uhai na kufanya fukuto liendelee chini kwa chini.

13. Mpango uwe kusonga mbele. Na huwezi kusonga mbele kwa kushabikia mizozo yenye mizizi ya MO29.

14. Mwaka 2026 usiwe mwaka wa kujengea kwenye msingi wa MO29.
Yaani MO29 usiwe msingi kwa Kila tofali linalokuja juu.
Tutafute msingi mwingine.

15. Serikali itafute namna ya kupunguza mtaji kwa wanaharakati kwa njia ya kushughulikia agenda wanazozisema.
Mfano;
Katiba mpya.
Kutokuwepo kwa wasiojulikana
Polisi na vyombo vya dola kufuata Sheria katika ukamataji.

16. Kuruhusu utoaji wa maoni ni kuua industry ya wanaharakati. Kwa sababu wao uthamani wao unaongezeka pale wanapozuiwa wasiseme.
Kama wakiruhusiwa thamani yao itaenda chini.

17. Wapo wanaharakati WA kweli ambao thamani Yao haitokani na migogoro ya serikali au kupambana na serikali.
Wao wanasimamia ukweli, haki, na upendo.
Hawa kuwatofautisha ni rahisi ni kwenye matumizi ya lugha,
Lakini pia wanakosoa na kutoa solusheni.

18. Wapo wanaharakati ambao wao hunufaika na mzozo na serikali.
Mara nyingi hawa hutumia haki ya kutoa maoni lakini wanavunja haki za wanaowakosoa.

19. Mfano; Mwanaharakati anaweza kuona mtibeli anatatizo fulani. Labda katika kampuni yake anaonea wafanyakazi, anadhulumu.

20. Yeye akiwa ananikosoa kwa Jambo ambalo ni kweli kabisa, na natakiwa kujirekebisha au kushughulikiwa na Sheria. Atanikosoa kwa lugha ya uonevu, Kali, kejeli, dhihaka na matusi ya nguoni.
Hii sio sawa. Na watu waungwana, wenye haki, wenye upendo, wenye Akili, wakweli hawawezi kufanya Jambo kama hilo.

21. Mwaka 2026 uwe mwaka wa uungwana. Mwaka wa Haki, mwaka wa Upendo, mwaka wa Ukweli. Mwaka wa Akili.
Mwaka wa UTU.

Kufikia hapa sina la ziada.

TaikonMaster
kwa sasa Dar es salaam
Solution hapa ni moja tu, hakuna blaablaa nyingi, anatakiwa kunyongwa.
 
Na akifungua tu mdomo tunaye
 
😅😅😅 Hatari Sana. Ukikaa kimya mtu hajui next move yako ni ipi. Hajui unawaza nini. Hajui mood yako. Yaani ni kimya
Swali ni kwamba kwnn unadhani anapaswa kukaa kimya? Je, humuamini katika kutoa hoja? Na kama humuamini, je unadhani anatosha? Na kama unadhani hatoshi (mana hili ni jibu lililo moyoni mwako 100%) kwnn unatetea uovu, una maslahi gn katika huo uovu?
 
Kuna tofauti kati ya kunyamaza na KUNYAMAZISHWA. Kunyamaza ni tendo la hiyari wakati KUNYAMAZISHWA si tendo la hiyari.

Kwa hiyo kanyamazishwa?
Lakini mbinu hiyo inafanyaga kazi kwa sababu kama angekuwa akiongea ninakuhakikishia Kila Siku huku mitandaoni pangekuwa pamoto. Memes, studio ya gen z na wanaharakati wangekuwa kazini.

Lakini kwa sasa kimya
 
MIMI HUWA NAWAAMBIA CCM INA WATU SMART SANA NA HAIPO KWA BAHATI MBAYA , UKIONA CHAMA KIMETAWALA MIAKA 60 UJUE AKILI KUBWA IMETUMIKA
 
Swali ni kwamba kwnn unadhani anapaswa kukaa kimya? Je, humuamini katika kutoa hoja? Na kama humuamini, je unadhani anatosha? Na kama unadhani hatoshi (mana hili ni jibu lililo moyoni mwako 100%) kwnn unatetea uovu, una maslahi gn katika huo uovu?

Nazungumzia hasira za watu haziangalii unahoja au hauna.
wewe uliwahi kukutana na watu wenye hasira Kali ukajifanya unahoja ukaona kilichotokea?

Wapi nimetetea uovu? Unaweza kuninukuu mkuu
 
Back
Top Bottom