Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mazingira magumu yenyewe kumbe yakujitakia kinamna hiyo!!,mi nilidhani kama yakutekwa ukatoa namba kwa jirani au mtu yeyote,bila kugundulika kwa mtekaji!!
 
Part 2:
Nilikuwa Samaki Samaki pale Mlimani City.

Napiga maji, ghafla nikaona Chuma kikali sijapata kuona aisee ubaya alikuwa na Boyfriend/Mume wake.

Basi nikamlia timing wakati wa kwenda Washroom nimfate huko huko (Mazingira ya pale kwa upande wa Washroom kuna Distance kubwa).

Basi kweli bhana Manzi akajipindua kuelekea Washroom na mimi nikaunga Tela, tulivyokunja kona tu ya kuingia corridor la choooni nikamshtua, akasimama nikamwomba namba akasema yeye ameisahau kama vipi nimpe yangu, basi akanipa simu yake nimuandikie Namba yangu..

Kumbe nyuma Bwana ake anakuja na yeye tyr kashanipa simu yake ndio niandike namba nashangaa Manzi kageuka chap kakimbilia choo cha wanawake. Mie nikawa nimesimama tu sielewi nini kinaendelea ila kwa kuwa nimesoma CUBA sikugeuka ila nikapiga jicho kwenye kioo (Reflection) nikaona mjuba anakuja ila bahati nzuri na yeye alikuwa anatembea huku anachat so hakuona tukio la mbele.

Sasa simu ninayo ya yule Manzi namrudishiaje??.. 🤣

Na jamaa kumbe alikuja kumsubir kule kule kwenye Corridor la Washroom ili arudi naye.

Mie nikajipindua Choo cha kiume kama Kawaida nikazuga zuga pale, Dem akatoka akanipa ishara ya nitulie huko huko.

Basi jamaa akarudi naye Mpaka walipokuwa wamekaa. Mie nikatoka baadae kurudi ktk meza yangu, nikamuita mhudumu mmoja hivi (Best yangu) nikamwambia nenda pale idondoshe hii simu miguuni (Mapajani) kwa yule Dada pale then uje kuna Zawadi yako hapa..

Mhudumu hakusita, alifanya hivyo na yule Dada aliiokota simu yake then.. tukaendelea kuwasiliana pale pale...

Huyu aliniletea shida sana.. mpaka nikawa naishi kama Mwizi.
Shida gani tena?
Kwa nini kwenye nyama ulipabania?
 
Back
Top Bottom