Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Part 2 aisee ni kisa kirefu kidogo..

Ila huyo Manzi baada ya kuwasiliana siku mbili tatu niligundua kuwa ni Mke wa Mtu na ametoka kufunga ndoa recently na aliyemuoa sio yule aliekuwa nae pale.

Yaan story ni ndefu ila ile Ndoa sina hakika kama ipo au La.. ila mie ndio nikawa Suspect namba moja, nilibadiri kuanzia namba yangu ya simu, Mpaka Makazi niliyokuwa naishi.
Unabadili namba Yann ,anakuwa hajaamua kukupata
 
Inaendelea..
Rayns mawardat Tiffay MIRA01 Aaliyyah Statics
Baada ya wiki kadhaa kupita kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba nilipata likizo fupi maana chuo wanafunzi walikuwa wamerudi nyumbani, mie kama mtu wa part time nilizidi kuwa free nikienda ni kwa ishu technical or short courses zile za computer. Si unajua tena mjini maokoto.

Nilipata muda zaidi wa kufatilia mawasiliano ya yule Jamaa, niliona mambo mengi sana na reports ambazo ni very confidential.. za wakuu wenzie etc.. na kutokana na hilo nikaona na mie nizidownload kwangu so nikawa na export file moja moja hasa nililoona ni potential. Jamaa alikuwa mshenzi sana maana hadi porn alikuwa anazo tena zile HD.

Nilikuwa na changamoto kidogo juu ya namna gani naweza pata access ya simu yake, hapa niwaweke wazi tu security features za Iphone zipo very strong compared na hizi Androids but haikupi guarantee kwamba eti ukiwa na Iphone huwezi kudukuliwa.. hapana. Wembe ni ule ule.

Huyu jamaa bahati nzuri alikuwa anatumia Android so sikupata kazi kubwa sana.. nilijuaje?.

Ni hivi: kama mtakumbuka wakati wa kuchunguza picha na kubaini details mbalimbali pale ndipo niligundua jamaa anatumia kifaa gani. Haijalishi hivyo tu, hizi simu zikiwa zipo na umeme na zipo standby basi muda wote zinawasiliana.

Ndio. Simu inawasiliana muda wote hata kama umeiweka hapo ukalock screen ila bado itaendelea kuwasiliana. Inawasiliana na minara, pia inawasiliana na device zote zilizokaribu yake. Naaam. Kaa ukilijua hilo kama ulikuwa hujui hapo kabla.

Sasa, kutokana na kuifanya Computer ya Jamaa kuwa ni Mzimu/Zombie hatua iliyofata ni kuitumikisha. Sawa na mchawi akikugeuza Ndondocha/Msukule anakufanya anavyotaka.. naaam.

Naomba nizungumzie kitu hapa.

Usiwe mtu wa kuacha simu yako ikiwa na utayari wa kuingiliwa. (Namaanisha nini?) Simu ukiacha Bluetooth on, Wi-Fi on, Location on.. etc tyr umeipa ruhusa ya kuingiliwa, ni kama mwanamke vile aliyetepeta kwa ulenda akisubiri kushughulikiwa tu.

Tuendelee..

Sasa, jamaa Simu yake nafkiri alikuwa ameiconnektia Bluetooth sijui alikuwa anaskiliza mziki kwa earpods or else.. ila ports za Bluetooth zilikuwa wazi. Nilichofanya ni kutengeneza Payload kupitia Computer yangu na kuinject kwenye ile system ya Computer ya Jamaa. Then nikaiamrisha iwe inafanya majaribio ya mara kwa mara (Retrial) mpaka shell ifanye binding. nakumbuka nilitumia siku nne bila mafanikio mpaka siku iliyokuja kukubali maana kulikuwa hakuna njia nyingine.

Basi, huku siku zinazidi kusogea bila mawasiliano na yule Dada, nikaamua niirudishie ile Moderm kwenye Pc nimtafute, nilimcheck kwa text moja zikajibiwa sita.

Kati ya hizo hakuna ya salamu, ni matusi na makasiriko meengi. Nilisoma zile txt, na kumjibu asiwe na wasiwasi anisikilize na tushauriane nini cha kufanya, maana bila shaka ni mjamzito tayari. Na anachohofia ni jamaa akirudi amkute ana huo ujauzito. Maana hakuwepo Mwezi mzima je wakienda kupima hospitalini na kuonesha kuwa ina umri wa mwezi na hakuwepo mjini? Na Bidada kutoa Mimba hataki.

Mie pia maswala ya kutoa Mimba siyaafiki, nikamwambia atulie na siku tuonane tuongee, aliniuliza lini? Nikamwambia atulie nitamjulisha. Ikaishia hivyo.

Huku tayari nishafanikiwa kupata access ila kwa ugumu kiasi kutokana na njia niliyotumia ni ngumu na kufanikiwa kwake ni asilimia chache ila uzuri bahati ilikuwa upande wangu, niliingiza/kupitisha mipangilio mbalimbali na kuiunga Simu yake katika ulimwengu wa Misukule ya kielectroniki.

Je unajua kwamba hata simu ukiacha hapo mezani na kuondoka kama imedukuliwa inaweza kurekodi maongezi yote au sauti zozote..? Kupiga picha bila kujua na mambo mengine.

Ndio maana aliyekuwa kachero mbobezi wa CIA bwana Edward Snowden alisema moja ya kanuni yake akinunua simu mpya ni kuondoa Camera na pia kudisable Microphone yaan kuikata waya kabisa. pia hata kwa upande wa hizi kompyuta zetu unaweza kuiona kawaida kawaida ila inafanya mambo mengi mnoo bila ww kujua.

Uzuri wa system ikiwa chini yako (Under Control) unaweza ukahamisha kila kitu ukavileta kwenye Pc yako na kujichambulia unataka nini..

Nilihamisha Txt zote, Phone/Dial log yote, na documents zote kasoro picha na videos mara nyingi hazinaga faida sana, isipokuwa kama mtu unamfanyia uchunguzi wa mwenendo wake wa kiusalama zaidi huwa hakiachwi kitu.

Baada ya kuvipata hivyo vitu nilisoma jumbe nyingi nikaja kugundua jamaa ana familia nyingine, pia ana Wanawake wengi tu wengine kawapangishia nyumba, mbaya zaidi ana mishe za kimafia (Sitaziweka wazi).

Basi, niliandaa folder nikaliencrypt vizuri na kutunza nyaraka za muhimu humo, huku nikijipa matumaini ya ushindi wa hii ishu.

Baada ya siku kadhaa Jamaa alirudi Tz, akawa anaendelea na harakati zake huku akiacha kabisa kumpeleka Mkewe kazini kama mwanzo (Alikuwa bize sana). Mkewe nae akawa free kiufupi jamaa alivyorudi alibadirika na kumuacha mkewe awe huru kama mwanzo.

Bidada aliforce tuonane na mie bila hiyana nilimkubalia, na hiyo siku ilikuwa siku ya kazi baada ya yeye kutoka kazini tulipanga tuonane pale Lumumba Grill.. tupate Sekela maana na mie nilikuwa maeneo hayo siku hiyo.

Story zilinoga maongezi mengi na mipango mingi, ingawa nilimsihi sana asitoe ujauzito niliompa maana ninaham sana ya Mtoto.. pia sipendi huo utaratibu. Alinielewa na kunihakikishia hilo.

Muda ulisogea sana ilikaribia saa 4 kasoro ndio akaanza kutoka pale, mie nilienda Mnazi mmoja kama kawaida yangu nikakamata daladala nikaelekea kwangu na yeye alidrive kuelekea kwake. Baada ya kufika nyumbani alikuta Mumewe kasharudi na kavimba kama kiboko.. kwa maelezo yake ni kwamba alipita kazini kwake siku hiyo hakuikuta ile gari pale nje, aliuliza walinzi wakasema ameshaondoka, Mume wake hakumpigia simu alinyoosha nyumbani na huko hakumkuta akasema atulie labda foleni.. ila kwa ule muda ni dhahiri alikuwa kapitia sehemu.

Jamaa hakutaka kuelewa ni matusi na mabishano ndani, na Mwanamke tena akiwa kakuchoka ni mbaya zaidi, akamjibu vibaya basi jamaa hakujiuliza mara mbili alimpiga sana mpaka kuzimia. Yaliendelea mambo mengi hapo kati ila mie nilikuja kujua baada ya kuona baadhi ya text anazotuma yule Jamaa kwa rafiki zake kwamba mkewe amelazwa anaumwa na mambo kama hayo.

Nilipata alert. sasa ni mke yupi ? maana jamaa inaonesha ana Mke mwingine nje ya yule pia ana Wanawake wengine. Nilifatilia kwa ukaribu nikabaini ni yule yule ambae anaishi nae. Akili iliniruka sana imekuaje ghafla kalazwa?.

Wiki nzima sina Amani na Jamaa mawasiliano ya simu hasa upande wa Sms za kawaida alipunguza, na kwa nature ya udukuz wangu kuingia ndani ya 3rd party app kama whatsapp ni ngumu kutokana na app privileges. Ilibidi niwe mpole na kufatilia baadhi ya maongezi na txt kadhaa.. sikupata kitu. Nikawa nawasi wasi zaidi.

Nitajua vipi yule Mwanamke kalazwa hospital ipi na kwa ishu gani? Maana nilikuwa napata text tuu ila kusikiliza mawasiliano ilikuwa ngumu.

kitu kingine ni kwamba huu udukuzi unategemea Internet, hivyo akizima data sipati kitu, na mara nyingi alikuwa anafanya hivyo anazimq zima data so nikawa nachelewa kupata taarifa za msingi, na kwa haraka.
Nilichofanya ni kumvizia siku kawasha data muda mrefu na kuingia ktk mfumo wa mipangilio ya mawasiliano kumwelekeza kibra, kuna kitu kinaitwa Call divertion.

Ni hivi: Kuna settings nyingi zipo ndani yake ila ipo moja ambayo unaipa sharti kwamba simu ikipigwa na hiyo simu yako kama haipo hewani basi ielekeze hiyo simu (Incoming calls) kwenye namba fulani. Same applies ikiwa unatumika/busy basi simu nyingine itaita kwenye number fulani ambayo umeiingiza au isajili kule kwenye settings. Pia kuna secret codes ambazo inafanya Call duplication yani itaita kwako itaita kwa mdukuzi. Ila akipokea mmoja ni kote itaonyesha simu inaongea yaani simu inajipokea, na sauti itachukua kote kwa wakati mmoja. Hii wanatumia sana Majasusi wa Kisiasa or Mapenzi...

Nimechoka kuandika.. nitaendelea.
Tunaendelea...
Rayns mawardat Tiffay Aaliyyah MIRA01 Statics

Baada ya muda wa wiki mbili kupita, nilipokea ujumbe kupitia utaratibu wangu kama kawaida, nilimjua mtuma ujumbe maana ndio mtu niliekuwa nawasiliana nae mara kwa mara, ujumbe ulikuwa mrefu na wa huzuni sana.

Mimba ilitoka kutokana na majanga aliyoyapata, pia aliumia kawaida maeneo ya kichwani na mgongoni kidogo maana wakati anaanguka baada ya kupigwa na kusukumwa alianguka kinyume nyume. Nilimpa pole kwa aliyoyapata na mimi nilipata hasira sana maana mtoto wangu/damu yangu ishapotea kijingajinga tu. Hamna noma, nilimuuliza yupo wapi kwa sasa, aliniambia yupo kwao kwa muda ili apate uangalizi maana hata damu ipo chini anahitaji kula na kupumzika vizuri.

Basi, nilimtakia kila la kheri ktk likizo yake ya kujiuguza. Niliendelea na mambo yangu na kufatilia mawasiliano kwa kila nukta. Bahati mbaya sikuwa nafatilia Emails zake kwa sana kama ninavyofatilia mawasiliano ya kawaida (Private). Nilifanikiwa kunasa namba ya simu ya mke wake mwingine naona huyu ndio mkubwa maana ana watoto watatu alishazaa nae na inaonekana yule mwingine hamjui wala hawajui hao watoto.

Pia, ana nyumba ipo Msasani ndipo anakaa huyu mke wake, kwa kuwa yule mwingine ni mgonjwa anatumia muda mwingi kwenda huko Msasani, nilipata picha na maongezi ya sauti pia hadi nyumba niliijua ilipo maana kuna siku nilikuwa na safari ya huko nikapitia kuiona na nyumba ilipo.

Ni hivi: kupitia ile system ya Track Me ISW Version unaweza kutrack real time location na pia ni wapi target wako anatumia muda mwingi kukaa eneo moja.

So kwenye database inanipa Kule Tabata, inafata Kazini kwake na pia sehem nyingine ni huko Msasani.

Kuna siku nilikuwa nimechoka tu kufanya mambo ya msingi nikaamua kupitia kwenye baadhi ya picha niliziexport kutoka ktk Drive yake hasa ktk folder 📂 la Downloads, nilikutana na picha za porn na videos kama zote pia nikakutana na picha ambazo sikuzielewa.

Kivipi? Kuna picha zilikuwa kama picha tu za ajabu ajabu yaan picha ambazo wewe ukiziona huwezi zielewa ila siku shangaa nikajua tu sometimes kila mtu ana mapendeleo yake.. ila kilichokuja kunishtua ni vitu vifuatavyo.

1- zile picha ni za mfanano yaan zinajirudia rudia

2- Zina KB/Size ndogo yaan picha moja unakuta ina kb 5 au 8.5

3- Jina: hizi picha zilikuwa zinaonyesha kabisa zilikuwa zinaseviwa kwa jina yaan sio kama zile za mwenye website utazidownload tu zikiwa hazina uniformity hizi zina uniformity na zilikuwa na code mwishoni. Mfano (Notice waves Capricorn x001) sasa inayofata unakuta (x001B) kitu ambacho ni mtu anasave kwa maksudi na sio kwamba ni system generated file names.

Nilitumia siku 3 kuzielewa zile picha, nikatoka kapa. Nilirudi katika Downloads nikafatilia zimeshushwa (Downloaded) lini nikaona ni ndani ya siku hizo hizo na siku hiyo ilishushwa moja nyingine.

Nilichofanya nikaingia ktk browser apps nikazama ktk history nikakutana na emails za baadhi ya website ambazo hazina uhusiano na yale niliyoyaona au niliyotaka kuyaona zaidi.

Nilikosa kujua ni wapi exactly chimbuko la hizo picha.

Nilitumia siku nne zingine bila mafanikio na kila siku zinakuja mpya. Niliingia ktk Emails upande wa inbox kuona emails zilizokuja na attachments sikupata kabisa nilichotaka.

Niliumiza kichwa mno, finally nikaamua kuingia ktk utumbo wa System.

Kuna kaelimu kidogo hapa, katika ulimwengu wa Cyber Forensic kuna trick na njia nyingi za kubaini uhalifu au abnormalities, na Operating system (Os) zimeundwa kama mfumo wa Binadamu ulivyo.

Kwa system kama ya Windows kwenye root folder upande wa system32 kwa ndani unakutana na mambo mengi kuna kitu kinaitwa Registry.

Hii Registry ni nini?
Hii aisee inatunza data na mipangilio ya programu za kompyuta, humu ndo zinakaa secret codes na mambo mengine ya msingi sana ya OS. sasa kuna utaalamu wa kuihamisha file la registry kwa kuligawa vipande vipande ili kulifanyia deep analysis.

Baada ya kufanya analysis kupitia Forensic tools mbalimbali nilikuja kujua kuwa jamaa anatumia sana incognito mode. Pia jamaa anafuta futa sana history ya browser na pia jamaa ana VPN mbili. Moja ni ya ofisini na nyingine ni custom made VPN ambayo anakuwa anaitumia mara moja moja sana.

Nilifanya utafiti wangu na kuja kupata hitimisho huyu jamaa hakuwa mtu wa kawaida kabisa.

Kupitia deep analysis kwenye registry files and other config files niliona ni wapi zile picha zilikuwa zinatokea, kuna link ambayo ni temporary email ambayo inakuwa generated automatically, hii link inakuja immediately after kuwasha ile VPN yake then analogin ndipo anapata access ya hiyo portal, pia portal haifunguki mpaka achomeke key, mfano USB Drive au SD Card ambayo imeprogramiwa kwa sababu ya authenticity. Ilinipa kiu zaidi kufahamu zile picha zinamaana gani.

Je wajua kuwa unaweza pandikiza ujumbe/Message ya SIRI ndani ya picha?

Naam kuna utaalam wa kutumia picha na kuipandikizia ujumbe ambao kwa mtu ambae hajaambiwa hawez jua. Ule ujumbe pia huwezi kuusoma mpaka software maalumu ambayo inadecode hiyo information ktk picha, sio hivyo pekee pia unahitajika kuweka password za ku decrypt file lilipandikiziwa ndani ya picha.

Pia unaweza kujibu huo ujumbe na kuirudisha picha kwa aliyekutumia.

Hii njia inatumika na Majasusi au watu wenye mambo ya Siri kupitiliza ikiwemo magaidi pia.

Nilitambua hilo, ingawa nilishindwa kufungua file na kusoma mpaka niwe na codes za kufungulia hilo file (Decryption).

Sasa nilipata kazi tena ya kutumia Akili zaidi kufanikisha hilo, niliwezaje?

Ni hivi: kwa kuwa nina system yake kiganjani, basi nilikaa chini na kuunda Spyware ambayo ni kundi la Keylogger.

Keylogger ni nini?
Huu huwa ni mfumo wa kidukuzi ambao unatumika kucapture/kunyakua kila kinachoandikwa. Mfano akiandika chochote basi huu mfumo unanakili nakusevu ktk format ya txt. Baadae mdukuzi anafatilia patterns na kunyakua taarifa za muhimu kama vile passwords etc.

So mie niliamua kupandikiza hilo dubwana na matokeo niliyaona baada ya wiki, maana alifungua (Decrypt file/Picha) kwa kutumia password. So zilijihifadhi kwenye txt file na mie baadae nilifanikiwa kuzipata na kufungua hizo picha moja baada ya nyingine na kujionea mambo ya kustaajabisha sana.

Sitayaweka yote wazi, ila moja wapo ni Biashara ya Madawa ya kulevya, ambayo alikuwa anashirikiana na baadhi ya wakuu niishie hapo kwenye neno WAKUU.

so kuna mtandao ambao upo very secured pia very sensitive. Huo mtandao wao wanawasiliana wao kwa wao na kwa usiri wa hali ya juu. Nilitunza taarifa zangu pia kwa usiri zaidi na kuamua kuwa mtulivu.
Pia nilibahatika kupata password za Bank zake mbalimbali maana alikuwa anatumia Password Vault ya Microsoft.

Baada ya hayo yote nilisubiri muda muafaka wa kuamua nini cha kufanya baada ya kukusanya taarifa za muhimu.
___________________________
Msione kimya aisee... nipo very busy na vimeo, I hope next episode itakuwa ya mwisho mwisho..

Itagusia ni namna gani nilimaliza ugomvi na kuwa huru, pia hizo taarifa nilifanyia nini? Pia yule Dada nilimalizana nae vipi.
 
Back
Top Bottom