Mbinu za kuishi mitaa ya kihuni, uswahilini

Mbinu za kuishi mitaa ya kihuni, uswahilini

Mtoa mada asipingwe alikuwa muhuni maeneo hayo...halafu we jamaa nakumbuka ulinipiga roba ya mbao yenye misumari ukaondoka na begi langu pamoja na manzi niliyekuwa naye..naomba uniludishie begi langu nimeshakufaham
Aaah unanitafutia matatizo na police
Ujue Kamanda Murilo yupo anasoma comment yako
 
Wanasemaga kambi popote
Kuna watu hawawezi kuishi hata siku mbili tu maeneo yaliyopinda, wanaogopa wahuni na vibaka, sijui panya road

Nishawahi kuishi Dar nikiwa na familia yangu huko Mbagala na lilikuwa kipindi cha panya road, hakuna muhuni alisumbua

Hapa nitawapa mbinu kadhaa

1. Unapoombwa hela na wahuni usiwape.

Wahuni Huwa wanapenda kutikisa watu Kwa kuwapima msimamo wao.
Anaweza akakwambia. Oyaa Uncle nigei jero ya fegi Mjibu huna au hutaki yaani isionekane ni haki kupewa kazi Bure

2. Shiriki mambo ya kijamii ya wahuni.
Wapewe michango kama ya mechi za ndondo, shughuli zao n.k

3. Kuwa mbabe kiasi
Itokee hata mhuni akizingua unampasua

4. Rudi usiku bila hofu
Ili wahuni au vibaka wasikuumize, we uwe na utamaduni wa kuingia na kutokea chimbo zao bila woga

5. Wajue wahuni baadhi
Ili wahuni wasikuumize we wajue wenzao kadhaa kwenye mtaa hata wakujue Kwa jina labda braza Salum

6. Usikae home Kinyonge
Labda weekend upo unafua na kukaangiza, hapo wahuni watakulia timing na watakuchukulia vyako

7. Fanya mazoezi nao
Kama ni kupiga chuma, muulize muhuni chimbo zao za kupiga chuma ni wapi, nenda pale kiwashe hadi wakutambue kuwa huyu si mnyoge

8. Juana na wazazi au ndugu zao

9 . Wakosoe wanapokosea na watishie kuwa unaweza kuwaadhibu, hapa watakuheshimu
Wewe ni mpumbavu na hakuna code hata moja unayoijua kuishi na machizi boti.

Hujajaa wewe kwenye 18 zao.
 
Wahuni sio watu wazuri pia hawana ujamaa ukiwapa chance ya kuwa karibu na wewe na ndivyo unawapa chance ya kukuumiza labda uwe apeche alolo
 
Kaa nao mbali kadri unavyoweza.
Wana akili fupi sana hao jamaa, kuna ambao hawana cha kupoteza, kukutia beto la tumbo kwa kosa la kipuuzi hawaoni kazi.

Wanachomana sana visu hao jamaa, ila habari hazisambai kwasababu ya status yao ya uhuni.
Mmekosana kidogo tu, wanaanza kusakana wachomane visu kuoneshana ubabe wa kijinga.

Ishi maisha yako tu na sio uish ili wahuni wakuone mwamba au mbabe, hujui kua kila mbabe na mbabe wake??
Mtoa mada anasema tu hawajui nimezaliwa na kukulia Kiwalani na hao wengi najuana nao sababu wakati tunakuwa tumeonana.Moja ya tukio ni ugomvu wao wenyewe mmoja alishika mpira wa nje wa baiskeli uliokatwa akitumia kumchapa mwenzie na mwingine alishika visu viwili akajaribu kumtoboa au kumchana mwenzie na ilikuwa usiku raia wote tuliwaangalia tu nani aingilie mpaka mama mzazi wa mmoja wao kuingilia vinginevyo tungeona maiti.
 
Mtoa mada anasema tu hawajui nimezaliwa na kukulia Kiwalani na hao wengi najuana nao sababu wakati tunakuwa tumeonana.Moja ya tukio ni ugomvu wao wenyewe mmoja alishika mpira wa nje wa baiskeli uliokatwa akitumia kumchapa mwenzie na mwingine alishika visu viwili akajaribu kumtoboa au kumchana mwenzie na ilikuwa usiku raia wote tuliwaangalia tu nani aingilie mpaka mama mzazi wa mmoja wao kuingilia vinginevyo tungeona maiti.
Hao walikuwa wamedata
 
Watu gani hawapendi utambulisho wao,eti kinyesi kisoda kanali, kijonitel, mizuna, kipande, geza, kibuyu, mudipa, pengo, jogoomsela, kitopaz, n.k
 
Back
Top Bottom