Jamii yetu imekuwa na vijana wa ovyo na walegevu mno
Furahia ya wazazi ni kuona kijana wao anapambana na kujitegemea.
Wazazi wanapenda wafurahie uzee wao bila kubanwa na nyie watoto, wazee wanahitaji wakae sebuleni wapate mabusu moto moto, Sasa jitu zima upo kwenu kuwabana wazazi
Kijana anafikia miaka 25+ Bado yupo Kwa wazazi, anakula Kwa wazazi, analala Kwa wazazi na hapo hana mpango wa kuoa, kuwa na biashara au kazi ya uhakika
Wazazi wetu walitumia mbinu hizi na vijana tuliondoka nyumbani bila kupenda na kwenda kujitegemea
1. Fanya chumba cha kijana kuwa stoo.
Yaani hapa weka mahindi, karanga, maharage, huko usiku atapambana na panya na mende,
Akili itamjaa ataamua kujitegemea
2. Hifadhi mziga wa nyuki humo chumbani,
Ataondoka tu
3. Mpangie muda wa kurejea nyumbani, mfano mpangie hapo kwako kabla ya saa 1 usiku kila mtu awe nyumbani akizidi hapo atafute pa kulala
Vijana wanapenda uhuru akiukosa kwako laZima autafute pengine
4 Mnyime uhuru wa kutumia vitu vidogo kama redio na TV
5 Mpe maneno ya fedheha
Mfano jitu zima unakula ugali wa mama
6. Vunja kitasa cha mlango, mfanyie upekuzi wa Siri zake.
Kwa mbinu hii ya maudhi laZima akupishe
7 weka mifugo kama kuku na bata humo chumbani
Jogoo wakiwika alfajiri ataamka na hakika atakupisha hapo kwako uzidi kufurahia uzee na mama yake
8 Usimpe chakula cha kutosha
9 Nuna/ kasirika bila sababu
Usimchekee vaa sura ya kamanda Mliro muda wote
Hapo laZima aondoke
10. Mpe majukumu ya house girls
Aoshe vyombo, afagie, akusanye mayai n.k
Hapo laZima aondoke