Mbinu za kupika sotojo / rosti la kitimoto, unaweza kula mpaka ujiume ulimi... Enjoy

Yaaani mbaya.....
Nimeitest Kwa picha...
Hajui rosti huyu
Hamna hiyo ni picha ya niliyoipika wiki 4 nyumaa... leo nimepika imekuwa safi zaidi... halafu mzikute nyie ndo hamjui kupika...

Mimi nikila chakula karoti na hoho huwa hazitakiwi kuiva sana ili zisipoteze vitamin.. ndo maana labda mnaona msosi hauvutii... ila ladha yake sio ya kawaida....kushinda hata kile wanapika cha kuuza
 
Ukimpata rosti la kazimoto pork.....utapiz wewe kama hiyo hapo unaona ni kazi kazi
Sawa mkuu... ila hiyo ni variety moja ... kuna ya mchicha pia nikipika ni hatari... kwenye mapishi nipo vizurii
 
Uzuri wa kitimoto hakinaga makeke mengi hata ukikosea kuipika bado taste yake haiwezi kufanana na kuku iliyopikwa kiufundi
Yaaani upo sahihi mkuu, ikishalainika tu kwa kuichemsha na kama uliweka limao basi inakuwa na taste nzuri..

Hapo ni kwenye mboga tu usikozee, lazima uienjoy
 
Habari wakuu, kwa wale wadau wa hii nyama yetu pendwa, ngoja leo nikupe mbinu.

1. Nunua nyama yako, ni vizuri kama atakukatia katia pale.

2. Weka nyama kwenye sufuria, weka na maji, halafu anza kuisuuza ili uondoe vile vimifupa vidogo vidogo.

3. Weka nyama kwenye sufuria safi, kisha kamulia limao, tia na chumvi halafu uichanganye.

4. Washa jiko lako la gesi uibanike ukiwa umeifunikia. (Usiweke maji kwanza)

5. Itachemka kwa kujichuja maji yenyewe. Kama haina mafuta sana yale maji ya kwanza yakikauka hapo unaweza sasa kuweka maji mengine na uiache walau kwa dakika 25..... kama ina mafuta sana, mimi huwa nachofanya siongezi maji bali naacha mpaka zile nyama za mafuta zinajichuja mafuta na kuanza kujikaanga... hapo sasa ni kukoroga ili isishike chini, ikianza kubadili rangi... ondoa kipande kimoja kimoja uweke pembeni...

6. Chukua sufuria mpya kaanga kitunguu, kikiva kidogo weka karoti, hoho kwa pamoja na uweka na pili pili ambayo umeikatia katia vipande vidogo vidogo...

7. Baada ya hapo, weka ile nyama kwenye mchanganyiko wa karoti na hoho halafu uikorogo mpaka ichanganyika vya kutosha.

8. Ikishachanganyikana, weka nyanya ili kutengeneza mchuzi.

9. Endelea kuchanganya, usifunikie kwa sababu haina maji itashika kwenye sufuria, wewe koroga tu vya kutosha.

10. Mchanganyiko ukikolea, sasa weka maji kidogo sana na ukoroge, ukiona mchuzi kidogo unejitengeneza, basi waweza funikia kwa dakika moja au moja na nusu...

11. Kisha funua na endelea kukoroga kwa dakika kama tatu zingine, na chakula chako kitakuwa tayari.

12. Huwa inapendeza kama utakula na ugali, ndizi za kukaanza, au Chipsi yote inaenda vizuri sana. Pembeni ukiwa na parachichi itapendeza zaidi.View attachment 2752470
Shukrani mkuu, nitajitahidi next weekend nifanye haya mambo
 
Kitu ichi apa 😋😋😋
IMG_20230917_185830.JPG
images (3).jpeg
 
Habari wakuu, kwa wale wadau wa hii nyama yetu pendwa, ngoja leo nikupe mbinu.

1. Nunua nyama yako, ni vizuri kama atakukatia katia pale.

2. Weka nyama kwenye sufuria, weka na maji, halafu anza kuisuuza ili uondoe vile vimifupa vidogo vidogo.

3. Weka nyama kwenye sufuria safi, kisha kamulia limao, tia na chumvi halafu uichanganye.

4. Washa jiko lako la gesi uibanike ukiwa umeifunikia. (Usiweke maji kwanza)

5. Itachemka kwa kujichuja maji yenyewe. Kama haina mafuta sana yale maji ya kwanza yakikauka hapo unaweza sasa kuweka maji mengine na uiache walau kwa dakika 25..... kama ina mafuta sana, mimi huwa nachofanya siongezi maji bali naacha mpaka zile nyama za mafuta zinajichuja mafuta na kuanza kujikaanga... hapo sasa ni kukoroga ili isishike chini, ikianza kubadili rangi... ondoa kipande kimoja kimoja uweke pembeni...

6. Chukua sufuria mpya kaanga kitunguu, kikiva kidogo weka karoti, hoho kwa pamoja na uweka na pili pili ambayo umeikatia katia vipande vidogo vidogo...

7. Baada ya hapo, weka ile nyama kwenye mchanganyiko wa karoti na hoho halafu uikorogo mpaka ichanganyika vya kutosha.

8. Ikishachanganyikana, weka nyanya ili kutengeneza mchuzi.

9. Endelea kuchanganya, usifunikie kwa sababu haina maji itashika kwenye sufuria, wewe koroga tu vya kutosha.

10. Mchanganyiko ukikolea, sasa weka maji kidogo sana na ukoroge, ukiona mchuzi kidogo unejitengeneza, basi waweza funikia kwa dakika moja au moja na nusu...

11. Kisha funua na endelea kukoroga kwa dakika kama tatu zingine, na chakula chako kitakuwa tayari.

12. Huwa inapendeza kama utakula na ugali, ndizi za kukaanga, au Chipsi yote inaenda vizuri sana. Pembeni ukiwa na parachichi itapendeza zaidi.View attachment 2752470
Mzee kama haya maelekezo ndio yanazalisha hicho ambacho nakiona kwenye hio sahani hapo basi una safari ndefu sana katika tasnia ya rosti ya mdudu.
 
Back
Top Bottom