Mbinu za kupika sotojo / rosti la kitimoto, unaweza kula mpaka ujiume ulimi... Enjoy

Mbinu za kupika sotojo / rosti la kitimoto, unaweza kula mpaka ujiume ulimi... Enjoy

Habari wakuu, kwa wale wadau wa hii nyama yetu pendwa, ngoja leo nikupe mbinu.

1. Nunua nyama yako, ni vizuri kama atakukatia katia pale.

2. Weka nyama kwenye sufuria, weka na maji, halafu anza kuisuuza ili uondoe vile vimifupa vidogo vidogo.

3. Weka nyama kwenye sufuria safi, kisha kamulia limao, tia na chumvi halafu uichanganye.

4. Washa jiko lako la gesi uibanike ukiwa umeifunikia. (Usiweke maji kwanza)

5. Itachemka kwa kujichuja maji yenyewe. Kama haina mafuta sana yale maji ya kwanza yakikauka hapo unaweza sasa kuweka maji mengine na uiache walau kwa dakika 25..... kama ina mafuta sana, mimi huwa nachofanya siongezi maji bali naacha mpaka zile nyama za mafuta zinajichuja mafuta na kuanza kujikaanga... hapo sasa ni kukoroga ili isishike chini, ikianza kubadili rangi... ondoa kipande kimoja kimoja uweke pembeni...

6. Chukua sufuria mpya kaanga kitunguu, kikiva kidogo weka karoti, hoho kwa pamoja na uweka na pili pili ambayo umeikatia katia vipande vidogo vidogo...

7. Baada ya hapo, weka ile nyama kwenye mchanganyiko wa karoti na hoho halafu uikorogo mpaka ichanganyika vya kutosha.

8. Ikishachanganyikana, weka nyanya ili kutengeneza mchuzi.

9. Endelea kuchanganya, usifunikie kwa sababu haina maji itashika kwenye sufuria, wewe koroga tu vya kutosha.

10. Mchanganyiko ukikolea, sasa weka maji kidogo sana na ukoroge, ukiona mchuzi kidogo unejitengeneza, basi waweza funikia kwa dakika moja au moja na nusu...

11. Kisha funua na endelea kukoroga kwa dakika kama tatu zingine, na chakula chako kitakuwa tayari.

12. Huwa inapendeza kama utakula na ugali, ndizi za kukaanga, au Chipsi yote inaenda vizuri sana. Pembeni ukiwa na parachichi itapendeza zaidi.View attachment 2752470
Mimi mvaa makobazi nahusika kweli hapa,labda kuonja lakini si kushiba.
 
mabanda ya kuchoma nguruwe yanatoa harufu kali sana midhili ya samadi au uvundo wa mboji
Ya vibandani kweli hawafuati taratibu.... cha kwanza huwa hawaoshi... nunua mwenyewe buchani halafu ufuate miongozo
 
Haya sasa, wate mlioponda upishi wangu leo nime rewind nimeliamshaa... Mlioniponda njooni hapa mnipe maua yangu... Formula ya mapishi ni ile ile niliyoweka.

Atoto Smith Rowe Eneliah Glenn Lavit Mpaji Mungu ephen_ masai dada Scars Ironbutterfly To yeye Dr hyperkid Missy Gf Half american Extrovert Ngongo Matawi ya juu MamaSamia2025 Lewis MVincent

20230924_173746.jpg
 
Back
Top Bottom