Mbinu zipi wamezitumia Wakinga kuwa wafalme Kariakoo?

Umeelewa mada.... inaonekana wewe sio mwenyeji wa kariakoo...
 
Kugawa mtaji kwakweli naona pesa haitatosha kwasababu hata huo mtaji niliokuulizia sio wote wangu si unajua huku mikoani kuna namna fulani ukijiweka watu wanakuletea akiba zao uwatunzie wakishauza korosho zao
Sasa kaka mpaka hapa ninachokiona ni jela unatafuta au kulogwa!

Uanaume ni kuingia front bila woga lakini kwa case yako hapana sikushauri,cha kufanya jichange upate angalao 50mill uingie ukiwa na cash yako hiyo ya wa mikoani endelea kuzungushia kwenye mazao kazi uliyoizoea.
 
lIgi za kitoto kila pahala.....
Utaskia wachaga ni wasomi,
Uchagani kumeendelea,
Wachaga wanatawala Biashara wachaga this wachaga that.
Anayesema hivyo unamkuta amelost yupo kama sie tu.
Mfano huu uzi Ulianzishwa ukiuliza kuhusu wakinga ( bado haina maana kufanya hivyo "ujinga") ila walikotokea wachaga.......
Wachaga biashara hivi wachaga maghorofa vile.
Yanini hayo? Unanufaika nini?
Unapata kini ukitambulika kwa kabila?
 
Hamna kaka siwezi kufungwa hawa wanaoniletea pesa zao ni wazee wangu kule kijijini unakuta mtu anauza korosho za milion 10 yote anakuletea umtunzie kwahiyo utakuta anachukua polepole tu na hawi mmoja wanafika mpaka wazee 12,huyu anakuletea milion 10 mwingine 6 mwingine 5
 
Mkuu una hakika GNM ya mchaga?GNM ya mkinga na hizo herufi ni initials za majina yake.Toka cargo yake ya kwanza Baiyun area,Guangzhou before 2014 huko naijua mpaka ilipo leo Nanhai Foshan
 
Sawasawa mkuu nimekuelewa,basi jitahidi kabla hujaitia hiyo hela kwenye biashara utakayoipenda ufanye kwanza uchunguzi wa mazingira ya pale town kwamba location ipi ni sahihi gharama za frame etc ili ukiingia iwe nyepesi kwako.
 
Kugawa mtaji kwakweli naona pesa haitatosha kwasababu hata huo mtaji niliokuulizia sio wote wangu si unajua huku mikoani kuna namna fulani ukijiweka watu wanakuletea akiba zao uwatunzie wakishauza korosho zao

Kama uko kwenye mazao jitahidi sana uanze kudeal na stock za mazao kama mpunga, ukanunue songea namtumbo kitanda huko au mbarali mbeya au kyela au kamsamba iko songwe, alizeti unanunulia hata songea, mtama mweupe mbeya unaenda kutafiti tu ununuzi usimame mwenyewe na namna ya kutunza uahkikishe mazao yako salama, ukiweka kwenye mavuno miezi minne mbele unapiga pesa, biashara ya kariakoo ina umafia sana na ukienda nenda na pesa kidogo ugange tu kama machinga huku ukisoma game kwanza baadae ndio utafute frem lakini wale wanaomwaga nje ukipata namna ungana nao utasoma mchezo kabla ya kutafuta frem yako
 
Duuuh, wenyeji hasa wa DSM yaani Wazaramo wako wapi?

Au walikuwa wapi?

Sorry, sijauliza kwa nia ya kuwadharau
 
Aise uneichambua vema kariakoo
 
Umetisha mkuu. Kuna nyuzi humu watu wengi tunapend kujua machimbo ya bidhaa Kariakoo kam hardware, electronics nk. Nadhani wewe uko vizuri zaidi kutuelekeza.
 
[emoji3581]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…