realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi kuanzia kidato cha tano na Sita wanadhani Maisha ya Chuo ni ya Starehe sana bila kujua undani wake.
Baadhi ya wanafunzi huenda Chuo wakiwa na matumaini makubwa sana ya kutimiza ndoto zao.
Lakini Ndoto hizo hukwamishwa na vitu vingi hasa kwa wale wenye tamaa na pupa.
Kwa kuanza na watoto wa kike ambao huwaona dada zao wamemaliza Chuo na kurudi nyumbani na watoto hutamani na wao wafanye hivyo bila kujua madhara yake.
Mara nyingi wanapoanza Mwaka wa Kwanza huwa ni wanafunzi wapole na watiifu.
Lakini baada ya Muda kidogo makundi hujigawa na kuanza kuonyesha tabia zao halisi.
Mara mtoto wa kike anajikuta amenasa mimba kutoka kwa mtu asiyemtarajia, anaishi na mimba kwa kumficha mzazi wake hadi anajifungua.
Changamoto katika hilo huanza pale atakapokosa matunzo kutoka kwa mhusika aliyekutana nae Chuo.
Kiwango cha masomo kinashuka, maisha huanza kuwa magumu na badala ya kuzingatia masomo na kutafuta fursa za ajira unazingatia malezi malezi zaidi.
Wazazi wanashindwa kupata kile walichokitarajia kutoka kwa mtoto wao kutokana hizo changamoto anazokumbana nazo.
Mnachopaswa kukifahamu watoto wa Chuo hao watu mnaokutana nao Chuo tayari walishadanganya wanafunzi wengi waliopita hapo.
Mnapaswa kukumbuka kuwa nyie sio wa kwanza. Umakini unapaswa kuchukuliwa mapema zaidi.
Maisha ya Chuo ni kusoma na kutafuta Fursa na sio kulea watoto.
Ingawa kuna wachache waliofanikiwa baada ya kupambana sana.