Mboga nilioikuta Tanga sijawahi kuiona popote, ni mbaya

Mlenda kuna wa majani , kuna wa bamia (waweza weka na ngogwe na nyanya kidogo), Kuna wa unga ambapo unavunwa maporini unakaushwa Na kutwangwa kwenye kinu kisha kuchekecha kupata unga.
Huo unga sasa unaunga ukisha chemsha maharagwe, kunde, mbaazi, machaga, ngwala, ndulele au ntula n.k.

Ni tamu usipime.

Hata ukiwa Na malaria hamu ya kula ikakata Kwa mlenda utakula ugali mpaka basi.

Ni appetizer nzuri hujapata kuona.

Na Kuna ule mlenda wa mkubugwa.

Huo ni ule wa haraka haraka faster wa kuweka Maji ya moto na unga tu labda na Ngogwe au nyanya.

Pia wengine hutumia wanapo ruzu.

Kwamba ameweza kupata unga uwezo wa kupata mboga hana na njaa imembana watoto wanalia njaa, mkubugwa unaandaliwa haraka.
 
Vipi wewe, si ungeomba upewe hata uono au samaki wa kupaka?
 
Hivi Kwa Nini mnasemaga mlenda ni mtamu?
 
Tanga Kuna Nani Palee Mbona Kila Kitu Kimekufaa
 
Yaani ndulele na tula si zile kama nyanya chungu tunachezea mdako,zinaliwa kwani?
 
Wamevhanganya na dawa za kimapenzi yaani Limbwata mradi umekula Tamga huondoki na utakuwa unaota Tanga tu

Hilo libwata wameunga hadi wametipitiliza viwango vya TBS vya wazee wa Tanga mpaka unaiona mboga mbaya
😂 🤣 😆 😄
 
Watu tunatofautiana aisee,
Yaani mimi kabichi hata ichemshwe tu na chumvi kwa mbali nitakula iwe kwa ugali au wali nitafurahia mno.

Naipenda sana kabichi.

Ipikwe ichanganywe na nyama au yenyewe tu naipenda mno.
Cabbage ni kwa ajili ya wanyama kama sungura na nguruwe.

Ile sio mboga.
 
🤣🤣🤣🤣🤣Umepata kisingizio au sio
Yani Nina kisingizio kizuri kabisa.

Ugali na kabichi nafaulu vipi vzr?

Kuna sehemu inaitwa "sukuma wiki "... Sasa Mboga inasukuma wiki,just imagine
 
Tanga kuna,zao la chai,wangekuchumia majani ya chai kidogo wakatia nyanya ukala ukashiba, pole sana kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…