SI KWELI Mboga za majani aina ya Chainizi husababisha upungufu wa Nguvu za kiume

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Ka
ma mimi nazifakamiaga kinoma na sijaona madhara yoyote, labda wataalam waje na neno hapa tuelimike.
 
Sijajua ni nini ila hiyo mboga nikikutana nayo naitandika bila wasi
 
Eti inasababisha mnara unasoma 2G
 
Ni ushamba. Mtu anakataa kula chinese huku anabugia mayai ya kisasa, unabugia energy, unabugia broiler.

Anyway, turudi kwenye uzi.

Sababu haswa ni kuwa wameaminishana kuwa chinese inamaliza nguvu za kiume. Wakose nguvu wasingizie mboga.

Je, ni kweli Chinese inamaliza nguvu za kiume? Jibu ni ndiyo na hapana.

Nitaanza kwa sababu gani ni HAPANA.
Mboga za majani aina ya Chinese pamoja kuwa na madini ya chuma, calcium na magnessium, pia ina vitamin A, K1, C na Folate.

Kwa taarifa tu ni kuwa, madini na vitamini hizo tajwa, zinasaidia sana kwa afya ya moyo, na utengenezaji wa chembe nyekundu za damu. Kwa swala la nguvu za kiume, moyo na damu ndizo hufanya kazi kubwa sana katika kufanikisha tendo husika kufanyika kwa viwango.

Sasa ya nini tuilaumu Chinese?
Ni ujuha.

Turudi sasa kwenye swala la NDIYO inasababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Chinese kama ilivyo mboga zingine, zinakuzwa haraka kwa kutumia madawa pamoja na mbolea nyingi.

Hii hufanywa na wakulima kwa minajili ya kupata faida haraka na wafanyabiashara kutokuwa na subra.

Mbolea zingine pamoja na dawa, zinaelekeza wazi kuwa chakula hicho kitumike siku 14 baada ya spray. Lakini wakulima pasipokujali afya za walaji, ndani ya siku mbili tu anauza.

Maana yake jamii inajikuta inatumia vyakula vyenye concentration kubwa sana ya mbolea na dawa za mimea. Yaani kwa lugha nyepesi jamii inalishwa SUMU.

Ulaji huo wa sumu unaathiri afya za walaji ikiwa pamoja na afya ya uzazi. Ndiyo kusema huko nguvu za kupeleka moto.

Wasichofahamu tu ni kuwa mboga nyingi zinazoliwa Dar zinalimwa katika green houses, ambapo ndipo kuna matumizi makubwa ya mbolea na dawa. Unabagua chinese, unabugia mchicha, nk. Ukijidai zipo salama, thubutu!.

Hivyo, chinese haina shida. Bali walimaji wa Chinese ndiyo wenye shida.
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha madai kuwa mboga ya Chinese inapunguza nguvu za kiume. Madai haya yanatokana na hadithi za watu na imani potofu, na hayategemei utafiti wowote uliothibitishwa.

Utafiti unaopatikana unaonyesha kuwa mboga ya Chinese inaweza kuwa na faida kadhaa kwa afya ya wanaume. Kwa mfano, baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mboga ya Chinese inaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo, kupunguza hatari ya saratani, na kuimarisha mfumo wa kinga.
 
Hivi ndiyo vitu napenda kuona kitu kinatolewa ufafanuzi unaoeleweka mi huwa nashangaa mtu anakimbilia tu kupunguza nguvu za kiume ukimuuliza kivipi kimya. Bravo
 
Hivyo, chinese haina shida. Bali walimaji wa Chinese ndiyo wenye shida.

Hapa unamaanisha nini..?
 
saivi bila mbolea na makemikali mengine makali sana bado haujazalisha mboga yoyote.
Kama unajipenda ACHANA NA MBOGAMBOGA ZOTE sio Chinese tu.
 
Hivyo, chinese haina shida. Bali walimaji wa Chinese ndiyo wenye shida.

Hapa unamaanisha nini..?
Umesoma comment yangu kwa uangalifu?

Huwa sirudiagi kutoa maelezo ambayo nilishayatoa. Ila acha nikupendelee.

Maana yangu ni kuwa endapo chinese italimwa kwa njia sahihi zinazopaswa bila kutumia madawa makali na mbolea nyingi kuikuza ili ikuwe kwa haraka, basi chinese ni mboga nzuri sana tu kiafya.

Wakulima ndiyo wenye shida. Kwa kuwa wanaichochea mboga husika kukua kwa haraka.
 
Ni mboga nzuri.Na kama unaipenda hakikisha imeoshwa vizuri,ipikwe ilainike na utafune vizuri kabla ya kuuruhusu iende tumboni.Naishia hapa.
 
Asante kwa upendeleo wako mkuu.
 
MBOGA ZA MAJANI ZINARUTHUBISHA KATIKA MWILI WA MWANADAMU, HAZINA MARADHA IKIWA HAZINA DAWA
 
Ndio mana nasema fasting ni muhimu sana kuondoa sumu mwilini,,, sio Chinese tu vyakula vyingi tu plus hayo madawa yanayowekwa yana sumu balaa,,we ushangai wazee wetu waliishi mrefu ila sisi kutoboa ngumu mara kukosa nguvu za kiume,mara ma presha,sukari,, etc
 
Ukitaka umuweze mwanaume wa kibongo mwambie kitu fulani kinaongeza/kinapunguza nguvu za kiume 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…