SI KWELI Mboga za majani aina ya Chainizi husababisha upungufu wa Nguvu za kiume

SI KWELI Mboga za majani aina ya Chainizi husababisha upungufu wa Nguvu za kiume

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na Madai ya kwamba matumizi ya mboga za majani aina ya chainizi yamekua na madhara katika ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume. Kuna ukweli gani katika hilo suala?

maxresdefault.jpg

Naomba nijibiwe kitaalam niweze kuelewa.
 
Tunachokijua
Chainizi hupatikana kwenye familia kubwa ya mboga za majani inayofahamika kwa jina la Brassica. Mfano wa mboga zingine zilizopo kwenye familia hii ni Kabichi (Cabbage) na Brokoli (Broccoli).

Asili ya Mboga hii ni nchi ya China ilikoanza kutumika Zaidi ya miaka 1500 iliyopita.

Bara la Amerika ya Kaskazini limeanza kulima mboga hii kwa zaidi ya miaka 100. Taarifa nyingi za kiuchunguzi na tafiti zinaonesha kuwa mboga hii kwa sasa imesambaa sehemu nyingi duniani, Tanzania ikiwemo.

Viambato na Kemikali zake
Kwa mujibu wa USDA, Mboga hii huwa na nishati, maji, protini, wanga, nyuzilishe, madini chuma, calcium, magnesium, phosphorus, selenium, potassium, sodium, zinc, copper na manganese.

Ni chanzo kizuri cha folate, vitamini C, viondoa sumu vya beta carotene pamoja na vitamin E.

Faida zake kiafya
Mjumuisho wa virutubisho vinavyopatikana kwenye Chainizi huwa na faida kubwa kwa afya ya binadamu. Kwa ujumla wake, mboga hii hufanya mambo yafuatayo-
  • Kutoa kinga dhidi ya aina mbalimbali za Saratani hasa ile ya utumbo mpana
  • Huzuia uvimbe (Inflammation)
  • Hupunguza nafasi ya kuugua magonjwa ya mfumo wa damu na moyo
  • Huimarisha afya ya mifupa
  • Huboresha afya ya macho
  • Huongeza uwezo wa kinga za mwili katika kupambana na magonjwa
  • Ni nzuri kwa afya mama mjamzito katika kuongeza damu na kumkinga mtoto asipatwe na changamoto za kimaumbile, hasa tatizo la kuzaliwa na mgongo wazi
Uhusiano wake na kupunguza nguvu za kiume
JamiiForums imefuatilia hoja hii kwa kuzungumza na wataalamu wa lishe na kugundua kuwa haina ukweli.

Chainizi haina kemikali sumu zinazoathiri ufanisi wa mwanamme kwenye kushiriki tendo la ndoa, pia hakuna tafiti za kiafya zinazoelezea madhara haya kwa binadamu.

Kwa kuwa msingi wa hoja za kisayansi hasa upande wa tiba huboreshwa, kupingwa na kuthibitishwa kwa tafiti, madai yanayohusisha mboga hii na upungufu wa nguvu za kiume hayabaki kuwa uzushi.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Marekani (NHI), upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na uwepo wa magonjwa sugu mwilini Pamoja na changamoto zingine zinazohusisha saikolijia, mfumo wa kati wa fahamu, homoni za mwili, mtindo wa Maisha Pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa.
Ndio mana nasema fasting ni muhimu sana kuondoa sumu mwilini,,, sio Chinese tu vyakula vyingi tu plus hayo madawa yanayowekwa yana sumu balaa,,we ushangai wazee wetu waliishi mrefu ila sisi kutoboa ngumu mara kukosa nguvu za kiume,mara ma presha,sukari,, etc
Nani alikudanga kuwa mwili wa binadamu una sumu? Umekuwa nyoka? Hii ni nadharia ya kibongo-bongo. Utasikia mtu anasema mboga au tunda fulani eti linaondoa sumu mwilini. Hii ni njia ya layman kuelezea mambo ya afya.
 
Ndio mana nasema fasting ni muhimu sana kuondoa sumu mwilini,,, sio Chinese tu vyakula vyingi tu plus hayo madawa yanayowekwa yana sumu balaa,,we ushangai wazee wetu waliishi mrefu ila sisi kutoboa ngumu mara kukosa nguvu za kiume,mara ma presha,sukari,, etc
Fasting inaondoaje SUMU mwilini???
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Ukijuwa ni kwanini iliitwa au kupewa jina hilo na chimbuko la hiyo mboga hauta tamani kuitumia tena.📌🔨
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Ninakushauri kama unataka kuishi kwa furaha kwa hapa Dar es Salaam usile mboga ya majani iitwayo chainizi, miaka ya zamani mboga hii iliishi shambani kwa furaha na raha kiasi ikajijengea sifa, lakini miaka ilivyokwenda akatokea mdudu aitwae nzimweupe, mdudu huyu hudhoofisha shina kwa haraka sana.

Mboga inapendwa na inakua kwa haraka sana sasa nini cha kufanya, mkulima wa hii mboga ikamlazimu ainyunyuzie dawa kuwaua hao wadudu, hivyo inanyunyuziwa dawa leo na leo inavunwa na leo mlaji anaila bila kujua kuwa imenyunyuziwa dawa labda tu kama una pua nzuri utaisikia harufu ya hiyo dawa ambayo itakudhuru wewe taratibu, kweli umasikini aghari.
 
saivi bila mbolea na makemikali mengine makali sana bado haujazalisha mboga yoyote.
Kama unajipenda ACHANA NA MBOGAMBOGA ZOTE sio Chinese tu.
Si kweli..
Samadi inatosha..
At home garden
 
Hivyo, chinese haina shida. Bali walimaji wa Chinese ndiyo wenye shida.

Hapa unamaanisha nini..?
Mboga nyingi za dar zinalimwa kwenye mabonde yenye mtiririko wa maji toka viwandani or mto msimbazi uliojaa kila aina ya taka, sehemu utakayokua na uhakika ni kwa mtu anaelima mboga kwa kuchimba visima na hii ni nje ya mji km ni katikati Basi mnakula mboga zenye mavi yenu wenyewe.
Ndio maana watu wengi hawapendi mboga mboga za majani za mjini
 
Mimi napiga na nachanganya na kitimoto
 
Walizituhumu kuwa zinapunguza nguvu za kiume. Tokea hapo ikawa ni mtihani kwa baadhi ya watu kuzila. Ila si kweli.
 
Mi binafsi sizipendi tu hata utie karanga hiyo mboga nilipishana nayo bila kujua sababu.
Mboga inajiongeza maji yenyewe kwenye bakuli ya nini hiyo?
 
Siyapendi hayo majani aisee! Sidhani kama yanatatizo kiafya though!
Tembele, mchicha, majani ya maboga, kunde, maharage, mnafu, kisamvu na figiri hizo ndio mboga nizipendazo! Zipikwe kiasili saafi😋😋😋
Mnafu si mzuri kwa wazee gout
 
Mboga nyingi za dar zinalimwa kwenye mabonde yenye mtiririko wa maji toka viwandani or mto msimbazi uliojaa kila aina ya taka, sehemu utakayokua na uhakika ni kwa mtu anaelima mboga kwa kuchimba visima na hii ni nje ya mji km ni katikati Basi mnakula mboga zenye mavi yenu wenyewe.
Ndio maana watu wengi hawapendi mboga mboga za majani za mjini
Basi mnakula mboga zenye mavi yenu wenyewe
Daaah aiseer
 
Ujinga na umasikini ni bado ni janja la taifa.
 
Kama huna nguvu huna tu, mie chainizi naitafuna vizuri, nipate ugali, chainizi na kuku, samaki au nyama ya kukaanga, nakula mpaka nahemea juu juu, nikipata na juice baridi, hapo janabi namuona kama mganga wa kienyeji 🤣😂😂
 
Waliotakiwa kujibu hili sio USAID kwanza wao ndo wanaleta adi Michele wenye virutubisho, mamlaka ya afya na TBS ndio wajibu hili
Siku hizi nafaka toka viwandani hapa Tanzania zina virutubisho, sijui kama unavijua hivyo virutubisho.
 
Back
Top Bottom