SI KWELI Mboga za majani aina ya Chainizi husababisha upungufu wa Nguvu za kiume

SI KWELI Mboga za majani aina ya Chainizi husababisha upungufu wa Nguvu za kiume

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na Madai ya kwamba matumizi ya mboga za majani aina ya chainizi yamekua na madhara katika ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume. Kuna ukweli gani katika hilo suala?

maxresdefault.jpg

Naomba nijibiwe kitaalam niweze kuelewa.
 
Tunachokijua
Chainizi hupatikana kwenye familia kubwa ya mboga za majani inayofahamika kwa jina la Brassica. Mfano wa mboga zingine zilizopo kwenye familia hii ni Kabichi (Cabbage) na Brokoli (Broccoli).

Asili ya Mboga hii ni nchi ya China ilikoanza kutumika Zaidi ya miaka 1500 iliyopita.

Bara la Amerika ya Kaskazini limeanza kulima mboga hii kwa zaidi ya miaka 100. Taarifa nyingi za kiuchunguzi na tafiti zinaonesha kuwa mboga hii kwa sasa imesambaa sehemu nyingi duniani, Tanzania ikiwemo.

Viambato na Kemikali zake
Kwa mujibu wa USDA, Mboga hii huwa na nishati, maji, protini, wanga, nyuzilishe, madini chuma, calcium, magnesium, phosphorus, selenium, potassium, sodium, zinc, copper na manganese.

Ni chanzo kizuri cha folate, vitamini C, viondoa sumu vya beta carotene pamoja na vitamin E.

Faida zake kiafya
Mjumuisho wa virutubisho vinavyopatikana kwenye Chainizi huwa na faida kubwa kwa afya ya binadamu. Kwa ujumla wake, mboga hii hufanya mambo yafuatayo-
  • Kutoa kinga dhidi ya aina mbalimbali za Saratani hasa ile ya utumbo mpana
  • Huzuia uvimbe (Inflammation)
  • Hupunguza nafasi ya kuugua magonjwa ya mfumo wa damu na moyo
  • Huimarisha afya ya mifupa
  • Huboresha afya ya macho
  • Huongeza uwezo wa kinga za mwili katika kupambana na magonjwa
  • Ni nzuri kwa afya mama mjamzito katika kuongeza damu na kumkinga mtoto asipatwe na changamoto za kimaumbile, hasa tatizo la kuzaliwa na mgongo wazi
Uhusiano wake na kupunguza nguvu za kiume
JamiiForums imefuatilia hoja hii kwa kuzungumza na wataalamu wa lishe na kugundua kuwa haina ukweli.

Chainizi haina kemikali sumu zinazoathiri ufanisi wa mwanamme kwenye kushiriki tendo la ndoa, pia hakuna tafiti za kiafya zinazoelezea madhara haya kwa binadamu.

Kwa kuwa msingi wa hoja za kisayansi hasa upande wa tiba huboreshwa, kupingwa na kuthibitishwa kwa tafiti, madai yanayohusisha mboga hii na upungufu wa nguvu za kiume hayabaki kuwa uzushi.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Marekani (NHI), upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na uwepo wa magonjwa sugu mwilini Pamoja na changamoto zingine zinazohusisha saikolijia, mfumo wa kati wa fahamu, homoni za mwili, mtindo wa Maisha Pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa.
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Nilitoa tangazo nyumbani kwangu kitambo sana... Sitaki kabisa kuona mboga ya chinese ikinunuliwa...
 
Siyapendi hayo majani aisee! Sidhani kama yanatatizo kiafya though!
Tembele, mchicha, majani ya maboga, kunde, maharage, mnafu, kisamvu na figiri hizo ndio mboga nizipendazo! Zipikwe kiasili saafi😋😋😋
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Inauwa nguvu za kibaba 😂
 
Hivi ndiyo vitu napenda kuona kitu kinatolewa ufafanuzi unaoeleweka mi huwa nashangaa mtu anakimbilia tu kupunguza nguvu za kiume ukimuuliza kivipi kimya. Bravo
Kiloka Morogoro Hizo Mboga Tele
 
Aisee hii ni kweli!!?
Za dar nyingi ukiona sehemu wanapozilima utaghairi kula,,dar mboga za majani lima kwako kama huwez pata wale wanaolima kwao na unajua maji wanayotumia kumwagilia,,,,,,,,ila hizi za mtaani unakuta kuna bonde fulani lina maji machafu mengine hata kuna kemikali za ajabu viwanda vinamwagia kwenye hizo sehem ndo yanatumika hayo maji kumwagilia hizo mboga
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Sio mboga hiyo ni chakula Cha mifugo kama nguruwe Haina tofauti na kabeji aka kaya maskini
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Mimi pia naipenda Sana....Je Kwa upande Wa wanawake Ina madhara yoyote pia?
 
Ndio mana nasema fasting ni muhimu sana kuondoa sumu mwilini,,, sio Chinese tu vyakula vyingi tu plus hayo madawa yanayowekwa yana sumu balaa,,we ushangai wazee wetu waliishi mrefu ila sisi kutoboa ngumu mara kukosa nguvu za kiume,mara ma presha,sukari,, etc
Vyakula vina sehemu yake, ila kikubwa waliishi muda mrefu kwa ajili ya kufanya kazi
 
Nime notice kitu kutoka huko uraiani ni zaidi ya mara kumi nimeona wanaume wakiikataa mboga ya majani ya chainizi migahawani na hata mahotelini..

Watu kibao utasikia aaa chainizi toa situmiagi kabisa wakati Mimi nazitandikaga tu. Sasa wazee kwani zina shida gani hizi?

Usikute najimaliza bila kujua maana mimi huwa nazifakamiaga balaa
Kaka iyo ni fake news mm nimekula iyo mboga miaka 20 Sasa na kwakweli sioni shida yoyote ni Imani za watu tuu Tena Wala chips ila si chainiz
 
Naichapa kwelikweli tena ichanganywe kwenye nyama.Nabondaa.
 
Ni ushamba. Mtu anakataa kula chinese huku anabugia mayai ya kisasa, unabugia energy, unabugia broiler.

Anyway, turudi kwenye uzi.

Sababu haswa ni kuwa wameaminishana kuwa chinese inamaliza nguvu za kiume. Wakose nguvu wasingizie mboga.

Je, ni kweli Chinese inamaliza nguvu za kiume? Jibu ni ndiyo na hapana.

Nitaanza kwa sababu gani ni HAPANA.
Mboga za majani aina ya Chinese pamoja kuwa na madini ya chuma, calcium na magnessium, pia ina vitamin A, K1, C na Folate.

Kwa taarifa tu ni kuwa, madini na vitamini hizo tajwa, zinasaidia sana kwa afya ya moyo, na utengenezaji wa chembe nyekundu za damu. Kwa swala la nguvu za kiume, moyo na damu ndizo hufanya kazi kubwa sana katika kufanikisha tendo husika kufanyika kwa viwango.

Sasa ya nini tuilaumu Chinese?
Ni ujuha.

Turudi sasa kwenye swala la NDIYO inasababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Chinese kama ilivyo mboga zingine, zinakuzwa haraka kwa kutumia madawa pamoja na mbolea nyingi.

Hii hufanywa na wakulima kwa minajili ya kupata faida haraka na wafanyabiashara kutokuwa na subra.

Mbolea zingine pamoja na dawa, zinaelekeza wazi kuwa chakula hicho kitumike siku 14 baada ya spray. Lakini wakulima pasipokujali afya za walaji, ndani ya siku mbili tu anauza.

Maana yake jamii inajikuta inatumia vyakula vyenye concentration kubwa sana ya mbolea na dawa za mimea. Yaani kwa lugha nyepesi jamii inalishwa SUMU.

Ulaji huo wa sumu unaathiri afya za walaji ikiwa pamoja na afya ya uzazi. Ndiyo kusema huko nguvu za kupeleka moto.

Wasichofahamu tu ni kuwa mboga nyingi zinazoliwa Dar zinalimwa katika green houses, ambapo ndipo kuna matumizi makubwa ya mbolea na dawa. Unabagua chinese, unabugia mchicha, nk. Ukijidai zipo salama, thubutu!.

Hivyo, chinese haina shida. Bali walimaji wa Chinese ndiyo wenye shida.
Nimeipenda hii
 
saivi bila mbolea na makemikali mengine makali sana bado haujazalisha mboga yoyote.
Kama unajipenda ACHANA NA MBOGAMBOGA ZOTE sio Chinese tu.
Kuna watu wengi tu wanalimia kwa kutumia mbolea ya samadi na hawatumii chemicals. Siku za nyuma nilikuwa na na bustani ya mboga mbali mbali na nilikuwa situmii dawa zozote.
 
Back
Top Bottom