Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

Mboga zangu 5 simple nizipendazo kulia chakula (hasa ugali) na Jinsi ninavyoziandaa

Hongera sana kwa juhudi., napenda kupika pia ila sio nikiwa nimechoka.,

Nikichoka nipikiwe tu tutakula kilichopo tulale.,hata km ni supu ya kunde😅
ukiwa na njaa huwa huchagui chakula eeh? 😂
 
Tuna enda pamoja kila seem kasoro kwenye mtind situmii kabisa

Pia kwenye iyo masala sijuh situmii naweka karanga za kusaga

Mimi parachichi ndio na weza kula na Gari sio mtindi
kwann hutumii mtindi mkuu,una shida na afya yako?
 
Ahshante. Mkuu japo shemejio ilibidi aingilia kati kwa simu. Nimeelekezwa kama hapa ulipoeleza. Nimefanikisha.
Nimetumia Karoti,Kitunguu,royco mchuzi mix .
Japo sipendi tambi.. kuna wakulungwa nimewarekebishia. Hope hawatapenda😀😀
Nishajishibia nyama za morombo jioni hii..
View attachment 1591536
Tambi ziko wapi mkuu?
 
Mkuu siku jaribu kupika majani ya maboga kwa carrots za kusaga,kitunguu,pilipili,curry powder,nazi ya azam na peanut butter kwa mbali....alaf pembeni pika rosti lako la maini na ugali......thank me later[emoji41]
Hii recipe nimeichukua[emoji1]
 
Asante nilisahau jina ila mchuzi natumia curry powder ile ina unjano njano flani hv ni nzuri.
Nenda maduka ya wahindi kanunue ile binzari halisi kabisa ya India na pilipili ya unga. Binzari ikaange baada tu ya vitunguu kabla ya nyanya...nogesha zaidi
 
Ni mazoea mabaya sana kupenda kula mayai kwa wingi na mara kwa mara!

Ni kwa bahati mbaya sana kwenye jamii ama hawana ufahamu juu ya maswala ya lishe salama au wengine wanafahamu athari ya kula mayai mengi mara kwa mara lakini wanapuuza miiko!
Ingekuwa vyema ungeleta madhara ya kila mayai kwa wingi tuyajue.
 
zamani hizo niko chini ya himaya ya wazazi hamna chakula nilikua sipendi kula kama ndizi,mpk naondoka nyumbani kila mtu anajua sipendi ndizi,lakini sasa hivi sijui ni maisha sijui nini ila nilijaribu jifunza pikaa ndizi tangu hapo hadi leo ndizi ni one of my favourite food.

hasa zikiwa za nazi na zaidi nizipike mwenyewe,nilimpkia mama angu 1st day ananitembelea kwangu tangu nitoke home alifurahi na hakuamini alihisi ni ndoto. Ndizi tamu sana na ndio mana ni moja ya vyakula gharama ktk kuvipika ili vitoke vitamu.
ndizi sizipendi hasa zisipokuwa zile zenye kiladha cha sukari...wanaita mzuzu!

Ila kwa upenzi wa ndizi mbivu mi ni zaidi ya gorrila
 
Nenda maduka ya wahindi kanunue ile binzari halisi kabisa ya India na pilipili ya unga. Binzari ikaange baada tu ya vitunguu kabla ya nyanya...nogesha zaidi
naenda nawambiaje na hayo maduka yako wapi?
 
Back
Top Bottom