Ashasembeko
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 226
- 914
Leo Watanzania tumeamka na uteuzi wa Mawaziri Dr. Phillip Mpango katika Wizara ya Fedha na Prof. Palamagamba Kabudi katika Wizara ya Mambo ya Nje. Maswali mengi yameibuka kuhusu huu uteuzi.
Kwanza huu uteuzi umekiuka utaratibu wa kikatiba. Ibara 51(1) ya Katiba yetu ta Tanzania inasema Waziri Mkuu kabla hajaanza kazi lazima ale kiapo mbele ya Rais. Pia ibara ya 55 inamtaka Rais kushauriana na Waziri Mkuu kabla hajaunda Baraza la Mawaziri.
Kwa mantiki hii JPM kavunja katiba maana Waziri Mkuu bado hajaapishwa Ikulu na kafanya uteuzi bila kumshirikisha. Na hata kama alimshirikisha, bado kavunja utaratibu maana Waziri Mkuu bado hajala kiapo.
Tuyaache hayo. Twende kwenye mada. Kwanini JPM kawateua Mpango na Kabudi haraka kuliko Mawaziri wengine?
Juzi niliandika uzi kuhusu jinsi diplomasia yetu itakua na changamoto kubwa katika kipindi hiki cha miaka mitano. - Hii itakuwa awamu ngumu ya kidiplomasia
Uteuzi huu unaonyesha dhahiri kuwa Magufuli anatambua kutakua na changamoto. Mpango anahitajika kuomba misaada na Kabudi kuwaconvice wahisani kuwa uchaguzi huu ulikua wa halali.
Nguvu kubwa itatumika sana kuwashawishi hawa watu na ukiangalia huku nje wapinzani, wameanaza campaign ya kulobby jumuiya ya kimataifa kutoitambua serikali hii. Tundu Lissu yupo Belgium sa hizi anatafuta nyayo ya kuhutubia Umoja wa Ulaya na kuongea na baadhi ya wanasenate na congress Marekani kuwaelezea kuhusu uchafuzi wa October. Tusubiri tuone.