Mbona hamkuniambia kuwa HISA ni mchezo wa kubet?

Kabla ya kununua hisa, lazima uelewe kuwa bei za stock huwa zinabadilika, na inawezekana kabisa ukapoteza mtaji/uwekezaji wako wote.
Jambo la pili, nini lengo lako la kuwekeza? Je ulifanya utafiti juu ya kampuni ambayo umewekeza? Unajua mapato ya kampuni hiyo, unajua madeni yake? unajua hali yake ya kibiashara?
Kabla ya kuwekeza kwanza pata taarifa maalumu.

Jambo la mwisho ambalo ni msingi sana; usiwekeze kwenye Hisa kwa sababu ya hadithi na kutaka kuwa tajiri.
 
Mkuu,kabla hujawekeza kwenye hisa unatakiwa kujua kabisa hisa kama ulivyo uwekezaji wowote ni kubet,kuna kupata au kukosa. Hiyo ipo kidunia. Lakini unaweza kupunguza uwezekano wa kupoteza pesa zako kwa kufanya uchunguzi sahihi wa kampuni kabla ya kuamua kununua hisa zake au lah . Pia unatakiwa kuwa na mtazamo wa muda mrefu, hisa zinaweza kushuka mwaka huu,mwakani zikapanda. Usipaniki zikishuka ghafla labda kama unaona hii kampuni kabisa inaenda kufa kufa.
Mimi binafsi nashukuru sijawahi kupoteza pesa zangu tangu nianze kuwekeza hapo DSE, kampuni zangu zote nilizowekeza zimenipa faida.
Ushauri wangu,tafuta elimu sahihi ya kuchambua kampuni kabla ya kununua hisa zake,elimu imejaa kwenye mitandao ya kijamii ,ni wewe tu.
Ila hisa ni uwekezaji mzuri,natamani ningejifunza kuwekeza mapema zaidi.
Kweli kabisa. Hisa aikupi faida muda mdogo wanaowekeza muda mfupi ndo wanabet ila muda mrefu inalipa kuanzia miaka 2-7.
 
Kabla ya kununua hisa, lazima uelewe kuwa bei za stock huwa zinabadilika, na inawezekana kabisa ukapoteza mtaji/uwekezaji wako wote.
Jambo la pili, nini lengo lako la kuwekeza? Je ulifanya utafiti juu ya kampuni ambayo umewekeza? Unajua mapato ya kampuni hiyo, unajua madeni yake? unajua hali yake ya kibiashara?
Kabla ya kuwekeza kwanza pata taarifa maalumu.

Jambo la mwisho ambalo ni msingi sana; usiwekeze kwenye Hisa kwa sababu ya hadithi na kutaka kuwa tajiri.
Hapo kutaka kua tajir
Ndio umenikata
 
Mkuu,kabla hujawekeza kwenye hisa unatakiwa kujua kabisa hisa kama ulivyo uwekezaji wowote ni kubet,kuna kupata au kukosa. Hiyo ipo kidunia. Lakini unaweza kupunguza uwezekano wa kupoteza pesa zako kwa kufanya uchunguzi sahihi wa kampuni kabla ya kuamua kununua hisa zake au lah . Pia unatakiwa kuwa na mtazamo wa muda mrefu, hisa zinaweza kushuka mwaka huu,mwakani zikapanda. Usipaniki zikishuka ghafla labda kama unaona hii kampuni kabisa inaenda kufa kufa.
Mimi binafsi nashukuru sijawahi kupoteza pesa zangu tangu nianze kuwekeza hapo DSE, kampuni zangu zote nilizowekeza zimenipa faida.
Ushauri wangu,tafuta elimu sahihi ya kuchambua kampuni kabla ya kununua hisa zake,elimu imejaa kwenye mitandao ya kijamii ,ni wewe tu.
Ila hisa ni uwekezaji mzuri,natamani ningejifunza kuwekeza mapema zaidi.
Umetoa ufafanuzi mzuri!
 
Back
Top Bottom