DOKEZO Mbona hii V8 ya Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho inatumika kwa shughuli binafsi ikiwemo kubeba mkaa na cement

DOKEZO Mbona hii V8 ya Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho inatumika kwa shughuli binafsi ikiwemo kubeba mkaa na cement

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
6a69c3d61d157.jpg


Kwa zaidi ya mwaka mzima sasa gari ambayo inatakiwa kutumiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kwa ajili ya shughuli za kiofisi badala yake imekuwa ikitumika kwa shughuli binafsi nyingi ikiwemo za masuala ya shamba.

Gari hilo lenye namba za usajili SU 42509 aina ya Land Cruiser V8 mali ya Bodi ya Korosho limekabidhiwa kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya matumizi ya bodi hasa kumbeba kiongozi anayehusika, lakini limeonekana mara kadhaa likibeba hadi mkaa kutoka shamba au ndiyo matumizi yenyewe ya gari hilo!

Mtu wa karibu wa Bodi hiyo ameniambia kuwa gharama zote za uendeshaji wa V8 hiyo zinabebwa na CBT, pia hata dereva anayeliendesha katika mizunguko yote hiyo iwe ya ofisi na nje ya ofisi naye gharama zake zinabebwa na bodi husika.

Gari hilo limekuwa linakuja huku kwetu shambani katika Kijiji cha Chienjele Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kufanya shughuli mbalimbali za masuala ya kilimo, mbali na hapo kuna magari mengine ya CBT nayo yamekuwa yakifika huku yakiwa yamebeba cement kutoka Mtwara hadi shambani Ruangwa.

Kuna wakati pia magari ya CBT hubeba mkaa kutoka shambani kwa Mwenyekiti kwa ajili ya kwenda kuuzwa mjini, kuchukua korosho kutoka shambani kupeleka Dar es Salaam.
 
Learn to mind your business. Watu wengine mnapenda kujitafutia matatizo bila sababu za msingi.
 
Umeamua kuja kunitangaza humu kwa wanoko wenzio c ndio?

View attachment 3640020
Sijui kwa nini ukimiliki kiriba tumbo cha namna hii, bila ya kujali umri, ukienda hospitali kupimwa ni lazima upatikane na tatizo la kiafya, hasa haya magonjwa yasiyo ya kuambukiza?

Sasa hivi nikimuona mtu katanguliza kitambi naanza kumuonea huruma!
 
Mwenyekiti mwenyewe anashinda bar kuanzia asubuhi hadi jioni
 
Sasa mkuu hilo Jengo linahusika vipi na hoja yako, wewe ungetuonesha hilo gari tuone hali yake kwa sasa.

All in all, hiyo inaitwa "Kula kwa urefu wa kamba"
 
Back
Top Bottom