Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mikoa kama hii kupoa kunachangiwa sana na serikali, ukiangalia majengo hayo ya miaka 1950 kurudi nyuma utajua kabisa huo mji ulikuwa na mishe za kutosha kwa wakati huo. Fikiria miaka hiyo hiyo miji mingine ilikuwaje kama sio mapori na vijiji vidogovidogo.

Tunasingizia umwinyi, sijui elimu akhera au uchawi lakini hii si kweli, unafikiri ingekuwaje miji hiyo ingeendelea kupewa kipaumbele kwa miundombinu na uwekezaji? Kwani Dar ilijengwa na watu tu au serikali ilianza kuijenga? Unafikiri Dar es Salaam na Bagamoyo ni mji upi ilianza kuchangamka? Leo hii hali ikoje?

Nitolee mfano mji ninaoufahamu Kigoma: Kipindi cha German East Africa ulikuwa ni mji mkubwa sana kwasababu Wajerumani waliwekeza station kubwa ya train (lilikuwa jengo kubwa kuliko station yoyote ya train Tanganyika) kwasababu waliutegemea mji huo kama kiungo na Congo, Burundi na Zambia na walikuwa na meli kubwa sana hapo S.S. Liemba, unafikiri kwa wakati huo kati ya Kigoma na Mwanza upi ulikuwa mji mkubwa? Sababu ni nini? Uwekezaji wa Mjerumani ulifanya mji uchangamke na watu walitoka sehemu mbalimbali kuja kujipatia riziki hapo.

Leo hii bandari ya Kigoma imedorola baada ya kutokupewa umuhimu na serikali, bandari inategemea reli na barabara kufikisha mizigo kutoka Dar port kwenda Zambia, Burundi na Congo. Lakini hadi leo hii barabara ya kuiunganisha Kigoma haijakamilika na reli inasuasua sana sababu haina ubora na cha ajabu zaidi reli hiyo ya kati inayojengwa sasa ya SGR ikapewa kipaumbele ya Dar - Mwanza tofauti na Dar - Kigoma! Hapo bado unatarajia mji ukue kwa juhudi za wananchi?!

Miji ya Congo kama Kalemie, Bukavu na Uvira wanategemea sana Tanzania kwa kila kitu kama chakula, mafuta, hardware n.k. Kama Kigoma ingekuwa na miundombinu mizuri kungekuwa na Viwanda vya kutosha kuilisha East Congo na mji ungetoa ajira za kutosha, bandari ingechangamka lakini kinyume chake hata umeme tu Kigoma wanatumia umeme wa generator! Alafu tunawalaumu waswahili wa ujiji na waarabu!

Hii kauli ya miji ya waswahili, mbona hatuisikii kwa Dar ya Wazaramo? Si waswahili wale? lakini mji wao kila mtu anataka kuwekeza huko. Hatakama wakazi wa mji husika ni waswahili lakini kukiwa na vyanzo vya michakato watakuja wageni kuwekeza na mji utachangamka.
 
Nadhani pia Lindi inaongoza kwa ulozi na uchawi kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana. Hiyo factor ina athari hasi kwa mkoa.


YESU NI KRISTO
Suala wakati mwingine sio uchawi huu wa kawaida. Wengi wenye historia ya Tanganyika wanasema yapo matambiko makubwa yalifanyika ili kuwafanya watawala waendelee kutawala. Makubwa yalifanyika Bagamoyo na Lindi. Huko walifunga anga na kupafanya watu wasivutiwe napo.Kwa mandhari zilizopo hayo maeneo kulitakiwa kuwe kama ulaya. Changamoto sio hata serikali ipeleke mradi mbona bwndari ilitakiwa kujengwa Bagamoyo je iliondokaje ondokaje? Maana kuna vitu vinaanzia kwenye ulimwengu wa roho. Kumbukeni Elisha alifika kwenye mji mmoja watu wakamwambia mji huu ni mzuri lakini maji yake huzaa mapooza na wala vitu havizaliwi huku. Aliuponya mji na ardhi yake haikuzaa mapooza. Kuna sehemu anga zake zimefungwa. Mpaka atakayeoneshwa ufunguo na Mungu ili afungue ndipo utaona maendeleo hiyo sehemu.
 
Hebu pitia hapo JM kwa Jasmine, ukapate bia moja nakuja kulipa!!
 
Mbona Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, Katavi hali ni hiyohiyo? Maji ya ndoo na Tv za Chogo mjini
 
Lindi mbona haijapakana na Dar mkuu
 
Niambie I Bei za viwanja huko ,hayo ndio maeneo Huwa napenda kushika ardhi yaani Lindi,Kigoma,Rukwa na Katavi..
Mimi mwenyewe sikupata fursa ya kuulizia kiwanja ila nilipapenda sana ki mandhari na wala sikuona uchawi wa aina yoyote.
 
Ka
Lindi iko mwambao wa pwani (Factor kubwa kwa ukuaji wa miji/mji)
Lindi ina beach nzuri (biashara, utalii, uvuvii)
Lindi ina makumbusho ya majengo ya kale nayo pia utalii wa kihistoria
Bado ina ardhi na vinginevyo

View attachment 2307018
Kama unaelekea kikwetu (airport) kuna kijiji kinapakana na mto,nikipat heka kwa one million ntashukuru,kama kuna possibility hito DM pls.
 
Kwa uwekezaji ule uliokuwa unafanyika Chato unaamini Baada ya muda ingeikaribia japo Mwanza hata Kama fursa nyingine hakuna mfano Viwanda.?
 
Ekari moja inasomaje ? Nije nibebe kama ekari 300 za korosho na mitiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…