Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mikoa kama hii kupoa kunachangiwa sana na serikali, ukiangalia majengo hayo ya miaka 1950 kurudi nyuma utajua kabisa huo mji ulikuwa na mishe za kutosha kwa wakati huo. Fikiria miaka hiyo hiyo miji mingine ilikuwaje kama sio mapori na vijiji vidogovidogo.

Tunasingizia umwinyi, sijui elimu akhera au uchawi lakini hii si kweli, unafikiri ingekuwaje miji hiyo ingeendelea kupewa kipaumbele kwa miundombinu na uwekezaji? Kwani Dar ilijengwa na watu tu au serikali ilianza kuijenga? Unafikiri Dar es Salaam na Bagamoyo ni mji upi ilianza kuchangamka? Leo hii hali ikoje?

Nitolee mfano mji ninaoufahamu Kigoma: Kipindi cha German East Africa ulikuwa ni mji mkubwa sana kwasababu Wajerumani waliwekeza station kubwa ya train (lilikuwa jengo kubwa kuliko station yoyote ya train Tanganyika) kwasababu waliutegemea mji huo kama kiungo na Congo, Burundi na Zambia na walikuwa na meli kubwa sana hapo S.S. Liemba, unafikiri kwa wakati huo kati ya Kigoma na Mwanza upi ulikuwa mji mkubwa? Sababu ni nini? Uwekezaji wa Mjerumani ulifanya mji uchangamke na watu walitoka sehemu mbalimbali kuja kujipatia riziki hapo.

Leo hii bandari ya Kigoma imedorola baada ya kutokupewa umuhimu na serikali, bandari inategemea reli na barabara kufikisha mizigo kutoka Dar port kwenda Zambia, Burundi na Congo. Lakini hadi leo hii barabara ya kuiunganisha Kigoma haijakamilika na reli inasuasua sana sababu haina ubora na cha ajabu zaidi reli hiyo ya kati inayojengwa sasa ya SGR ikapewa kipaumbele ya Dar - Mwanza tofauti na Dar - Kigoma! Hapo bado unatarajia mji ukue kwa juhudi za wananchi?!

Miji ya Congo kama Kalemie, Bukavu na Uvira wanategemea sana Tanzania kwa kila kitu kama chakula, mafuta, hardware n.k. Kama Kigoma ingekuwa na miundombinu mizuri kungekuwa na Viwanda vya kutosha kuilisha East Congo na mji ungetoa ajira za kutosha, bandari ingechangamka lakini kinyume chake hata umeme tu Kigoma wanatumia umeme wa generator! Alafu tunawalaumu waswahili wa ujiji na waarabu!

Hii kauli ya miji ya waswahili, mbona hatuisikii kwa Dar ya Wazaramo? Si waswahili wale? lakini mji wao kila mtu anataka kuwekeza huko. Hatakama wakazi wa mji husika ni waswahili lakini kukiwa na vyanzo vya michakato watakuja wageni kuwekeza na mji utachangamka.
 
Fursa gani unayo zaidi ya kumponda Jiwe kwa shekeli ya buku 7 toka Lumumba
Unaona wabishi tuko huku
Hapa ndiyo camp
Alafu tukija mjini tukiwa viti virefu
Tunapata mambo yetu anakuja mtu
Anataka kutupangia matumizi

Ova
IMG-20220719-WA0016.jpg
IMG-20220719-WA0021.jpg
 
Nadhani pia Lindi inaongoza kwa ulozi na uchawi kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana. Hiyo factor ina athari hasi kwa mkoa.

YESU NI KRISTO
Suala wakati mwingine sio uchawi huu wa kawaida. Wengi wenye historia ya Tanganyika wanasema yapo matambiko makubwa yalifanyika ili kuwafanya watawala waendelee kutawala. Makubwa yalifanyika Bagamoyo na Lindi. Huko walifunga anga na kupafanya watu wasivutiwe napo.Kwa mandhari zilizopo hayo maeneo kulitakiwa kuwe kama ulaya. Changamoto sio hata serikali ipeleke mradi mbona bwndari ilitakiwa kujengwa Bagamoyo je iliondokaje ondokaje? Maana kuna vitu vinaanzia kwenye ulimwengu wa roho. Kumbukeni Elisha alifika kwenye mji mmoja watu wakamwambia mji huu ni mzuri lakini maji yake huzaa mapooza na wala vitu havizaliwi huku. Aliuponya mji na ardhi yake haikuzaa mapooza. Kuna sehemu anga zake zimefungwa. Mpaka atakayeoneshwa ufunguo na Mungu ili afungue ndipo utaona maendeleo hiyo sehemu.
 
Shoo inaanza karibia 70% ya mkoa ni mapori.. mji umejaa umwinyi sana na kurogana.. kiufupi wakazi hasa lindi mjini ni watu wa ndumba sana.

Hili hupelekea vijana wengi kuukimbia huu mkoa na kwenda DSM kusaka maisha na hawarudi kuwekeza kwao.

Asilimia kubwa ya watu walindi sio wasomi yaani hawana elimu dunia bali elimu akhera hili nalo tatizo.

Licha ya kuwa na ardhi nzuri na rasilimali nyingi bado miundombinu hususani barabara hazifiki maeneo mengi hasa vijijini.. maji safi tatizo umeme nao tatizo.

Wajanja wanapata hela sana Lindi kwa maana ya mazao kama ufuta, korosho, mbaazi n.k.

Karibu sana Lindi Ruangwa.

#MaendeleoHayanaChama
Hebu pitia hapo JM kwa Jasmine, ukapate bia moja nakuja kulipa!!
 
Mikoa nane uliyotembea ni michache sana kwako kuijadili lindi
Nimetembea Tanzania yote kila mkoa , ni wilaya baadhi tu sijafika na nyimgi ni hizi mpya ,
Lindi pamedorora , na maisha yake kama mtwara tu ni ghali ! Nimelala Guest house ya 25000 lindi , kitanda ni 4x6 na hakina neti maji ni ya kuchota na ndoo, tv ya chogo., hii sionmiaka ya 90, ni juzi tu hapa zimepita siku 9 tu
Mbona Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Mtwara, Katavi hali ni hiyohiyo? Maji ya ndoo na Tv za Chogo mjini
 
Sumbawanga wao wamejukita sana katika kilimo mkuu ndio shughuli yao kubwa ya kiuchumi mkuu......

Pia ukilinganisha na iringa kama unavosema kumbuka iringa katika wilaya ya mufindi mji wa mafinga wao ndio wanaongoza kwa production ya mbao Tanzanian nzima unaambiwa 75% ya mbao if I'm not mistaken yatoka kwao....huwezi compare na Lindi ambayo pia ndio ina bahari as you claim kuwa inaweza kuwa chanzo cha mapato kama beach au Wenda hata kama bandari...lakini kumbuka kama anavyodai huyo mkuu aliyetangulia kuwa Lindi yazungukwa na Dar ea salaam na Mtwara Miji ambayo ina beaches nzuri na bandari nzuri kubwa luliko hata huko Lindi.....

Even if wakijenga bandari huko ngumu sana kuwa kubwa kama ya mtwara au Lindi

Issue ya morogoro kuwa mbona opo katikati ya Dar es salaam na Dodoma lakini inakuwa hali ya kuwa haipigiwi promotion Mimi nakataa....
Kuna miradi mingapi mikubwa ipo morogoro hali yakuwa Lindi haipo???

SGR imepita hadi Lindi pia????
Lindi mbona haijapakana na Dar mkuu
 
Ka
Lindi iko mwambao wa pwani (Factor kubwa kwa ukuaji wa miji/mji)
Lindi ina beach nzuri (biashara, utalii, uvuvii)
Lindi ina makumbusho ya majengo ya kale nayo pia utalii wa kihistoria
Bado ina ardhi na vinginevyo

View attachment 2307018
Kama unaelekea kikwetu (airport) kuna kijiji kinapakana na mto,nikipat heka kwa one million ntashukuru,kama kuna possibility hito DM pls.
 
Mikoa kama hii kupoa kunachangiwa sana na serikali, ukiangalia majengo hayo ya miaka 1950 kurudi nyuma utajua kabisa huo mji ulikuwa na mishe za kutosha kwa wakati huo. Fikiria miaka hiyo hiyo miji mingine ilikuwaje kama sio mapori na vijiji vidogovidogo.

Tunasingizia umwinyi, sijui elimu akhera au uchawi lakini hii si kweli, unafikiri ingekuwaje miji hiyo ingeendelea kupewa kipaumbele kwa miundombinu na uwekezaji? Kwani Dar ilijengwa na watu tu au serikali ilianza kuijenga? Unafikiri Dar es Salaam na Bagamoyo ni mji upi ilianza kuchangamka? Leo hii hali ikoje?

Nitolee mfano mji ninaoufahamu Kigoma: Kipindi cha German East Africa ulikuwa ni mji mkubwa sana kwasababu Wajerumani waliwekeza station kubwa ya train (lilikuwa jengo kubwa kuliko station yoyote ya train Tanganyika) kwasababu waliutegemea mji huo kama kiungo na Congo, Burundi na Zambia na walikuwa na meli kubwa sana hapo S.S. Liemba, unafikiri kwa wakati huo kati ya Kigoma na Mwanza upi ulikuwa mji mkubwa? Sababu ni nini? Uwekezaji wa Mjerumani ulifanya mji uchangamke na watu walitoka sehemu mbalimbali kuja kujipatia riziki hapo.

Leo hii bandari ya Kigoma imedorola baada ya kutokupewa umuhimu na serikali, bandari inategemea reli na barabara kufikisha mizigo kutoka Dar port kwenda Zambia, Burundi na Congo. Lakini hadi leo hii barabara ya kuiunganisha Kigoma haijakamilika na reli inasuasua sana sababu haina ubora na cha ajabu zaidi reli hiyo ya kati inayojengwa sasa ya SGR ikapewa kipaumbele ya Dar - Mwanza tofauti na Dar - Kigoma! Hapo bado unatarajia mji ukue kwa juhudi za wananchi?!

Miji ya Congo kama Kalemie, Bukavu na Uvira wanategemea sana Tanzania kwa kila kitu kama chakula, mafuta, hardware n.k. Kama Kigoma ingekuwa na miundombinu mizuri kungekuwa na Viwanda vya kutosha kuilisha East Congo na mji ungetoa ajira za kutosha, bandari ingechangamka lakini kinyume chake hata umeme tu Kigoma wanatumia umeme wa generator! Alafu tunawalaumu waswahili wa ujiji na waarabu!

Hii kauli ya miji ya waswahili, mbona hatuisikii kwa Dar ya Wazaramo? Si waswahili wale? lakini mji wao kila mtu anataka kuwekeza huko. Hatakama wakazi wa mji husika ni waswahili lakini kukiwa na vyanzo vya michakato watakuja wageni kuwekeza na mji utachangamka.
Kwa uwekezaji ule uliokuwa unafanyika Chato unaamini Baada ya muda ingeikaribia japo Mwanza hata Kama fursa nyingine hakuna mfano Viwanda.?
 
Shoo inaanza karibia 70% ya mkoa ni mapori.. mji umejaa umwinyi sana na kurogana.. kiufupi wakazi hasa lindi mjini ni watu wa ndumba sana.

Hili hupelekea vijana wengi kuukimbia huu mkoa na kwenda DSM kusaka maisha na hawarudi kuwekeza kwao.

Asilimia kubwa ya watu walindi sio wasomi yaani hawana elimu dunia bali elimu akhera hili nalo tatizo.

Licha ya kuwa na ardhi nzuri na rasilimali nyingi bado miundombinu hususani barabara hazifiki maeneo mengi hasa vijijini.. maji safi tatizo umeme nao tatizo.

Wajanja wanapata hela sana Lindi kwa maana ya mazao kama ufuta, korosho, mbaazi n.k.

Karibu sana Lindi Ruangwa.

#MaendeleoHayanaChama
Ekari moja inasomaje ? Nije nibebe kama ekari 300 za korosho na mitiki
 
Back
Top Bottom