Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Siyo kweli. VETA ipo mwanzo mwanzo huku unaingia Lindi ukitokea Mchinga. Ipo karibu na airport. Mnazi mmoja Mingoyo iko kama 20km kutoka mjini kuelekea Mtwara.
Ooooh ahsante kwa kunisahihisha.
 
NBS inautaja mkoa wa Ruvuma kuwa top ten katika mikoa tajiri nchini..


Sijui wanatumiaga vigezo gan wale

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkoa hauna hata kitu cha maana, yaan khaaah.
Labda utajiri wa Ardhi na kilimo. Mweeeeh
 
Jipe moyo..ebu tujulishe ile gesi ya mtwara ambayo tuliambia mtwara itakuwa jiji kubwa afrika mashariki kutokana na gesi kiko wapi sasa.

Ukuaji wa seheme unachangizwa na mengi sana..sikatai ujenzi wa hivyo vyuo unaweza kuwa chachu..ila kuhusu gesi ambayo bomba litapita kuelekea dsm sahau kuhusu maendeleo ya lindi..kamaana tayari uzoefu tunao tangu ile ya mtwara inapigiwa upatu.

Kuhusu kumiliki ardhi lindi ni jambo jema kwa manufaa ya badae pia mana ardhi ni mali.

#MaendeleoHayanaChama
Acha ujuaji. Usijifanye unaijua sana lindi kuliko wazoefu waliopo hapo wanaelewa kitu gani kinaendelea. Nani kakuambia mradi wa LNG bomba linaenda dar.
 
Nawasoma tu wadau humu wanalopoka tu lopoka tu

Wanaiponda lindi ....lindi kuna mradi mkubwa sahv wa uchimbaji wa magnesium na kuna mradi mkubwa mkubwa wa uchimbaji wa graphite

Na sahv lindi kuna mahali wanachimba watu dhahabu na purity yKe iko vzr kuliko hata ya kutoka kanda ziwa....

Fursa zipo San na sahv huko kuna mchanganyiko wa watu wanaenda

Wavaa tai,wakaa mjini hawawezi elewa

Ova



Kwa mtafutaji lindi fursa zipo
Watu wanakaririshana hapa. Watu tumeenda lindi na tunapiga hela wao wanapiga makelele tu hapa. Tembeeni muone acheni kulishana matango pori hapa.
 
Serikali ndo chanzo hamna promo hamna miradi mikubwa


Ngoja uje kuona miaka 10 ijayo dodoma itakavyokuwa
 
Kama hayo mambo yapo basi ni hapo Lindi mjini acha kujumuisha vijana wote wa Lindi,vijana huku wilayani tunajituma sana tunalima kwa wingi mazao ya biashara;ufuta,mbaazi,mihogo na korosho..kiufupi hatupo kama mnavyotuchukulia,Lindi ndio mkoa unaoongoza katika hii nchi kwa kuingiza pato kubwa litokanalo na mapato ya zao la ufuta.#Shikahiyo!
Hivi unajua kuna wasukuma,wamakonde wengi sana wanalima ufuta huko lindi?

#MaendeleoHayanaChama
 
... Halafu wanakuja kupiga kelele baadaye walitengwa! Anyway, Lindi imetoa watu maarufu nchi hii; Simba wa Vita, First Lady, current PM. Kama naona Ruangwa itajitenga kuwa mkoa unaojitegemea maana hadi timu wana timu yao ligi kuu.
Ruangwa, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Liwale wakiunda mkoa wao watapiga hatua sana..
 
Watanzania sisi ni washamba sana na malimbukeni na tusiojielewa; hivi tz hii ukiacha Dar kuna wapi kwingine kulikoendelea kiasi cha mtu kukesha akiponda sehemu nyingine?!!!!!!

Hivi makelele haya ninayoyaona ni ya watu kutoka sehemu hizi hizi za tz nilizotembelea na mimi au zingine?!!!!

Mikoa nane (8) ya nchi hii niliyowahi kufika na kuishi inanifanya nicheke sana baadhi ya commentsi humu.......
Watu sijui wanapata wapi nguvu ya kuponda mikoa mingine. Hali ni mbaya sana. Na kila sehemu kuna fursa inategemea unafanya nini. Hapo hapo lindi kuna watu wanapiga hela kiasi kwamba wakikuta unaongea vibaya kuhusu Lindi wanakushangaa.
 
Acha ujuaji. Usijifanye unaijua sana lindi kuliko wazoefu waliopo hapo wanaelewa kitu gani kinaendelea. Nani kakuambia mradi wa LNG bomba linaenda dar.
Kaa utulie uone kama hiyo gesi itawanufaisha watu wa lindi..mtakua mnaona mabomba yanaelekea dsm tu..mkipendelewa sana mtaona meli tu zinatia nanga kubeba gesi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ruangwa, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Liwale wakiunda mkoa wao watapiga hatua sana..
Liwale ipo kushoto sana..ila nilisikia hicho kitu kuanzisha mkoa wa masasi ila sidhani kama itawezekana kwa sasa kwasababu ya population ya huko kusini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom