Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Siyo kweli. VETA ipo mwanzo mwanzo huku unaingia Lindi ukitokea Mchinga. Ipo karibu na airport. Mnazi mmoja Mingoyo iko kama 20km kutoka mjini kuelekea Mtwara.
Ooooh ahsante kwa kunisahihisha.
 
NBS inautaja mkoa wa Ruvuma kuwa top ten katika mikoa tajiri nchini..


Sijui wanatumiaga vigezo gan wale

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkoa hauna hata kitu cha maana, yaan khaaah.
Labda utajiri wa Ardhi na kilimo. Mweeeeh
 
Acha ujuaji. Usijifanye unaijua sana lindi kuliko wazoefu waliopo hapo wanaelewa kitu gani kinaendelea. Nani kakuambia mradi wa LNG bomba linaenda dar.
 
Watu wanakaririshana hapa. Watu tumeenda lindi na tunapiga hela wao wanapiga makelele tu hapa. Tembeeni muone acheni kulishana matango pori hapa.
 
Serikali ndo chanzo hamna promo hamna miradi mikubwa


Ngoja uje kuona miaka 10 ijayo dodoma itakavyokuwa
 
Hivi unajua kuna wasukuma,wamakonde wengi sana wanalima ufuta huko lindi?

#MaendeleoHayanaChama
 
... Halafu wanakuja kupiga kelele baadaye walitengwa! Anyway, Lindi imetoa watu maarufu nchi hii; Simba wa Vita, First Lady, current PM. Kama naona Ruangwa itajitenga kuwa mkoa unaojitegemea maana hadi timu wana timu yao ligi kuu.
Ruangwa, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Liwale wakiunda mkoa wao watapiga hatua sana..
 
Watu sijui wanapata wapi nguvu ya kuponda mikoa mingine. Hali ni mbaya sana. Na kila sehemu kuna fursa inategemea unafanya nini. Hapo hapo lindi kuna watu wanapiga hela kiasi kwamba wakikuta unaongea vibaya kuhusu Lindi wanakushangaa.
 
Acha ujuaji. Usijifanye unaijua sana lindi kuliko wazoefu waliopo hapo wanaelewa kitu gani kinaendelea. Nani kakuambia mradi wa LNG bomba linaenda dar.
Kaa utulie uone kama hiyo gesi itawanufaisha watu wa lindi..mtakua mnaona mabomba yanaelekea dsm tu..mkipendelewa sana mtaona meli tu zinatia nanga kubeba gesi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ruangwa, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Liwale wakiunda mkoa wao watapiga hatua sana..
Liwale ipo kushoto sana..ila nilisikia hicho kitu kuanzisha mkoa wa masasi ila sidhani kama itawezekana kwa sasa kwasababu ya population ya huko kusini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…