Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

View attachment 2306268
View attachment 2306269
mkuView attachment 2306270
View attachment 2306271
Mkuu ukiongelea Location mi nakataa
kwasababu:
-lindi iko mwambao wa pwani (Factor kubwa kwa ukuaji wa miji/mji)
-Lindi ina beach nzuri (biashara,utalii,uvuvii)
-Lindi ina makumbusho ya majengo ya kale nayo pia utalii wa kihistoria
-bado ina ardhi na vinginevyo

Huwezi fananisha na mji kama iringa au sumbawanga ambayo ni landlocked
Mh, sasa kumbuka kuwa Pwani ni sababu ya kizamani ya mji kukua, biashara siku hizi iko bara kuliko Pwani, Iringa kumbuka ndio njia kuu ya biashara kwenda Congo na Zambia, pia ni njia panda ya kwenda Mbeya, Morogoro na Dodoma, Lindi sasa yenyewe iko Pwani ndio, ila ukitoka hapo Lindi unaenda wapi tena kwenye mzunguko wa biashara.

Halafu pwani ishatwaliwa na miji kama Dar, kidogo na Tanga na Mtwara inakujakuja siku hizi, kumbuka Mtwara sio tu wana bandari kubwa pia wana njia kuu ya kwenda Songea na Mbeya na Malawi hivyo Mtwara ni kituo kikubwa cha biashara kuliko Lindi.

Hapo kwasababu za kushindani Lindi inapoteza taji kwa Mtwara
 
Location ya Morogoro inabeba mji, miundo mbinu karibia yote muhimu ya kitaifa imepita mji huo, kuanzia ya gridi ya taifa, barabara kuu, reli zote mbili, ni njia panda, location ina favor mji wa morogoro
Umesahau kitu kimoja: Moro kuna vyuo vikuu vinne, vya umma viwili na vya binafsi viwili vinachangia kwa kiasi kikubwa katika swala zima la Income na kuchangamsha Mji.
 
Kuna miji ina location nzuri inayofanya miji hiyo ikue bila kutumia nguvu, miji kama Morogoro, yani yenyewe naturally tu inakuwa mikubwa hata kama hakuna uwekezaji wa makusudi. Lindi ishu kubwa ni location ilipo, idadi ndogo ya wakazi hayo mambo yana fanya wawekezaji wasishawishike sana kwenda
Inshu sio location..hivi unaijua Ifakara iliko..lakini mbona inapiga hatua.

Kama kuna biashara watu watafika tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Shoo inaanza karibia 70% ya mkoa ni mapori..mji umejaa umwinyi sana na kurogana..kiufupi wakazi hasa lindi mjini ni watu wa ndumba sana.
Hili hupelekea vijana wengi kuukimbia huu mkoa na kwenda dsm kusaka maisha na hawarudi kuwekeza kwao.

Asilimia kubwa ya watu walindi sio wasomi yani hawana elimu dunia bali elimu akhera hili nalo tatizo.

Licha ya kuwa na ardhi nzuri na rasilmali nyingi bado miundombinu hususani barabara hazifiki maeneo mengi hasa vijijini..maji safi tatizo umeme nao tatizo.

Wajanja wanapata hela sana lindi kwa maana ya mazao kama ufuta,korosho,mbaazi n.k.

Karibu sana lindi ruangwa.

#MaendeleoHayanaChama
Lindi katika swala la Wizard sidhani kama kuna mkoa unafua dafu hata Sumbawanga haioni ndani. MZ wakati wa uhai wake alichezeshewa picha moja kali sana.
 
Soko la lindi!!..
Ina maana yale masoko ya kisasa yanayojengwa kila mkoa huku hamna

IMG_4118.jpg

IMG_4117.jpg
 
Location ya Morogoro inabeba mji, miundo mbinu karibia yote muhimu ya kitaifa imepita mji huo, kuanzia ya gridi ya taifa, barabara kuu, reli zote mbili, ni njia panda, location ina favor mji wa morogoro
... plus higher learning institutions - SUA, MU, etc. they bring new people every year, new ideas, thinking, life styles, etc. Sasa mamwinyi wa Lindi culture zao tu tayari ni tatizo!
 
Back
Top Bottom