Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Mbona Lindi iko unpopular sana? Shida ni promotion au wakazi?

Lindi kunawaislam wengi sana ndio maana
Uislam upo pwani yote mkuu. Hata kusini kuwa na wakristo wachache usishangae hawa jamaa walimpinga mzungu Kwa kishindo (maji maji 1905/7). Hii ndio ishara kubwa kabisa ya kuliona hili
 
Wakati wa vuguvugu la gesi ile miaka ya 2011/2012, nilikuwa masomoni chuo kikuu fulani hivi na nilikuwa nimetoka kazini huko kusini wakati wananchi wameshaanza kuhamasishana na ile kauli yao 'haitoki'!

Kule kusini, hoja ilikuwa shughuli zifanyiwe kule ili wenyewe nao wafaidike kwani walijiona ni watu wanaotengwa mno na serikali linapokuja suala la maendeleo.......na hiyo ndo ilikuwa hoja yao kubwa.
Ajabu ni kuwa kule chuoni, kwa wasomi wanaotegemewa kuwa na habari za kiuchunguzi, yaani huwezi kuamini, walikuwa wanawazodoa watu wa kusini kuwa ni wabinafsi na kwamba 'hawawezi tu kuwafikia watu wa kaskazini hata wafanye nini'. Binafsi nikajionea ni namna gani hali ilivyo ya hatari........yaani hao ndo wasomi wa elimu ya juu, vp wanakijiji kule chini?!!!!!
 
Kwa uwekezaji ule uliokuwa unafanyika Chato unaamini Baada ya muda ingeikaribia japo Mwanza hata Kama fursa nyingine hakuna mfano Viwanda.?
Mfano mzuri sana, inawezekana isingeizidi Mwanza lakini ingefika mbali sana. Medical Department Store(MSD) ya mkoa imewekwa Chato, hospitali kubwa ya rufaa, chuo cha VETA, uwanja wa ndege, maandalizi ya bandari ya nchi kavu baada ya SGR kufika mwanza, njia ya kwenda hifadhi ya Burigi kupitia Geita mjini ilifungwa na kutakiwa kutumika ya Chato tu na mengine mengi.

Hizo ni sababu tosha za kuufungua mji na kutokana na hilo watu walikuwa wameanza kukimbilia viwanja huko vya makazi na biashara (wakiwemo jamaa zangu wa karibu) na viwanda vilianza kufunguliwa, kuna mwekezaji mmoja ameenda kung'oa structure ya kiwanda chake baada ya kuona upepo kubadilika.

Watu wa Chato hawatomsahau hayati Magufuli kamwe kwani mwanga walianza kuuona.
 
Ikipewa kipaumbele kila kitu kitakaa sawa. Ahsante sana

Wanaogopa kuongezeka na kuujaza mkoa wao?

Safi sana, wasiache mila na tamaduni zao,huku wakiangalia ni jinsi gani watautoa kidedea mkoa wao
Nalog off Z
Ndugu Washawasha
nimefurahishwa sana na ufafanuzi wako.
qRI8Gs7.gif
 
Karibuni mtazame kazi nzuri ya sanaa kutoka FILAMU PICTURES, msubscribe na kutoa maoni yenu juu ya kazi hii

 
Nisiwacheke sana Lindi, maana mwenyewe kwetu hali ni hiyo hiyo japo kuna nafuu kidg. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Tena bora lindi watajivunia Bahari na bandari,. Sisi Ruvuma ni vumbi tyuuh. Sisi ndo tulikosea nn Dunia, sio kwa mkoa wetu khaaah.
Ruvuma kupo vzur wewe fursa nying za kilimo

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Nianze tuu kwa kusema nimeishi Lindi zaidi ya miaka minne mlandege street, kwa makunguru, mitwelo,na mnazi mmoja

Shida ya mkoa huu kwanza wengi wa wakaazi ni wazawa na ukiona mji wenye wazawa pekee maendeleo hapo utayatafuta kwa tochi

Angalia kata ndogo kabisa ya Ndanda ina income kuliko Lindi mjini kwa sababu za wamisionari waliopo pale nenda nyangao Ruangwa nk mwamko ni mkubwa wa maendeleo
Kikubwa wananchi wa Lindi wakubali kuwaachia watu maeneo haswa ya vivutio kutoka nje ya Lindi naamini maendeleo yataonekana

Nawakilisha
 
Haijapewa kipaumbele...
Huu ndio ukweli wenyewe.
Viongozi wa juu huwa wanachagua kanda za kuziendeleza kimaendeleo miaka yote na bado hawajamaliza malengo yao.
Hii inapelekea mikoa iliyo nyuma kimaendeleo kuendelea kusahsulika hadi leo.
 
Shida ni elimu. Hizi zimambo nyingine za Imani z inaletwa na tamaduni ya watu wa kule kushindwa kukubaliana na maisha ya kisasa(more resistant to modernity)
Hii ina ukweli kwa asilimia 50.
Modernity wakati mwingine huletwa na wageni wa kutoka sehemu nyingine.
Kwa mfano ikianzishwa miradi mikubwa ya kiserikali kama viwanda,vyuo vikuu,Mabenki kuna wafanyakazi au wanachuo wa kutoka maeneo mbalimbali watakuja wataongeza idadi ya wakazi wa eneo hilo na culture ya wazawa itaanza kubadilika polepole na ndipo modernity itapatikana automatically.
Ni ngumu kupatikana modern lifestyle kama hiyo location wanaishi watu wa jamii moja tu.
 
Ruvuma si bora niwe kwenye handaki tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji38][emoji38]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila Ruvuma acha kabisaa yaan, tushapazoea na tunapapenda wenyewe.
 
Back
Top Bottom