Mikoa kama hii kupoa kunachangiwa sana na serikali, ukiangalia majengo hayo ya miaka 1950 kurudi nyuma utajua kabisa huo mji ulikuwa na mishe za kutosha kwa wakati huo. Fikiria miaka hiyo hiyo miji mingine ilikuwaje kama sio mapori na vijiji vidogovidogo.
Tunasingizia umwinyi, sijui elimu akhera au uchawi lakini hii si kweli, unafikiri ingekuwaje miji hiyo ingeendelea kupewa kipaumbele kwa miundombinu na uwekezaji? Kwani Dar ilijengwa na watu tu au serikali ilianza kuijenga? Unafikiri Dar es Salaam na Bagamoyo ni mji upi ilianza kuchangamka? Leo hii hali ikoje?
Nitolee mfano mji ninaoufahamu Kigoma: Kipindi cha German East Africa ulikuwa ni mji mkubwa sana kwasababu Wajerumani waliwekeza station kubwa ya train (lilikuwa jengo kubwa kuliko station yoyote ya train Tanganyika) kwasababu waliutegemea mji huo kama kiungo na Congo, Burundi na Zambia na walikuwa na meli kubwa sana hapo S.S. Liemba, unafikiri kwa wakati huo kati ya Kigoma na Mwanza upi ulikuwa mji mkubwa? Sababu ni nini? Uwekezaji wa Mjerumani ulifanya mji uchangamke na watu walitoka sehemu mbalimbali kuja kujipatia riziki hapo.
Leo hii bandari ya Kigoma imedorola baada ya kutokupewa umuhimu na serikali, bandari inategemea reli na barabara kufikisha mizigo kutoka Dar port kwenda Zambia, Burundi na Congo. Lakini hadi leo hii barabara ya kuiunganisha Kigoma haijakamilika na reli inasuasua sana sababu haina ubora na cha ajabu zaidi reli hiyo ya kati inayojengwa sasa ya SGR ikapewa kipaumbele ya Dar - Mwanza tofauti na Dar - Kigoma! Hapo bado unatarajia mji ukue kwa juhudi za wananchi?!
Miji ya Congo kama Kalemie, Bukavu na Uvira wanategemea sana Tanzania kwa kila kitu kama chakula, mafuta, hardware n.k. Kama Kigoma ingekuwa na miundombinu mizuri kungekuwa na Viwanda vya kutosha kuilisha East Congo na mji ungetoa ajira za kutosha, bandari ingechangamka lakini kinyume chake hata umeme tu Kigoma wanatumia umeme wa generator! Alafu tunawalaumu waswahili wa ujiji na waarabu!
Hii kauli ya miji ya waswahili, mbona hatuisikii kwa Dar ya Wazaramo? Si waswahili wale? lakini mji wao kila mtu anataka kuwekeza huko. Hatakama wakazi wa mji husika ni waswahili lakini kukiwa na vyanzo vya michakato watakuja wageni kuwekeza na mji utachangamka.