Mbona nchi nyingine za Afrika haziruhusu mimba shuleni, na hakuna lawama za mataifa ya nje?

Mbona nchi nyingine za Afrika haziruhusu mimba shuleni, na hakuna lawama za mataifa ya nje?

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,649
Nimeipata hii picha ktk mjadala wa baadhi ya nchi za Africa wakishangaa hawa wadada wanafunzi pichani. (Nimeambatanisha picha)

Wachangiaji wengi walionesha kushangaa hao wadada, kusoma huku wakiwa wajawazito.

Katika mjadala wengi wao walisema "It's only South Africa" Japo kuna nchi kama Kenya wameruhusu.

Nikajisemea kumbe kuna nchi Africa hawajaruhusu wajawazito kwenda shule. Nchi kama Ethiopia.

Hawa uwa wanamisimamo haswa. Linapokuja swala la utamaduni, mila, desturi na imani hawayumbishwi.

Najiuliza tu baba wa mtoto miaka 30. Mtoto anazaliwa na kukua bila baba.

View attachment 2113277

FB_IMG_1644355410227.jpg
 
Na atueleze anaposema 'Ulaya' ana maanisha nchi gani hasa? kwani tafsiri ya sheria ya mtoto kwetu na kwao zinaingiliana? kuna mataifa 16yrs fresh tu!
Hatujaongelea umri wa mtoto. Hapa ni swala la mwanafunzi kusoma na mimba. Si umri wa kuanza mapenzi. Sheria bado inaruhusu kwa Tanzania miaka 15 kuolewa kwa idhini ya wazazi au mahakama
 
Mkuu, si kila kitu cha mzungu ni chakufuata. Jiongeze
Inaonesha uelewi naongea nini. Wazungu ndo wametushinikiza tufuate sera zao kuwa watoto wenye mimba waende shule. Ndo maana nikasema Ethiopia uwa hawashinikizwi. Wamegomea mambo mengi ya wazungu.
 
Ukifanya refference na hapa kwetu issue ya umri haikwepeki mzee! Tafakari kwa mawanda mapana!
Hatuongelei umri. Sheria ya elimu inasema ukimpa mimba mwanafunzi ni miaka 30 jela haijataja umri wa mwanafunzi. Hata akiwa na miaka 19 halafu mwanafunzi wa sekondari ni jela. So hapa siongelei umri. Ni mimba na kusoma. Soma uelewe mada.
 
Inaonesha uelewi naongea nini. Wazungu ndo wametushinikiza tufuate sera zao kuwa watoto wenye mimba waende shule. Ndo maana nikasema Ethiopia uwa hawashinikizwi. Wamegomea mambo mengi ya wazungu.
Sasa hilo nalo mpaka mzungu akuambie au ushurutishwe. Mimba ni sehemu ya maisha ya mtoto wa kike (mwanamke). Akiipata bado mdogo asihukumiwe kwa kukoseshwa elimu. Akanywe kwa busara na hekima huku tukijua analo jukumu la kulea hicho kiumbe
 
Kwa context yako Ukifanya refference na hapa kwetu issue ya umri haikwepeki mzee! Tafakari kwa mawanda mapana!
Nadhani hujui mada inaongelea nini. Kwa Tanzania ni kosa kufanya ngono na mwanafunzi. Haijataja umri ukifuata sheria ya elimu. Lakini sheria ya makosa ya jinai ni kosa kufanya mapenzi na mtoto chini ya miaka 18. Lakini hiyo hiyo sheria inaruhusu kuoa binti wa miaka 15.
 
Sasa hilo nalo mpaka mzungu akuambie au ushurutishwe. Mimba ni sehemu ya maisha ya mtoto wa kike (mwanamke). Akiipata bado mdogo asihukumiwe kwa kukoseshwa elimu. Akanywe kwa busara na hekima huku tukijua analo jukumu la kulea hicho kiumbe
Sasa mbona mmesubiri mpaka mzungu ndo kawambia muwaruhusu wasome kama sivyo hakuna msaada.
 
Nadhani hujui mada inaongelea nini. Kwa Tanzania ni kosa kufanya ngono na mwanafunzi. Haijataja umri ukifuata sheria ya elimu. Lakini sheria ya makosa ya jinai ni kosa kufanya mapenzi na mtoto chini ya miaka 18. Lakini hiyo hiyo sheria inaruhusu kuoa binti wa miaka 15.
Ngoja ni withdraw all my statements, nimekuelewa ..kwenye mda yako husika hujagusia kabisa hayo..weka 'nyama' kaka!
 
Hujazaa wewe..na kama umezaa hauna mtoto wa kike..hakuna mzazi atakayefurahia kuona mtoto wake haendelei masomo kisa mimba.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom