Mbona pesa imekuwa ngumu sana, Mbona kila mtu analalamika, Kwani shida iko wapi?

Mbona pesa imekuwa ngumu sana, Mbona kila mtu analalamika, Kwani shida iko wapi?

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Hakuna salamu

Moja kwa moja kwenye mada, Kwani nyie wenzetu mnapata wapi pesa, mbona biashara zimekuwa ngumu sana, yaani kweli hadi kijana wa chuo kikuu yupo field kwenye taasisi moja hv eti anakwambia, Braza toa elfu 30 ya faster niipileke document yako kwa incharge akupitishie faster.

Mbona kama kila mtu amekuwa dalali, mbona kama wazee wa kumanipulate mifumo wamerudi kwa kasi sana, mbona kama kuna daraja kubwa sana kati ya wenye pesa na ambao hawana.

Mwisho; Mbona pale kariakoo sasahv watoto wanaolala nnje wamezidi sana ? Dah roho imeniuma sana yaani naamdika hii post huku nawaza sana mpaka nataka kukata tamaa.

Anyway ngoja tusubirie labda mambo yatabalidika.

Kidumu chama cha mapinduzi!

Nawasilisha

NB; Basi hapo mtu anaweza akasoma uzi wote huku akitafakari kwa makini sana ila alipoona tu nimeandika "Kidumu chama cha mapinduzi" anafikiria kudondosha bonge la tusi kwenye comment.
 
Mwenye buku anikopeshe .....

au kama una elfu 10 nipe nitakurudishia buku yako.
 
Hakuna salamu

Moja kwa moja kwenye mada, Kwani nyie wenzetu mnapata wapi pesa, mbona biashara zimekuwa ngumu sana, yaani kweli hadi kijana wa chuo kikuu yupo field kwenye...
Leo nimekaa sehemu na jamaa tunapanga mipango ya kugombea urais wa Tanzania, nasikia kwenye siasa kuna pesa za kumwaga.
 
Hao wanao lalamika ni CHADEMA bila shaka ambao wao kila kitu kipinga na kulalamika, kila kukicha watu wanafungua hardware kuonyesha watu wanazo pesa za kujengea watu kila siku wananunua mandinga mapya inshort hao wanaolalamika ni njia ya kukunyima wewe coz wakisema wanacho utawaomba, kwahy sema huna pesa sio watu hawana pesa.
 
Kiuhalisia suala la hela kuwa ngumu sio siku hizi tu, tangu zamani watu wanasema "siku hizi hela imekuwa ngumu". Tumekuwa na majukumu sasa, tukaze humo humo!
 
"July- September TRA imeweka rekodi ya mapato"
Mbona wazabuni na wakandarasi hawalipwi?
Watu wanauziwa assets zao kisa serikali hailipi!
Hali kitaa ni tete,bado utaskia ushabiki uchwara,"anaupiga"...nonsense!
 
Back
Top Bottom