Mbona Serikali haisemi ukweli kuhusu suala la umeme?

Mbona Serikali haisemi ukweli kuhusu suala la umeme?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Wananchi wanateseka hasa akina Mama machinga kama wauza barafu, saluni, vinywaji baridi nk.

Tuliaminishwa kuwa tatizo la umeme litapungua sana katika muda wa wiki mbili lakini haya yamekuwa ni maneno tu huku wananchi wakiteseka sana.

Umeme unakatika saa moja asubuhi na unarudi saa moja usiku hapa kuna biashara gani itafanyika. Tunawaona wakubwa wanavyokula raha.

Misafara ya magari ndo usiseme. Sasa hii ni nchi gani ambapo kila kukicha wananchi wanapata taabu.
 
IMG-20231019-WA0002.jpg
 
Noma sana kwahio umeme gani huo unaopatikana adi tunapongezwa
 
Noma sana kwahio umeme gani huo unaopatikana adi tunapongezwa
Ukweli usemwe tu, tumezoea kulalamika sana
Ndo kawaida ya wabongo,
Aliefanikiwa upande wa umeme ni wakoloni pamoja na magufuli pekee
Hii ccm tunayomiaka nenda rudi na siku ya kuchagua wa kuangalia maisha ya watanzania watamchagua tena na tena kisha tuanze kulalamika ktkt ya safari
Acheni unafiki na kulalamika na wivu wa kishamba
Unakuta jitu limesoma mpaka chuo kikuu eti nalo linakwambia kuwachagua wanasiasa unamchagulia kwenda kula bora liendelee na maisha yake
Haya kuleni maisha na giza acheni kulalamika
Tafadhari ili bandko sio majibu yako mtoa post bali kwa wanafiki wote wanaojitambua na wanaojidai wanajua kumbe awajui
 
Wananchi tumepiga kelele kwa kukosa nishati ya umeme kwa shughuli za kiuchumi lakini tumedanganywa sana na uongozi wa Serikali ya Tanzania kuwa tatizo la umeme ni suala la muda tu.

Mpaka sasa wananchi bado tunateseka hivyo natoa kauli kwa wote kuwa tuiondoe CCM madarakani kupitia kura zetu.

Tumechoka.
 
CCM hawezi badilisha chcht zaidi yakuzidi kuharibu n miaka 60 ss ya uhuru lkn bd Kila ktu kipo kvyake vyakee tu km wtt yatima walioachwa bila wazazii .
 
CCM haiwezi kuanguka Kwa njia ya Kura, hata kama umeme unakatika Kwa miezi 12 mfululizo bado CCM watashinda Kwa kishindo tena asubuhi SAA 4..... Kwa katiba hii ya kilofa ni Nani anaweza kuiangusha CCM
 
Kwani tumepata Uhuru mwaka 2022 mpaka umeme uwe sababu ya kuingusha CCM?! Bado sa 8 usiku usingizi umenoga.
 
Wananchi tumepiga kelele kwa kukosa nishati ya umeme kwa shughuli za kiuchumi lakini tumedanganywa sana na uongozi wa Serikali ya Tanzania kuwa tatizo la umeme ni suala la muda tu.

Mpaka sasa wananchi bado tunateseka hivyo natoa kauli kwa wote kuwa tuiondoe CCM madarakani kupitia kura zetu.

Tumechoka.
Hilo ccm wamelijua na ndiyo maana wamewaondoa hao waswahili wasanii na kuwaweka wachapa kazi, watoto wa wakulima kubeba zigo hilo. Hawa wachapakazi watakuwa wamelimaliza hili tatizo la mgawo wa umeme ifikapo mwezi January 2023, yaani ndani ya miezi miwili tu tangu wapewe kazi hiyo na kudhibitisha usemi wa wahenga kwamba Mzigo mzito mupe Mnyamwezi kuubeba.

Ni kweli hao wasanii wameacha doa baya kwa ccm kupoteza kura nyingi kwenye chaguzi zijazo, ambalo kwa wengi linaweza likawa siyo rahisi kulifuta unless hao wasanii watumbuliwe.
 
Hv mleta mada una akili Kweli CCM toka lini wakayoka madarakani kisa ukozefu wa umeme.
 
Mpaka sasa wananchi bado tunateseka hivyo natoa kauli kwa wote kuwa tuiondoe CCM madarakani kupitia kura zetu.

Tumechoka.
Hakuna kitu kama hicho, ingekuwa Ulaya labda!, lakini Bongo mbona tumezoea!. Kwani hii ndio mara ya kwanza?. Wengi tumezaliwa vijijini umeme tumekuja kuukutia shule!.
P
 
Imefikia point ya mhusika "kujiuzulu". Mlala hoi anategemea salon yake ili apeleke chakula nyumbani. Kilio cha walio wengi ambao ni walala "pu" , inabidi mtu kujiuzulu.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom