Mbona sielewi maisha yanavyoenda, wakuu, nyie mnaishi vipi mtaani?

Mbona sielewi maisha yanavyoenda, wakuu, nyie mnaishi vipi mtaani?

Victoire kuna tatizo kubwa sana linalotukumba na chimbuko kuu ni mfumo wetu wa elimu kwa ujumla tokea ngazi ya awali.
Hatufundishwi ili kupata maarifa ila tunafundishwa ili tuwe na uwezo wa kukariri,YES.
Leo tunamkaririsha mtoto kusoma kuandika na kuhesabu kwenye shule ya awali,then akianza shule ya msingi tunaendelea kumfundisha hadithi za kina Mkwawa, na Chief Mangungo wa Msovero. Akianza kidato cha kwanza tunamfundisha kukariri mito mirefu na milima distinguished duniani,huku tukimlazimisha kujua kiungo kimoja baada ya kingine cha panzi. Akianza kidato cha tano tunamkaririsha technique za kujibu maswali kidato cha sita mara paap yupo Elimu ya juu ambayo nako ni kumezeshwa madesa till miaka yako mitatu,minne ama mitano imalizike ulipe joho urudi mtaani bila maarifa yoyote. Matokeo yake ndio haya!
Mtoto wangu siku akifika form 4 tu namrusha kwenye ufundi
 
Tafuta laki moja hata kwa kumuomba shemeji tafuta kitaa ambapo kuko bize na hakuna usumbufu weka limeza la matunda kama ndizi au machungwa jioni then wauzie watu wanaopita eneo hilo haswa wanaotoka makazini. Hukosi elfu 10 jioni na mtaji ukikuwa unahamia biashara nyingine. Pia muda wa mchana ambapo huko free jaribu kufanya vibarua au kama kuna eneo lima bustani za mbogamboga kama mchicha matembele na pilipili za mwendokasi. Unaamka usiku kama saa 10 au 11 unamwagilia
 
Wewe dada yangu kipenzi. Mpakwa mafuta.

Itabidi nikutafute maana mengine ya nyumbani naweza kuyakosa hapa.

Kuna watu wanatembeza chupi maofisini usawa huu unavyogomba?

Say it ain't so.

Astaghafurullahi!
Wapo kabisa kaka yangu,sio chupi tu hata nguo zingine,urembo,perfume,na vitu vingine vinavyobebeka.
 
nikiwa na umri wako nilikiuwa na kitanda kizuri pamoja na godoro huku makochi yakiwa ni mbao tupu na nimepanga vyumba viwili na kaa mbagala mpenzi wangu anatoka sinza. upo hapo? lakini kipindi hicho sikuwa na degree ndo nilikuwa nafikiria kuacha kazi na kurudi shule.
maisha ni rahisi na nimagumu yapo kwa kadri wewe unavyoyachukulia.
chakwanza angalia fursa ulizo nazo na je unaziona fursa kwa kiasi gani. natamani kuongea na wewe kwa simu naweza kukushauri vizuri na ninauhakika ukiwa tayari yapo mambo yatabadilika kwako. ukiwa tayari nitaarifu
 
Simu ndio faraja yangu

Ndio rafiki yangu wa kudumu

Ndio tunapiga nae Story

Nikiuza nitakuwa nimejitoa kwenye raman
[/QUOTE]
hauko serious na hauoni ni kututukanisha kuendelea kukaa kwa shemeji.
 
andaa Kama elfu hamsini hivi, nikuelekeze ukachukue bidhaa ya dish soap, zinakaa 48, kwa shikingi 15000, so wew tembeza mtaani au weka kijiwe kwenye stend ya basi,uza kila moja 700-1000, ukimaliza mzigo wa katoni mbiki tu,unakunja 50+, hii ni fursa maana si unajua kila mtu anatumia sabuni. ukitembea Sana unaona vitu vingi Sanaa. nakutania mwayaa si unajua tena Mimi napendaga utaniii
 
Aisee! Mi mwenyewe ndo soon namalizia chuo.ila kikubwa uhai kama una mikono,miguu anything is possible ushauri wa bure omba mtaji kwa huyo shemeji uangalie interest yako ni ipi kama ni business au,unaweza kutumia ujuzi wa academic ulioupata unaweza fungua tution au omba hata mahali temporary pakufundisha hata ukiwa unalipwa elfu hamsini kwa mwezi sio mbaya.Ikishindikana vyote then bro usione haya tafuta hata kazi za ulinzi hata boda,au kama unaleseni fanya kazi ilimaadam you make anything perday! .ni ushauri wangu mi mdogo wako niko second year now.
Ukimaliza chuo ,fanyia kazi huu ushauri wako
 
Sio poa
JamiiForums-982558150.jpg
 
Back
Top Bottom