Kijana nikushauri vitu vichache kutokana na uzoefu mdogo ambao nimeupata kwa ku_run project yangu mwenyewe kwa miezi 7 saba sasa baada ya kuacha ajira.
1. Umetengeneza nini kwa ajili ya nani? Hilo ni swali la kwanza lisitoke kwenye akili yako kila unapofanya improvement ya product yako, pia hilo litakusaidia kujua content gani uweke, na upromote kwa wateja wa aina gani, zingatia kuwa sio kila mtu anaweza kuwa mteja wako so choose your niche.
2. Don't build it for money, tengeneza product inayoleta thamani kwa mteja, ukiona wateja wametumia free trial ikaisha then wakaachana na app yako hii ikupe alert kuwa hawajaona value ya kile ambacho unatoa (Yaani thamani ya unachotoa ni ndogo kuliko thamani ya pesa yake). Hivyo, jitahidi kutengeneza bidhaa yenye thamani then wateja watakuwa tayari kulipia
3. Simplicity, Inaweza kuwa ni app nzuri, ina contents nzuri lakini kama inakosa kumfanya mtumiaji aone urahisi wa kuitumia fahamu kuwa mtumiaji huyo hawezi kudumu.
4. Utofauti, Yaani mimi nikiingia kwa app yako nitapata kitu gani ambacho hakipo kwa app nyingine ambayo inatoa the same kind of service?
5. UVUMILIVU usikimbilie pesa, focus kwenye kutengeneza bidhaa bora nimeangalia play store inaonyesha umepublish app yako Mar 15, 2024, then hakuna any updates imefanyika mimi binafsi najiuliza first version ya app yako haijawa na dosari yoyote au any customization from March to May? kwa kuwa siamini kama first version inaweza kuwa stable na kukosa updates za muhimu/customization ambazo wateja wamekushauri. Hivyo wekeza muda kwenye kutafuta feedback zza wateja ambao waliitumia na kuacha ujue kwa nini wameacha kuitumia app yako, wanataka nini kiboreshwe, au waulize walipo install walitarajia kupata nini na matarajio yao hayakufikiwa. Hayo yote ni muhimu sana kwenye kuboresha product yako.
Huo ni ushauri binafsi kulingana na uzoefu mdogo ambao nimeupata kwa kusimamia project ya app yangu mwenyewe baada ya kuacha kazi, hivyo unaweza kuchanganya na akili zako kuona ni wapi uboreshe.